LGE2024 Ado Shaibu: Wasimamizi wa vituo vya uandikishaji wapiga kura kuwanyima mawakala kujua idadi ya waliojiandikisha ni bomu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Katibu Mkuu chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwa utaratibu wa wasimamizi wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kuwanyima mawakala haki ya kujua idadi (orodha) ya wapiga kura waliojiandikisha siku husika ni bomu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Ado amayasema hayo leo Jumapili Oktoba 13, 2024 kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Ado ameongeza kuwa hali hiyo inafanya mawakala wanaonekana kama vikaragosi kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Soma Pia: ACT Wazalendo: Mawakala wa Vyama vya Siasa wanalazimishwa kwenda kuapa Halmashauri ambako ni mbali na maeneo wanayotoka
 
ni kweli hao mawakala watakua kama vikatagosi tu kwasasabu hakuna haja ya wao kuwapo humo vituoni. Ingependeza zaidi wawepo siku ya uchaguzi..

ila dar bana duh 🤣
 
Nasisitiza tena, Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hayo yanayoendelea humo ndio ushahidi wenyewe. Mara nyingi mambo haya huisha baaada ya machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi.
 
Tuwe wakweli,
Wakala yupo,wanaoandikishwa anawaona,anaijua kusoma na kuandika,anashindwa kuwahesabu kweli ikifika saa kumi na mbili? Si waende na notebook na wao wawe wanakkeep record? Tatizo liko wapi?
Tuache kulalamika wakati suluhu zipo
 
Katibu Mkuu chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwa utaratibu wa wasimamizi wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kuwanyima mawakala haki ya kujua idadi (orodha) ya wapiga kura waliojiandikisha siku husika ni bomu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Ado amayasema hayo leo Jumapili Oktoba 13, 2024 kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Ado ameongeza kuwa hali hiyo inafanya mawakala wanaonekana kama vikaragosi kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Soma Pia: ACT Wazalendo: Mawakala wa Vyama vya Siasa wanalazimishwa kwenda kuapa Halmashauri ambako ni mbali na maeneo wanayotoka

Wapinzani ltalia lia mpaka lini ?
Hamjiongezi tu ?
Yaani uchaguzi wa Serikali za mitaa ni uchaguzi mwepesi sana kuwadhibiti wazee ambao hajui chochote kuhusu hii CCM ya wauaji na mafisadi .

Yaani wazee kweli wanawashinda vijana wa ACT na Chadema kuwadhibiti ?
Vijana wa kizazi hiki ni hovyo kabisa.

CCM walishasema hawamjali hata Mungu ,apende asipende wao ushindi ni lazima .
Mtu asiyemuogopa Mungu unalhurumia vipi ?
Hawa CCM ni sawa na Manefili wakati enzi za zamani waliomuasi Mungu .
Yalikua ni majitu katili sana kwa binadamu kwa sababu yalikua na nguvu sana . Hata hivyo Jitu la mwisho liliuawa na Kijana mdogo Daudi kwa kupigwa jiwe.
Daudi hakuwa na huruma na kitu lilikua linamtukana Mungu .
Sasa ACT na Chadema wao wanakimbilia kwenye mitandao kwa kuamini kuwa kila mmoja anaweza kuishinda CCM peke yake.

Rushwa ni kitu kibaya sana .
Pesa za Bandari zilikuwa na watu wengi sana wakiwemo baadhi ya wapinzani wakidhani kuwa wanamkoloa Tundu Lisu na Mwabukusi na Mpina . Sasa leo hii mnalia lia badala ya kushirikiana kumdhibiti Mhalifu kwa nguvu ya kadiri anavyokuja .
Hao wanao kataa kutoa orodha ni kwa mujibu wa sheria au ni ukada na uchawa unaotumika ?
Kama ni uchawa basi chawa anapigwa pasi tu na kuondoka na mayai yake .

Huu uchaguzi ulitakiwa uwe ama ufuate utaratibu au usifanyike mpaka Katiba mpya hata ikiwa ni 2030 kuliko kupotezana muda na vyama vyenye wasanii na wajanjanja .

ACT ilijisahau kuwa CCM linapokuja suala la Madaraka ni bora ukutani na Shetani maana anamwogopa Mungu sana mapaka anatetemeka lakini sio maCCM.

Waislam na wakristo waliopo ACT msikubali kuipigia kura CCM maana CCM ikishinda basi kwenda kwenu Misikitini na makanisani ni bure kabisa ni bora kabisa watu wa Korea kaskazini wasio na dini za Kumwamini Mungu muumba mwenye kutoa pumzi ya uhai na mwenye kusimamia Haki kwa kila mtu .
Kushinda kwa CCM ni sawa na kushindwa kwa Mungu aliyeumba vitu vyote na hii nchi Simia Mchengerwa watakua ni maarufu na wakuu kuliko Mungu .
Kama wetu wanasujudu na kugalagala mbele ya Rais Samia huku wakimwomba Rehema na ufadhili na kumsifu kuliko Mungu basi ni wazi kuwa akishinda tena na CCM yake basi imani zitadharauliwa sana na machawa watajikweza sana na Samia ataitwa kila jina zuri kuliko Mwenyezi Mungu. Hii hakika ni shirki.
Tunataka watawala watakao heshimu wetu na kumwogopa Mwenyezi Mungu kuliko vitu vyote.

CCM wameanza kuchana watu na viwembe wakati wanaomba kura ili watuongoze.

Sasa hatutumii akili tu kuwa hawa wetu ni makatili na hawafai kabisa kukaa kwenye ofisi za umma.
Mtu anaomba kura kwa kupiga watu na hila halafu bado pakatokea Muumini wa Kikristo au kiislam anamchagua, halafu siku za Ijumaa na Jumapili wamejaa makanisani wanaomba Mungu nchi iwe na neema na mvua ya kiasi . Itakua ni sawa na kumkejeli Mungu.

Kumbukeni kauli hii ya kidhalimu na Kufru kubwa kwa Mungu," CCM kushinda hakuna cha Mungu akipenda " Mungu apende asipende CCM Ushindi ni lazima ".

Haya makufuru ni makubwa mno wamejihakilishia maisha na uhai kama vile wao ndio watoa pumzi na waweka pumzi.

CCM mnaweza kutoa pumzi za watu kwa kuua lakini kamwe hamwezi kumpa mtu pumzi ya uhai.

ACT na Chadema kaeni pamoja muweke tofauti zenu kwenye huu uchaguzi .Uchaguzi huu ndio wakuona mapungufu ya wagombea wenu wasiofaa na wanaofaa , waaminifu na wasio waaminifu . Ili uchaguzi mkuu uwe rahisi na muwe na wapiga kampeni kuanzia ngazi za chini kabisa.

Mkigombania fito na kugawana vikura vya serikali za mitaa basi uchaguzi mkuu utakua mgumu sana maana itakua ni rahisi sana kuibiwa kura zinazohesabiwa na tume na kutangazwa bila mtangazaji kuweza kumdhibiti endapo atajaribu kubadili kura.
 
Wapinzani wanapolalamika hivi Sasa nawashangaa. Kwani walitegemea nn?

Walipaswa kupambania katiba mpya na tume huru. Kwakuwa imeshindikana kuvipata basi hawakupaswa kushiriki chaguzi hizi.
Kwani wewe,huhitaji katiba mpya??
 
Katibu Mkuu chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwa utaratibu wa wasimamizi wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kuwanyima mawakala haki ya kujua idadi (orodha) ya wapiga kura waliojiandikisha siku husika ni bomu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Ado amayasema hayo leo Jumapili Oktoba 13, 2024 kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Ado ameongeza kuwa hali hiyo inafanya mawakala wanaonekana kama vikaragosi kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Soma Pia: ACT Wazalendo: Mawakala wa Vyama vya Siasa wanalazimishwa kwenda kuapa Halmashauri ambako ni mbali na maeneo wanayotoka
Sheria hairuhusu kutoa takwimu za serikali kwa mamlaka isiyo husika , haiwezekani takwimu za walio jiandikisha apewe wakala wakati wakati sio mamlaka inayo paswa kupewa taarifa, taarifa inatakiwa kutolewa kwenye mamlaka husika na wao wakizitaka watazipata huko upinzani acheni ujuaji wa kijinga. Over
 
Tuwe wakweli,
Wakala yupo,wanaoandikishwa anawaona,anaijua kusoma na kuandika,anashindwa kuwahesabu kweli ikifika saa kumi na mbili? Si waende na notebook na wao wawe wanakkeep record? Tatizo liko wapi?
Tuache kulalamika wakati suluhu zipo
Uko sahihi
 
Wapinzani wanapolalamika hivi Sasa nawashangaa. Kwani walitegemea nn?

Walipaswa kupambania katiba mpya na tume huru. Kwakuwa imeshindikana kuvipata basi hawakupaswa kushiriki chaguzi hizi.
Ni wachumia tumbo tu hapo wapo kazini kama kazi nyingine mm upinzani wa tanzania sio wa kuuamini isee..ni wachumia tumbo
 
Back
Top Bottom