Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu Ado, ameikosoa vikali CCM kwa ukimya wake kuhusu madai ya kutekwa kwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho na Balozi wa Tanzania, Humphrey Polepole, akidai hatua hiyo inaonesha unafiki wa kisiasa na kudhoofisha matumaini ya wananchi kupata utetezi kutoka kwa viongozi wao.
Ado alitoa kauli hiyo jana, Juni 14, 2026, jijini Dar es Salaam, alipohutubia mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliofika katika Makao Makuu ya ACT-Wazalendo kuchukua kadi na kujiunga rasmi na chama hicho.
Pia soma > Humphrey Polepole atekwa usiku wa kuamkia leo Oktoba 6
---
"Na mimi nawaambia wana CCM, kama nyinyi mnashindwa kumtetea mwana CCM mwenzenu, ambayo ni ishara ya juu ya unafiki—yaani nyinyi mnajua mwenzenu katekwa, na huyu mwenzenu alikuwa balozi, alikuwa msemaji wa chama, mjumbe wa kamati kuu—mpaka leo hakuna statement yoyote ya CCM kulaani jambo lile?
Mimi nilimtarajia katibu mkuu wa CCM, Balozi Migiro, kweli kwa kuishi Umoja wa Mataifa, kukaa kwenye chombo chenye dhamana ya haki za binadamu duniani, nilidhani yeye ataleta nafuu kidogo. Kumbe CCM bwana, ukishaingia kule ndani, hata uwe na nafuu gani, na wewe unakuwa kwisha habari yako!
Leo hii hakuna kauli ya Balozi Migiro, hakuna kauli yoyote kupinga kutekwa kwa Humphrey Polepole."