Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema chama chao cha ACT Wazalendo kingekuwa kimefanya kosa la kimkakati ikiwa wangesusa kushiriki uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, wakieleza kuwa kwasasa timu yao ya wanasheria wanajiandaa kufungua Kesi mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vya sheria na kanuni za Maadili ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza kwenye kipindi cha Kinagaubaga kinachorushwa na idhaa ya kiswahili ya Ujerumani (DW) leo Aprili 15, 2025, Shaibu ameeleza kuwa eneo jingine linalopaswa kupewa kipaumbele na vyama vinavyopingana na baadhi ya sheria na mifumo ya uchaguzi ni pamoja na kuhamasisha Jamii kuungana nao katika kudai Katiba mpya itakayokuwa na mifumo ya haki na uhuru katika chaguzi za kisiasa zitakazokuwa zinafanyika nchini.
Akizungumzia hoja ya Viongozi wa CCM kudai kuwa muda umeisha wa kufanya mabadiliko ya sheria za uchaguzi, Ado ameieleza idhaa hiyo ya kiswahili kuwa bado upo uwezekano wa kupeleka bungeni ajenda maalum ya marekebisho ya sheria na mifumo ya uchaguzi ikiwa tu dhamira hiyo itabebwa na serikali iliyopo madarakani.
Ado Shaibu ameiambia Dw kwamba Chama chao hakitokata tamaa katika kudai mabadiliko ya sheria, akieleza kuwa kutofautiana njia za kudai haki hiyo kati ya ACT Wazalendo na Chama cha Demokrasia na maendeleo ambao malalamiko na hoja zao zimefanana, hakuathiri chochote kwani tayari walishakaa kikao na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu na kukubaliana baadhi ya mikakati katika kudai mifumo huru, yenye usawa na haki katika kusimamia chaguzi za kisiasa.
See translation
Source: Jambo Tv