Naona umetoka Jukwaa la siasa sikukujibu, umenifuata huku. Naona sasa unatafuta sana kujibiwa na mimi. Haya ngoa nikijibu kitaalamu tu:
Mosi,
Hakuna Super power isiyokuwa na ushawishi katika siasa, uchumi na tamadumi za mataifa mengine duniani. Umelitazama hili katika mawazo butu mnoo: Nchi kubwa kama Marekani haiihitaji kutawala mipaka yote ya dunia ili tuseme linatawala dunia,...kwenye sayansi ya siasa kuna kitu wanakiita Hegemonic Power.
Ambapo taifa moja kubwa halitawali taifa jingine moja kwa moja bali kwa kupitia ushawishi. Mfano mzuri tu, Dola la Rumi halikuwa na mipaka dunia yote lakini lilikuwa na maamuzi mazito kiuchumi, kibiashara na kitamaduni kwa karibia mataifa mengi sana duniani. Hapa naongelea Civilised Nations of Europe, Asia, Africa and Central Asia.
Kipindi cha vita Baridi Kulikuwa na kitu kinaitwa Structural Theory of The Balance of Power. Dunia nzima iligawanywa katika kambi mbili kuu. Ile ya Wakilomunisti chini ya Urusi na Ile wabeapari chini ya Wamarekani.
Warusi na Warekani hawakufika Tanzania lakini maamuzi ya Moscow au Washington yalikuwa yanaathiri maisha yetu kiuchumi, kisiasa na kitamaduni. (This is purely hegemonial influence)
Pili,
Kama unajua kabisa Hitler alitaka kuunganisha Ulaya kama Dola la Mrumi basi nilitegemea kwamba ungejua kwamba Ulaya iliyo chini ya The Third Reich ndiyo ingetawala dunia.
Ni lazima ujue kwamba kama Hitler angempiga Urusi kwenye The Great Patriotic War 1941-1945 basi leo hii yeye angetawala dunia kwasababu kusingekuwa na mtu wa kumpinga kimaamuzi hapa duniani.
Kitabu cha The Rise and Fall of the Third Reich kiliandikwa na maprofessa wa Marekani ambao walipewa ruhusu kupitia nyaraka zaidi ya 30000 za Wanazi zinasema kwamba Hitler aliwadanganya Wajapani wajiunge naye na akawa anawaza baada ya kupiga Ulaya avamie Japan au The Empire of the rising sun.
Hebu pitia vizuri mambo kabla ya kuleta ubishi mkuu.
Tatu,
Umeshau ukweli wa muhimu sana ambao unathibitisha kwamba Hitler alitaka kutawala dunia. Ukweli ni kwamba mnamo karne ya 20 hasa kuanzia miaka ya 1945 hadi kufikia 1845. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na Uchumi wa Makoloni....
Hitler angeyapiga mataifa yote ya Ulaya na yakakubali kukaa chini yake basi ni lazima angerithi na makoloni yote ya duniani.
Haya nikupe mfano mzuri tu,
Baada ya Vita ya Kwanza ya dunia kuisha Ujerumani alipewa adhabu kule Ufaransa kupitia mkutano wa Versailles Peace Treaty ambapo moja ya adhabu ilikuwa kunyanganywa makolono yake yote duniani.
Hivyo nilitegemea kwamba wewe ungefahamu kwamba Hitler angewapiga Waingereza, Wafarasansa, Wabelgiji, Wareno na Wamarekani huko Ulaya ni dhahiri kabisa angetawala dunia nzima kwasababu angerithi na makoloni yao.
Haya sasa,
Kipindi hicho cha vita ya kwanza na ya pili ya dunia. Muunganiko wa falme za Uingereza au The British Empire pekee alikuwa ana miliki Asilimia 20% ya Ardhi ya dunia, kuanzia Africa, Amerika na Asia. Hivyo kama Hitler angemshinda Muingereza pekee basi angejichukulia nchi kama Canada, India, Pakistan, Ghana, Tanganyika,Kenya, Uganda, Zimbabwe, Misri, Malawi, Zambia na Vijisiwa vingi hapa duniani.
Wewe unahisi huku siyo kutawala dunia ???
Haya angempiga Mfaransa pekee kabisaa,
Angejinyakulia Algeria, Vietnam,Burma, Central African Republic na mengineyo uyatafute.
Angempiga Ubelgiji pekee,
Angerithi koloni la Congo DRC.
Kifupi angepiga Ulaya yote ile basi angetawala Makoloni ya Afrika yote.
Sasa mtu mwenye yoyote makini ni lazima angeangalia madhara makubwa ya Hitler kutawala Ulaya pekee basi angetawala nusu ya dunia na Utajiri wake, kitu amacho kingemfanya atawale dunia nzima.
Nne,
Kuna kiti wanakiita The Mother Heart Theory,
Iliandikwa na mwanasayansi wa Siasa wa Uingereza ainyeitwa Sir Harlford McKinder, ambaye anasema Yeyote atakeyevunja nguvu ya Urusi basi atatawala karibia bara lote la Asia.
Huyu ndiye mwalimu wa Siasa wa Henry Kissinger. (The notorious cold Warrior)
Hujiulizi kwanini Hitler alitumia nguvu sana kuvamia Urusi na Uingereza ?? Wao ndiyo walikuwa na rasilimali nyingi sana duniani.
Urusi ingeanguka basi wakati ule basi Hitler angepata rasilimali nyingi sana za kuweza kuvamia Marekani na makoloni ya Afrika.
NB:Ndiyo maana asilimia 80% ya silaha zote za Wanazi zilitumika Urusi. Jiulize kwanini hakuzitumia Ulaya amalize kazo tu ??
Tano,
Usidanganyike na kilichoandikwa kwenye vitabu, jifunze kupima vitu kwa mapana zaidi. Hitler alikuwa ni mdanganyifu na mwenye mbinu mbaya sanaa na ovu.
NB:Kama angekuwa na nia ya kuifanya Ujerumani Super Power barani Ulaya, basi ni dhahiri kwamba angeheshimu Mkataba wa Molotov-Ribbentrop Pact wa mwaka 1949 ambao walikubaliana na Urusi kwamba hatavamia kwenda Mashariki kwa Poland. Kumbe ni mwongo na anaanda kitu kinaitwa The March to the East.
Mfano mwingine,
Kama Hitler alikuwa hana mpango wa kutawala dunia basi APPEASEMENT POLICY ya Waziri Mkuu wa Uingereza Neville Chamberlain ingefanikiwa kwa asilimia 100%. Wajerumani walivamia The Rhine Land, wakavamia Czechoslovakia, Uhispania na dunia ikasema tuwape kwasababu wataishia hapo. Hitler anataka kutawala hapo tu..
Nakuuliza sasa,
Je, Hitler aliishia hapo ambapo alikubaliana kwenye makaratasi na wenzake ???
Sita,
Ujerumani kama angevamia Japana wakati ule basi ni lazima angejipatia Uchina, Taiwan na Korea zote mbili ambazo zilikuwa ni sehemu muhimu kwa Ufalme wa Japan.
Hivyo basi,
Angetawala dunia yote kwa mkakati wa kusema "Shoot the head and the body will fall"
Saba,
Umesahau tena fact za muhimu.
Ujerumani ilikuwa Super Power tangu kipindi cha Prussia hadi kufikoa kwenye Franco-Prussian War of 1871. Kiufupi yeye ndiye alikuwa ni taifa lenye nguvu sana duniani hadi kufikia mwaka 1914. Miaka miwili ya vita ya kwanza ya dunia Ujerumani alishashinda vita na Muingereza alishajipanga kusalimu Amri.
Blunder la Arthur Zimmerman waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ndilo lilifanya Marekani aingie vitani. Wazayuni wakipigia debu sana vita iendelee.
Hivyo hoja yako hapa haina mashiko kabisa na nyepesi sanaaaaaaaa.............
Nane,
Nithibitishie kwamba Hitler angeshinda vita basi angeyaacha Makoloni yote ya Mahasimu wake na kitutangazia uhuru....
Nithibitishie kwamba Hitler angeshinda vita basia asingetamani kumvamia Marekani kwa kutumia Japan na Mexico kama alivyopanga kuitumia Mexico kwenye vita ya kwanza ya dunia. Akiwaahidi Mexico kwamba wakimvamia Marekani basi angewarudishia majimbo yao ya Texas, California na Nevada.
NB: Soma The Zimmerman Telegram
Mkuu nakushauri ufanye utafiti kabla ya kukurupula kujibu hizi hoja hapa.......
CC:
Consigliere,
zitto junior,
Red Giant