PreGE2025 Ado Shaibu: Tukikaa kimya CHADEMA ikiumizwa, tutafuata sisi ACT

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakiwezi kunyamaza kimya endapo CHADEMA itakandamizwa, kikisisitiza mshikamano wake na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Akizungumza katika kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema chama chake hakiwezi kufumbia macho matukio yanayoikumba CHADEMA, ikiwemo kuzuiwa kwa mikutano yao na kutoweka kwa baadhi ya viongozi wao.

Pia soma Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Baadhi ya watu wametuhoji kwa nini ACT inakuwa sauti ya CHADEMA. Leo nataka niwaambie Wanakilwa, ikiumizwa CHADEMA tukakaa kimya, anayefuata ni nani? Ni sisi ACT Wazalendo. Ikiumizwa CHADEMA tuchukulie kwamba tumeumizwa na sisi," amesema Shaibu.

Akiendelea kusisitiza mshikamano huo, amesema ACT Wazalendo inachukizwa na jeshi la polisi kwa kile alichokiita upendeleo wa wazi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa mikutano ya chama tawala hupewa ulinzi mkubwa kwa kusindikizwa na gari za polisi, huku mikutano ya upinzani ikizuiwa.

"Tunafahamu viongozi wao wawili hawaonekani mpaka sasa katika kipindi cha wiki chache zilizopita. Tunafahamu pia kuwa jeshi la polisi limezuia mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliopangwa kufanyika Machi 25, 2025, kule Mbarali, Mbeya. Ninawaambia ndugu zetu wa CHADEMA tupo pamoja, tutashirikiana, na tunalionya jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa ubaguzi. Kwa nini CCM wanapewa mpaka magari ya polisi yanasomba watu kwenye mikutano yao, lakini mikutano ya upinzani inawekewa vikwazo?" amehoji.
 
Huu ndio upinzani sasa
 
Sijui kwa nini huwa napata ukakasi kuamini kwamba ACT ni Chama cha upinzani.
 
Oparesheni LINDA DEMOKRASIA ya ACT WAZALENDO na NO REFORMS NO ELECTION ya CHADEMA ni Oparesheni muhimu sana kwenda kuwaeleza Wananchi wapigakura jinsi CCM inavyopora Kura zao.
 
Wao ACT hawawezi kuumizwa, mtu anaumizaje mtoto wake?
ZZK lini amewahi hata kulala sero katika harakati zake?
 
Yuko sawa, mtetezi wa haki anapaswa kumtetea yeyote anayekandamizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…