Uchaguzi 2020 Ado Shaibu: ACT kumsimamisha Membe iwapo atatimiza vigezo vinavyotakiwa

Uchaguzi 2020 Ado Shaibu: ACT kumsimamisha Membe iwapo atatimiza vigezo vinavyotakiwa

Mkuu sijui unafikiriaje kuhusu siasa! Kumbuka alipofukuzwa ccm ni sababu za kisiasa vilevile"

Kwamba tofauti iliotokea kati yake na wanaccm wenzie ndo upinzani wenyewe,
hivo ni sahihi kwake kutafuta chama chenye sera zinazoendana na msimamo wake.
Usiumize kichwa mkuu hama hama ndo siasa zenyewe!

Sisi tunatakiwa tupigie kura sera za chama, na si kupigia chama flani"

Kuna haja hawa wanaojiita wapinzani wakae chini na kujitafakari. Wanaishi maisha ya kukariri sana. Wanarudia makosa hayo hayo kwa kutarajia matokeo tofauti. Ni kama vile mtu kujua kuwa njia unayopita ina shimo na ulishawahi kutumbukia lakini bado unapita hapo hapo kwa matumaini ya kuwa labda shimo litakuwa limejifukia.

Inafikirisha pia kuona hao hao wapinzani wanatarajia watu kutoka chama tawala ndio wanaofaa zaidi kuwa wagombea wa vyama vyao. Hili linapelekea kwenye fikra, kuwa wao kama wao hawana uwezo wa kuongoza wala kusimamia kile wanachokihubiri na kuwa chama tawala ndio bora katika kutoa watawala.

Ifike kipindi kina Zitto wasimame wenyewe kwenye kugombea uraisi hata kama wakijua watashindwa kuliko kutegemea makapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mi natamani ACT watuletee membe, patakuwa hapatoshi!
Membe siyo CCM, Membe ni mwananchi huru
Kudhani Membe ni CCM ni sawa na kudai kuwa Maalim Seif ni CCM eti kwa sababu naye amewahi kuwa CCM. By the way maalim Seif na Membe wote wanashare characteristic moja, Wote walifukuzwa CCM.

Ado ameongea vizuri kuwa kama Membe atafikia vigezo basi agombee kupitia ACT, mimi. naunga mkono asilimia mia kwa mia kwanza
1. Kitendo cha Membe kusimama against JPM tangu akiwa ndani ya CCM ni kitendo cha kishujaa sana, maana yake anajiamini na yuko tayari kupambana ili kuwasaidia watanzania dhidi ya utawala dhalimu wa sasa wa CCM

2. Pili Membe amepikwa kiuongozi ameiva, CV yake ni nzuri, ana sifa nzuri sana za uongozi, ana exposure na siyo katili

3. Membe ni mwanadiplomasia makini, anaamini katika demokrasia, amejiandaa kwenye uraisi, hakurupuki kuutaka uraisi. Kiufupi yuko vizuri kulinganisha na mtawala wa sasa.

ACT tuleleteeni Membe, msirudi nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wasingempokea lowasa na hata wangeshindwa bila lowasa bado wanachama wengi wangekuwa na imani,chadema ilikuwa inakabili vitu viwili 2015 ,either lowasa ashinde ,na asiposhinda imani ya wanachama kupungua
Mkuu nadhani maamuzi yao yalikuwa sahihi sababu wananchi walikuwa ba common enemy hivyo yeyote aliyepambana na CCM ni lazima muungane.

CUF walikua CCM-B sababu walikua SUK, NCCR nayo CCM B sababu ya uteuzi wa Mbatia n.k ila waliungana licha ya tofauti zao hizo.

Kwahiyo hakuna imani iliyoshuka ndio maana kura ziliweka rekodiotherwise wangemkataa wazi wazi kma Dr Makaidi kule Mtwara.

Kilichoidhoofu CHADEMA ni kuzuia mikutano,Bunge kuwa gizani, nguvu ya dola kuwakatisha tamaa, Lissu kupigwa risasi iliwaziba midomo wale wajasiri n.k kwahyo ikitokea CHADEMA imekufa ni sababu ya hujuma za TISS sio ujio wa Lowassa au udhaifu wa Mbowe.

Ndio maana tukasema mazingira ya kisiasa yaleyale yangeachwa alafu CHADEMA ikose wanachama ndio mngekua na hoja. Ssa mnawabana kila siku kesi, no operation sangara,M4C n.k alafu mnasema Mbowe kaua chama.

Kma hya ndio mawazo ya wananchi wote TZ basi tuna safari ndefu sana ya kuamka kifikra.
 
Tatizo la cdm Ni kutojiamini tu,,kisiasa kuhama vyama ndo siasa zenyewe hizo,,lowasa aliwainua Sana cdm,ila kura hazikutosha,,so haina maana Sasa eti ndo inekuwa dhambi kuchukua wageni na kuwapa ugombea,,mbona hata CCM wanachukua kina waitara na kuwapa ugombea?,siasa Ni game na ili ushinde lazima uwe,Master of the Game
Umeongea point nzuri sana lakini uneshindwa kujua kitu kimoja mbinu za ccm za kuwachukuwa wapinzani ni tofauti kidogo na za chadema.. Kosa walilofanya chadema ni kwamba bado chadema ilikua inajenga uaminifu kwa watanzania lkn kwa upeo mdogo waviongozi wakshindwa kujua kwamba ilkua inahitaji miaka km ishirini mbele kuichukua nchi ndio wakaamini wakimchukua lowasa wangechukua nchi. Chadema bado walkua na fursa ya kuongeza namba ya wabunge na madiwani katika hali ya uaminifu kwa wananchi wake ili pia ikaweze kubadili baadhi ya sheria kandamili km ya tume ya uchaguzi. Ccm kwa sababu tayari wanadola ht km hawana uaminifu wananguvu ya kupambana coz tayar wanao kundi la kuwalinda kwa maana ya polisi, tume ya uchaguzi, jeshi, mahakama, fedha n.k. Angalia pia tofauti ya ccm na chadema, ccm wao wanapoteza mmoja wanavuna kumi. Kazi ni ndefu sn kwa upinzani tanzania
 
Ukweli ni kwamba hata CDM wapo tayari kumpa hiyo nafasi Membe akiitaka tena bila hata masharti.

Halafu hawaoni kama kilichofanyika kwa Lowasa ni makosa bali ndo siasa zenyewe hizo.
 
ACT wazalendo imebainisha msimamo wake kuhusu uwezekano wa kumsimamisha Bernad Membe nafasi ya kugombea Urais iwapo atajiunga na kutumiza vigezo vinavyotakiwa,hayo yamesema na katibu mkuu wa ACT wazalendo Ado Shaibu alipozungumza na Nipashe.

Naona ACT wanafanya kosa lile lile waliyofanya chadema,hivi vyama vya upinzani vimekuwa takataka ya wagombea wanaowekwa dustbin kule CCM
Kigezo si kujiunga tu? Kuna kingine zaidi ya hicho?
 
Chadema bila lowasa hata wangeshindwa watu wangekuwa bado wanaimani sana maana hamna wale mafisadi ambao waliwatukana hawapo kwenye chama ,na hata mwaka huu wangeingia wabunge wengi wa chadema (wabunge wangeongezeka),ila huu uchaguzi wa mwaka huu chadema inaonekana kupoteza au kurudi namba zile zile
Umeongea point nzuri sana lakini uneshindwa kujua kitu kimoja mbinu za ccm za kuwachukuwa wapinzani ni tofauti kidogo na za chadema.. Kosa walilofanya chadema ni kwamba bado chadema ilikua inajenga uaminifu kwa watanzania lkn kwa upeo mdogo waviongozi wakshindwa kujua kwamba ilkua inahitaji miaka km ishirini mbele kuichukua nchi ndio wakaamini wakimchukua lowasa wangechukua nchi. Chadema bado walkua na fursa ya kuongeza namba ya wabunge na madiwani katika hali ya uaminifu kwa wananchi wake ili pia ikaweze kubadili baadhi ya sheria kandamili km ya tume ya uchaguzi. Ccm kwa sababu tayari wanadola ht km hawana uaminifu wananguvu ya kupambana coz tayar wanao kundi la kuwalinda kwa maana ya polisi, tume ya uchaguzi, jeshi, mahakama, fedha n.k. Angalia pia tofauti ya ccm na chadema, ccm wao wanapoteza mmoja wanavuna kumi. Kazi ni ndefu sn kwa upinzani tanzania
 
Back
Top Bottom