McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amedai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina dhamira ya kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, akisema hadi sasa hakuna hatua zozote zinazoonyesha utekelezaji wa ahadi iliyotolewa kuhusu kuanza kwa mchakato huo.
"Sasa mimi nawauliza, tangu tuapishwe mwezi wa 11 mwaka jana mpaka leo imepita miezi mingapi? Miezi saba ama nane, au sio? Miezi nane. Mchakato wa katiba umeanza? (Watazamaji: Haujaanza) Haujaanza!
Lakini nyinyi mkiwa watu wa kuridhika kwa maneno mepesi, mtamsikiliza Waziri Omeira kwa kila alichokisema juu ya katiba. Anasema CCM imeweka kwenye ilani yake ahadi ya katiba mpya. Lakini ukweli ni kwamba CCM haitaki katiba mpya hata kidogo. Katiba mpya inaitisha CCM. CCM ikisikia neno katiba mpya huwa inaona kama itaondoka madarakani. Na mara zote kazi ya CCM ni kuhujumu mchakato wa katiba mpya.
Wamefanya kazi hiyo tangu ilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Nyalali miaka ya 90. Hivi sasa wamebuni mbinu mpya. Wameona tukiipinga katiba mpya kwa sababu Watanzania wanataka katiba mpya, tutakwama. Mbinu mpya waliyoamua kuja nayo, wameamua na wao wajifanye wanaitaka katiba mpya—kama mbinu ya kuihujumu, kuchelewesha michakato, kuchelewesha taratibu"