Adolf Mkenda atajwa kuwa chanzo cha Godlisten Malissa kukamatwa tena

Kimsingi Taarifa ile ya Mauaji ilikuwa sahihi, kwamba ni kweli yule mtu aliuawa, na wauaji wamekamatwa, hakuna aliyesema Muuaji ni Mkenda, isipokuwa Mkenda anasema marehemu hakuwa mfanyakazi wake, sasa wadau na majirani wanasema ni mfanyakazi wake, sasa cha kushangaza Mkenda anaogopa nini hadi afungue kesi kuwafunga wanaojua ni mfanyakazi wake, anataka kuficha nini?

Kwa kukutonya tu ni kwamba hii Kesi itamwanika zaidi Mkenda kuliko hata kifo cha mfanyakazi yule

Kinachotakiwa ni kuwapanga vyema hao mashahidi majirani wanaoweza kushuhudia mahakamani kuthibitisha kuwa huyo aliyeuwawa alikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa familia ya Prof. Mkenda..

Timu yake inapaswa kuwa smarter than ya mshitaki wake na ajue tu kuwa hilo analopambana nalo ni li - CCM..

Akumbuke tu pia, kuwa, ushahidi wa majirani ni very delicate maana wanaweza kuhongwa kirahisi mapesa mengi ili kuziba midomo yao. Haya maCCM sio ya mchezo eti, yana mahela ya wizi kila sehemu..
 
Kama ndio hoja hii, basi hiki unachouliza sio utetezi..

Kisheria housemaids/boys haki na maslahi yao yanalindwa na sheria za kazi za nchi kama alivyo mfanyakazi mwingine yeyote aliyeajiriwa iwe ktk sekta binafsi au serikalini..

Mwajiri yeyote asiye na mkataba na mfanyakazi wake wa ndani ni kosa kisheria.

Kama Godlisten Malissa ana uhakika kuwa Prf. Adolf Mkenda aliajiri mfanyakazi huyo na ana ushahidi wa kimkataba aidha iwe wa maneno (kuelewana kwa mazungumzo ya mdomo tu) au kwa maandishi, basi yuko salama..

Lakini kama amerusha tuhuma hizi pasipo kuwa na ushahidi wowote, basi iko shida na atapata shida sana kuthibitisha..

Hii haina maana kuwa tuhuma hizi dhidi ya Prof. Mkenda na familia yake si za kweli ama za kweli. Hilo anajua yeye.

Lakini ukiwa kama mwanasiasa smart, na kwa kuzingatia utata wa siasa za kiafrika na hasa za hapa Bongo na hususani kwa uhasama uliopo kati ya CCM na CHADEMA , mtu wa upande mmoja kurusha tuhuma fulani dhidi ya upande ule, mtu huyo anapaswa kuwa amejipanga kwelikweli kwa utetezi wa kisheria kwa sbb inaweza kuwa ndio mwanzo wa anguko la kisiasa la mtu huyo...

Jifunzeni kwa Makamu Mwenyekiti wenu Tundu Lissu. Huwa hakurupuki hovyo kurusha tuhuma fulani dhidi ya CCM au kiongozi yeyote wa serikali. Ukiona anasema jambo fulani lenye uelekeo wa kutuhumu, ujue kabisa ameshajipanga na anajua anafanya nini na matokeo yake yatakuwa nini...!

Mpaka hawa jamaa kuamua kumkamata Godlisten Malissa wanajua ni threat ktk engo fulani ya siasa zao...

Na tafsiri yake ya haraka haraka tu, ni kuwa wanamtafuta siku nyingi, na sasa wamepata weak point ya kisheria ili kumtesa nayo kuua nguvu yake ya ushawishi kisiasa. Na akikaa vibaya, watamfunga gerezani kabisa...!!
Wewe wa kwako umempa mkataba tuanzie hapa, au huna na hukuwahi ajiri, ivi wajua waweza kuwa na mtu na kukubaliana mpa posho na si mshahara? Ndo maana msukuma anawatukana wasomi uchwara
 
Na yeye akalalemo, walau awe na sura ngumu za kichadema chadema, mtu ana kasura laini kama keki ya ubatizo, sasa akikosa mkorogo huko ndani, ndio atatoka mweusi kama John Garang
 
Mkenda anadai kwamba amechafuliwa na kwamba anamtaka Malissa athibitishe kwa kuweka Mkataba hadharani ili kuonyesha kwamba ni kweli Mtu huyo aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Mkenda.
Watu na heshima zao mara nyingine hujidhalilisha wenyewe.
Huo mkataba ataupata wapi huyo Malisa. Hakuna njia nyingine za kupinga taarifa kama ni ya uongo?
 
Wewe wa kwako umempa mkataba tuanzie hapa, au huna na hukuwahi ajiri, ivi wajua waweza kuwa na mtu na kukubaliana mpa posho na si mshahara? Ndo maana msukuma anawatukana wasomi uchwara

Sina housemaid wala houseboy..

Kwa hapa, wewe hata hujaipata point yangu..

My point hapa wala hata sio ishu ya Adolf Mkenda na housemaid wake walikuwa na legal written contract kati yao or not..

Bali ilikuwa ni kumtahadharisha yeyote anayetatuhumu kuwa mtu mwingine kuhakikisha amejipanga technically kiutetezi/kiushahidi kabla ya kutuhumu..

Prof Adolf Mkenda anaweza kumshinda Godlisten Malissa kiurahisi tu kwa legal techniques kwa sababu anajua anayemtuhumu kuwa alikuwa na housemaid huyo (possibly alikuwa naye kweli) kisha akafa mikononi mwake kwa kifo cha utata, basi sharti a - produce ushahidi wa mkataba wa maandishi au uthibitisho wowote ule..
 
Tumeendelea kufuatilia ili kujua sababu hasa ya Bwana Malissa kukamatwa tena leo na kwamba eti ana kesi mpya huko Kilimanjaro.

Katika machache tuliyoyapata ni kuhusika kwa Adolf Mkenda, anayedaiwa kufungua kesi dhidi ya Malissa baada ya kuripoti huko nyuma kuhusu kuuawa kwa Mfanyakazi wa ndani wa Mkenda, huku wauaji wakiachwa hadi pale Malissa aliporipoti jambo hilo.

Mkenda anadai kwamba amechafuliwa na kwamba anamtaka Malissa athibitishe kwa kuweka Mkataba hadharani ili kuonyesha kwamba ni kweli Mtu huyo aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Mkenda.

Huu ndio msingi wa kukamatwa tena Godlisten, lalamikaji ni Mkenda.

Tutaendelea kufukua kila kilichopo nyuma ya jambo hili bila huruma yoyote, LIWALO NA LIWE .

Usiondoke JF.

===

Kuhusu Malisa kukamatwa na kusafirishwa, soma:

Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro

Madai ya Malisa yaliyomuhusisha Adolf Mkenda na kifo cha Beatrice Minja:

Arusha: Jeshi la Polisi lamtia mbaroni mtuhumiwa anayedaiwa kumuua Beatrice Minja
Atiwe adabu za kutosha huyo Godlisten pamoja na yule mwenzie
 
Unajuaje kama iliishi naye kama ndugu tu ,au kwa makubaliano ya posho tu, na je wewe waweza ishi na mtu majirani wako wasijue ,likitokea la kutokea basi watu wakae kimia kisa hamko katika maandishi ya mkataba? Hoja hapa inaweza kuwa mtu aliekua anaonekana kwako yuko wapi ? Kama amerudi kwao ijulikane, kama ameenda tafuta maisha pengine ijulikane period , yani itokee unakaa na mtu majirani wanajua alafu atoweke kwa mfano tu ,watu washindwe kuhoji kisa jificha kwenye maandishi ya makaratasi hakuna iyo

Twende mbele tutajua , uyu mtuhumiwa sio mjinga ila pia sipo hapa tetea mtu anaezushia mtu mwingine , haki itendeke basi ijulikane mbivu na mbichi
 
Tumeendelea kufuatilia ili kujua sababu hasa ya Bwana Malissa kukamatwa tena leo na kwamba eti ana kesi mpya huko Kilimanjaro.

Katika machache tuliyoyapata ni kuhusika kwa Adolf Mkenda, anayedaiwa kufungua kesi dhidi ya Malissa baada ya kuripoti huko nyuma kuhusu kuuawa kwa Mfanyakazi wa ndani wa Mkenda, huku wauaji wakiachwa hadi pale Malissa aliporipoti jambo hilo.

Mkenda anadai kwamba amechafuliwa na kwamba anamtaka Malissa athibitishe kwa kuweka Mkataba hadharani ili kuonyesha kwamba ni kweli Mtu huyo aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Mkenda.

Huu ndio msingi wa kukamatwa tena Godlisten, lalamikaji ni Mkenda.

Tutaendelea kufukua kila kilichopo nyuma ya jambo hili bila huruma yoyote, LIWALO NA LIWE .

Usiondoke JF.

===

Kuhusu Malisa kukamatwa na kusafirishwa, soma:

Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro

Madai ya Malisa yaliyomuhusisha Adolf Mkenda na kifo cha Beatrice Minja:

Arusha: Jeshi la Polisi lamtia mbaroni mtuhumiwa anayedaiwa kumuua Beatrice Minja
Ukweli ni kwamba hata kama ni kweli hawezi kupata huo mkataba na waziri anajua kabisa. Tangu lini wa housegal wa Tanzania wakawa na mikataba ya maandishi tuwe wa kweli jamani. Labda wale wa kuchukua kwa Joyce Kiria.
 
Kama ni kweli kafanya hayo akajibu, kuropoka kwake, ni sawa.
Huo muda ulioisha tangu hizi tuhuma zitolewe inaonyesha kuna ukweli. Mkenda alisubiri ili ''kufukia'' ukweli kwanza, ndiyo akaja na hili. Ila mkataba tu siyo unaothibitisha kuwa huyu ni mfanyakazi wa ndani wa fulani. Kuna wengi sana wanafanya bila mkataba au niseme kwa kutumia mkataba wa mdomo.
 
Hakuna mtu anaweza fukia ukweli. Acha porojo.
 
Akili ndezi hizi nazo....

Kwamba wewe ukitoa maoni kwamba: Mbowe aliiba hela za chadema akajenga nyumba ukatangaza publicly na una ushahidi, Mbowe anaweza kufukia ushahidi? Wewe basis ya kusema hayo kama ni nini? Si unapaswa uwe nazo?
 
Badala ua kuongea mambo ya msingi na wizi unaoendelea nchini mnakimbilia mbowe😕
 
Tumeendelea kufuatilia ili kujua sababu hasa ya Bwana Malissa kukamatwa tena leo na kwamba eti ana kesi mpya huko Kilimanjaro.

Katika machache tuliyoyapata ni kuhusika kwa Adolf Mkenda, anayedaiwa kufungua kesi dhidi ya Malissa baada ya kuripoti huko nyuma kuhusu kuuawa kwa Mfanyakazi wa ndani wa Mkenda, huku wauaji wakiachwa hadi pale Malissa aliporipoti jambo hilo.

Mkenda anadai kwamba amechafuliwa na kwamba anamtaka Malissa athibitishe kwa kuweka Mkataba hadharani ili kuonyesha kwamba ni kweli Mtu huyo aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Mkenda.

Huu ndio msingi wa kukamatwa tena Godlisten, lalamikaji ni Mkenda.

Tutaendelea kufukua kila kilichopo nyuma ya jambo hili bila huruma yoyote, LIWALO NA LIWE .

Usiondoke JF.

===

Kuhusu Malisa kukamatwa na kusafirishwa, soma:

Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro

Madai ya Malisa yaliyomuhusisha Adolf Mkenda na kifo cha Beatrice Minja:

Arusha: Jeshi la Polisi lamtia mbaroni mtuhumiwa anayedaiwa kumuua Beatrice Minja
Haya ni madai binafsi iweje akamatwe na polisi?
 
Back
Top Bottom