Ado Shaibu ahoji kuhusu utekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Namiungo wilayani Tunduru

Ado Shaibu ahoji kuhusu utekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Namiungo wilayani Tunduru

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amehoji hatua zinazochukuliwa na Serikali kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Namiungo wilayani Tunduru, akisema ahadi hiyo ilitolewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Ado amesema Kata ya Namiungo ina vijiji saba na idadi kubwa ya wananchi, hivyo inahitaji huduma bora za afya na inapaswa kupewa kipaumbele katika mipango ya Serikali.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa TAMISEMI, Prof. Shemdoe, amesema Serikali inatambua ukubwa wa Kata ya Namiungo na mahitaji ya wananchi wake, huku ikitafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Awali, Ado amesema ameondoa hoja yake ya kuomba mwongozo wa Spika kuhusu hatma ya vituo vya afya vya kimkakati, baada ya Serikali kupeleka fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kimkakati Nampungu, ambacho ndicho alichokuwa akikiombea mwongozo wa Spika.
 
Back
Top Bottom