Ado: Serikali ikibaini madini, Wananchi wapewe kipaumbele, Wachimbaji wadogo wasifukuzwe "hii ni nchi yao!”

Ado: Serikali ikibaini madini, Wananchi wapewe kipaumbele, Wachimbaji wadogo wasifukuzwe "hii ni nchi yao!”

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mbunge Ado Shaibu Ado akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Kijiji cha Ngapa, Kata ya Wilaya ya Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma amesema Wananchi walipogundua madini na kuanza kuchimba kama wachimbaji wadogo, Serikali badala ya kuwawezesha kwa teknolojia na mitaji ili faida ibaki ndani, inaenda kumtafuta mwekezaji mmoja anayewafukuza wachimbaji wadogo na wenye mashamba bila fidia inayoeleweka.

Ametoa wito kwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kufanya uchunguzi maalum juu ya mwekezaji, mikataba ilivyofanyika na kama wananchi, serikali ya kijiji na kata walishirikishwa.
 
Wazee wa kujitekenya na kucheka wenyewe.

Kwamba hadi mchakato wa kupata mwekezaji na ulipaji wa fidia za hovyo unakamilka, mbunge na diwani hawajui??

Walishawageuza wananchikama masaveya wao wa madini wakipata yalipo wanakuja na fieldfoce.
 
Back
Top Bottom