Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Siasa kwa nchi za Africa ni mchezo mchafu unaochezwa na washenzi na wajinga wenye mamlaka na maslahi binafsi, na kifo ni consequences and the end result.

Wajinga wasiojitambua hawapendi kukosolewa, hasa akiwa na power. Maamuzi ya mtu mjinga hayana mipaka wala reasoning. Atafanya chochote ili akunyamazishe. Especially kama ana maslahi binafsi. Then ataenda to the extremes.

Kama wewe ni Kapuku mmoja tu tena clueless kwenye maswala ya technology na internet usiyeweza kumaintain anonymousity mtandaoni. Basi huo mchezo kaa nao mbali. Hata JF humu usijiamini sana.

Alafu kweli, ngoja nitokee mlango wa uwani. Kwaherini.
 
kama tusipochukua maamuzi ya kiuwendawazimu kama wa KENYA watawala na mafala wenzao jeshi la polisi watatumaliza...taifa lipo nyuma kwa kila kitu nasi tumelala usingizi wa pono
 
Kumiliki car wash 11 mjini dsm ni ishara kwamba kijana ni mhangaikaji haswaa,kukwaruzana na watu/mtu/kampuni au taasisi ktk harakati za utafutaji ni jambo la kawaida,lakini namna ya kulihandle inategemea utashi wa aliyekwaruzwa,hasa kwa nchi zetu hizi ambzo bado zina unyani nyani bado.

Muhimu vijana ni kuwa makini ktk pilika za kila siku.
 
Huyo mbona ni marehemu siku nyingi ....hao ndugu zake wange mtafuta Rostam azizi wamuangukie na kumsujudia basi ndugu yao angelikuwa hai hadi leo
 
Unapigiwaje simu na kukimbilia kutuma pesa kiholela? Yani mume wangu anipigie simu yupo kwenye maumivu makali hiyo nguvu ya kutuma pesa nitaipata wapi badala ya kukimbilia kwa uharaka kituoni alikonitaarifu yupo kwa wakati huo?

Kwa amani ya familia kipindi hiki cha sintofahamu sidhani kama hiyo taarifa ya mpenzi wa Dodoma ilipaswa kuwekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…