Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Tumeendelea kufuatilia ili kujua sababu hasa ya Bwana Malissa kukamatwa tena leo na kwamba eti ana kesi mpya huko Kilimanjaro.
Katika machache tuliyoyapata ni kuhusika kwa Adolf Mkenda, anayedaiwa kufungua kesi dhidi ya Malissa baada ya kuripoti huko nyuma kuhusu kuuawa kwa Mfanyakazi wa ndani wa Mkenda, huku wauaji wakiachwa hadi pale Malissa aliporipoti jambo hilo.
Mkenda anadai kwamba amechafuliwa na kwamba anamtaka Malissa athibitishe kwa kuweka Mkataba hadharani ili kuonyesha kwamba ni kweli Mtu huyo aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Mkenda.
Huu ndio msingi wa kukamatwa tena Godlisten, lalamikaji ni Mkenda.
Tutaendelea kufukua kila kilichopo nyuma ya jambo hili bila huruma yoyote, LIWALO NA LIWE .
Usiondoke JF.
===
Kuhusu Malisa kukamatwa na kusafirishwa, soma:
Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro
Madai ya Malisa yaliyomuhusisha Adolf Mkenda na kifo cha Beatrice Minja:
Arusha: Jeshi la Polisi lamtia mbaroni mtuhumiwa anayedaiwa kumuua Beatrice Minja