Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema chama hicho kitampa nafasi mtu yeyote atakayehamia kuweza kugombea nafasi ya Urais.
Ado amesema taratibu za chama hicho zinasema mtu akishakuwa mwanachama anaruhusiwa kutangaza nia na taratibu zingine za usaili zikifanyika na zikampitisha basi ataweza kuwa Mgombea Urais.
"Mimi nina imani hata sasa kwa wapiganaji wengi wakifanya uchambuzi wa jukwaa mbadala katika mapambano bila shaka jibu litakuwa ACT Wazalendo tutawapa nafasi ya kugombea Urais, urais ni haki ya mwanachama kila mwanachama anaruhusiwa kutangaza nia" amesema Ado