Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Kutoka Ukurasa wa Boniface Jacob Mtandao wa X: SIKU 280 TANGU APOTEE ADINANI HUSSEIN MBEZI MIKONONI MWA POLISI

Maarufu kama (ADAM),umri wa miaka 32,mkazi wa Kinyerezi,mtaa wa Faru,Jimbo la Segerea,Baba wa watoto wanne.

1. Adinan Hussein Mbezi alipotea tarehe 12 September 2023 alipokuwa safarini Mwanza

2. Adinani Hussein Mbezi alizaliwa mwaka 1992 ni mfanyabiashara anaye miliki vituo 11 vya kuoshea magari Dar es saalam vya "ONE TOUCH" Pia ni mwanasiasa ambaye alishawahi kuwa CCM baadae akagombea udiwani kupitia ACT WAZALENDO uchaguzi wa 2020 kata ya Yombo Vituka.

3. Tarehe 12 September 2013 ADINANI alipiga simu kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE kumtaarifu kuwa amekamatwa na Polisi,kwamba wapo njiani kurudi Dar es saalam atamjulisha kituo watakacho mpeleka baada ya kufika Dar es saalam.

4. Tarehe 19 September 2023 ADINANI alipiga simu kwa Mama yake mlezi anayeishi maeneo ya ZOO,Chanika,Dar es saalam kwa kupitia namba ya simu 0659167082

Akimueleza Mama yake kuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Tazara,akaomba Mama yake amsaidie kumpatia namba ya Kaka yake aitwaye SAMIR HUSSEIN MBEZI

Pia aliomba Mama yake ampe taarifa rafiki yake aitwaye AMIR KHALID NASIBU (SAM) mwenye namba za simu 0711959432
ambaye amekuwa akishirikiana na familia katika kumfuatilia ADINANI kwa kila hatua.

5. ADINANI alijitahidi sana kufanya mawasiliano na ndugu zake kila kituo alichokuwa anapelekwa Jijini Dar es saalam tangu akamatwe Mwanza.

Alipiga simu akiwa Central Police Station,alipiga simu akiwa Kituo cha polisi Stakishari na simu ya mwisho alipiga kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE akiwa Tazara kupitia simu ya Polisi nambari 0659167082

Sasa akimtaarifu mke wake kuwa amepigwa sana,anahali mbaya ambayo mke wake aligundua hali ya mme wake kuwa yupo katika mateso

ADINANI aliomba mke wake atume kiasi cha Shillingi laki 5 katika namba 0659167082 ambayo alisema namba ya simu ya Polisi aliyekuwa naye wakati huo,kwa ahadi ya kiasi hicho kingesaidia asiendelee kuteswa zaidi.

Mke wake ROSEMERRY MASSAWE alitekeleza ombi la mume wake kwa kutuma laki tano.

6. Ndugu wa ADINANI walifika kituo cha Polisi Tazara,ambapo afande Kaduma mwenye namba 0757078736 alikana kumshikilia ADINANI kituo cha Tazara

Mwisho walienda Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo walielekezwa waende Kituo cha polisi kati ofisi ya ZCO kandaa maalum DSM,kumuuliza Afande Mafwele kuhusu ndugu yao kushikiliwa na Polisi

ZCO Mafwele alikana kumshikilia ADINANI,aliwatolea orodha ya mahabusu wanaoshikiliwa kituoni pale, Jina la ndugu yao halikuwemo katika orodha ya mahabusu.

Pia aliwataarifu kuwa na wao Kanda maalum ya Dar es saalam wanamtafuta ADINANI kama mtuhumiwa,wakimpata wataitaarifu familia yake.

7. Ndugu wa ADINANI katika kumtafuta ndugu yao walifanikiwa kuonana na Kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi,ambaye aliwathibitishia kuwa ndugu yao yupo Kituo cha Polisi Tazara,aliomba kiasi cha shillingi million 10 ilikuwasaidia kumaliza sakata la ndugu yao,

Ndugu walitoa kiasi cha shillingi million 10 kupitia dereva wake,lakini baada ya kutoa kiasi hicho,Kigogo huyo aligeuka kuwapa jibu kumbe ni majina tu ndiyo yanafanana,lakini ndugu yenu hayupo kituo cha polisi Tazara

8. Baada ya siku kadhaa kupita ndugu wa ADINANI walipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari wa Kituo cha polisi Mburahati kupitia namba ya simu 0713440820

Askari huyo aliwaeleza Kuwa ADINANI yupo Kituo cha Polisi Mburahati na hali yake ni mbaya sana.
Askari huyo aliomba watumiwe kiasi cha Millioni 2 na laki 5 ili wasiendelee kumuadhibu na kumpa mateso ndugu yao.

Ndugu walipotuma shillingi million mbili na laki tano simu hiyo haikuwahi kupatikana tena.

9. ADINANI alikuwa na mpenzi wake mwingine Dodoma,ADINANI alimpigia mpenzi wake huyo kumjulisha kuwa amekamatwa na Polisi na kumtaarifu kuwa kama anamtafuta amtafute kupitia rafiki yake mwenye namba 0742866092

Alipompigia mtu huyo alikata simu ya kawaida akapiga video call na kuwataarifu ADINANI hayupo tena Duniani

10. Gari ya ADINANI yenye usajili T146 DPY imeonekana kituo cha Polisi Selander bridge.


View attachment 3040943
Kila ubaya utalipwa
 
siku yaja watalia na kusaga meno wakitamani siku zirudi nyuma wasitende waliyoyatenda ila haitawezekana

Kiburi cha mtu ni uzima, mali na madaraka ila vyote huisha.

Siku ghadhabu ikiwaka juu ya hao watu risasi haijawahi kutuliza wala kuogofya!

Binadam mtu hatari sana anakuwa anakuchora tu.
Siki upi wakati tunakuwa sana maboya? hakuna kulia na kusaga meno kama tunaendelea kuwa mazezeta
 
Raisi lazima ni benefisiary wa huu utekaji yeye sio mjinga, Police wanao teka wana Back up kutoka juu, wao sio wajinga kiasi hicho.

Watu wanalaumu sana Police ila ukweli ni kwamba hakuna Police kichaa watafanya vitu kama hivi bila kwanza kuwa na Back up, wanajua mziki wa kufanya vitu kama hivi kwa utashi wao wenyewe
 
Ukiona watoto wa simba wanacheza wenyewe jirani na kichaka, jua kabisa Mama yao na Baba yao wako ndani ya kichaka wametulia tuli kabisa. Hawa watoto wa simba bila wazazi wao kuwa ndani ya kichaka hawawezi kamwe kucheza cheza nje make wanaweza fanywa mbaya na Predetor wengine kama Chui na Fisi au Mbwa mwitu.

So Police sio wajinga kwenye utekaji,
 
Ukiona watoto wa simba wanacheza wenyewe jirani na kichaka, jua kabisa Mama yao na Baba yao wako ndani ya kichaka wametulia tuli kabisa. Hawa watoto wa simba bila wazazi wao kuwa ndani ya kichaka hawawezi kamwe kucheza cheza nje make wanaweza fanywa mbaya na Predetor wengine kama Chui na Fisi au Mbwa mwitu.

So Police sio wajinga kwenye utekaji,
naam wana baraka.
 
Is Magufuli alive or died? Some one said we won’t hear some body missing or abducted becuse Magufuli is dead….
What went wrong my people?
 
Intelegensia inanituma hivi, hapa kuna kisasi, hasa hasa, " Sio kangangania mke wa mtu mwenye wadhifa mkubwa kweli?, sio kila issue ni ya kisiasa yapo ya visasi kwa wenye nyadhifa zao!
-Siku hizi watu hawasemi tena utanijua mimi nani?, zama zimegeuka na kuwa Action! 😈
Kila siku mntatetea mpaka ikufikie ndio utajua uchungu ulivyo. Eti mke wa Mtu. Kila Mtu akitekwa ni mke wa Mtu. Ok
 
Siku hizi ukiwa jambazi hasa wa kutumia silaha, polisi wanamalizana na ww mapema sana...

Huyu jamaa ndugu waseme kwa nini alienda kukamatiwa mwanza? Mwanza alifuata nini!
Acheni kutetea ujinga. Kama kakamatwa Mwanza ndio auawe? Tena kwa kufichwa?
 
Zitto Kabwe alienda kwa rais akapewa pesa za matibabu kwa Sativa, aende Tena kwa rais amwulize kuhusu huyo ndugu au anasubiri mpaka aokotwe ajifanye shujaa.
 
Swali langu dogo tu. Kwanini ndugu zake walikuwa wepesi sana kutuma pesa ili ndugu yao aachiwe. Na pesa zinatumwa kiholela tu. Je walikuwa wanajua nini juu au wanajua nini juu ya ndugu yao.
 
Unapigiwaje simu na kukimbilia kutuma pesa kiholela? Yani mume wangu anipigie simu yupo kwenye maumivu makali hiyo nguvu ya kutuma pesa nitaipata wapi badala ya kukimbilia kwa uharaka kituoni alikonitaarifu yupo kwa wakati huo?

Kwa amani ya familia kipindi hiki cha sintofahamu sidhani kama hiyo taarifa ya mpenzi wa Dodoma ilipaswa kuwekwa.
Nyumbu unadhani Wana akili!!..hawajui kipi waseme kipi wasiseme,eti mpenzi wake wa Dodoma!!,lingeandika rafiki yake wa Dodoma lingepungua nini!?..linataka mke amlaani mumewe!!?
 
Gari ya ADINANI yenye usajili T146 DPY imeonekana kituo cha Polisi Selander bridge.
Hii gari nimeangalia kwenye website ya polisi inaonekana ipo barabarani inaendeshwa na mara ya mwisho imepigwa fine tarehe 10/07/2024 na namba ya leseni ya dereva aliyekuwa anaendesha inaonekana.
 

Attachments

Huyo mbona ni marehemu siku nyingi ....hao ndugu zake wange mtafuta Rostam azizi wamuangukie na kumsujudia basi ndugu yao angelikuwa hai hadi leo
Kwanini Rostam Aziz?
 
Back
Top Bottom