Adolf Mkenda atajwa kuwa chanzo cha Godlisten Malissa kukamatwa tena


Kinachotakiwa ni kuwapanga vyema hao mashahidi majirani wanaoweza kushuhudia mahakamani kuthibitisha kuwa huyo aliyeuwawa alikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa familia ya Prof. Mkenda..

Timu yake inapaswa kuwa smarter than ya mshitaki wake na ajue tu kuwa hilo analopambana nalo ni li - CCM..

Akumbuke tu pia, kuwa, ushahidi wa majirani ni very delicate maana wanaweza kuhongwa kirahisi mapesa mengi ili kuziba midomo yao. Haya maCCM sio ya mchezo eti, yana mahela ya wizi kila sehemu..
 
Wewe wa kwako umempa mkataba tuanzie hapa, au huna na hukuwahi ajiri, ivi wajua waweza kuwa na mtu na kukubaliana mpa posho na si mshahara? Ndo maana msukuma anawatukana wasomi uchwara
 
Na yeye akalalemo, walau awe na sura ngumu za kichadema chadema, mtu ana kasura laini kama keki ya ubatizo, sasa akikosa mkorogo huko ndani, ndio atatoka mweusi kama John Garang
 
Mkenda anadai kwamba amechafuliwa na kwamba anamtaka Malissa athibitishe kwa kuweka Mkataba hadharani ili kuonyesha kwamba ni kweli Mtu huyo aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Mkenda.
Watu na heshima zao mara nyingine hujidhalilisha wenyewe.
Huo mkataba ataupata wapi huyo Malisa. Hakuna njia nyingine za kupinga taarifa kama ni ya uongo?
 
Wewe wa kwako umempa mkataba tuanzie hapa, au huna na hukuwahi ajiri, ivi wajua waweza kuwa na mtu na kukubaliana mpa posho na si mshahara? Ndo maana msukuma anawatukana wasomi uchwara

Sina housemaid wala houseboy..

Kwa hapa, wewe hata hujaipata point yangu..

My point hapa wala hata sio ishu ya Adolf Mkenda na housemaid wake walikuwa na legal written contract kati yao or not..

Bali ilikuwa ni kumtahadharisha yeyote anayetatuhumu kuwa mtu mwingine kuhakikisha amejipanga technically kiutetezi/kiushahidi kabla ya kutuhumu..

Prof Adolf Mkenda anaweza kumshinda Godlisten Malissa kiurahisi tu kwa legal techniques kwa sababu anajua anayemtuhumu kuwa alikuwa na housemaid huyo (possibly alikuwa naye kweli) kisha akafa mikononi mwake kwa kifo cha utata, basi sharti a - produce ushahidi wa mkataba wa maandishi au uthibitisho wowote ule..
 
Atiwe adabu za kutosha huyo Godlisten pamoja na yule mwenzie
 
Unajuaje kama iliishi naye kama ndugu tu ,au kwa makubaliano ya posho tu, na je wewe waweza ishi na mtu majirani wako wasijue ,likitokea la kutokea basi watu wakae kimia kisa hamko katika maandishi ya mkataba? Hoja hapa inaweza kuwa mtu aliekua anaonekana kwako yuko wapi ? Kama amerudi kwao ijulikane, kama ameenda tafuta maisha pengine ijulikane period , yani itokee unakaa na mtu majirani wanajua alafu atoweke kwa mfano tu ,watu washindwe kuhoji kisa jificha kwenye maandishi ya makaratasi hakuna iyo

Twende mbele tutajua , uyu mtuhumiwa sio mjinga ila pia sipo hapa tetea mtu anaezushia mtu mwingine , haki itendeke basi ijulikane mbivu na mbichi
 
Ukweli ni kwamba hata kama ni kweli hawezi kupata huo mkataba na waziri anajua kabisa. Tangu lini wa housegal wa Tanzania wakawa na mikataba ya maandishi tuwe wa kweli jamani. Labda wale wa kuchukua kwa Joyce Kiria.
 
Kama ni kweli kafanya hayo akajibu, kuropoka kwake, ni sawa.
Huo muda ulioisha tangu hizi tuhuma zitolewe inaonyesha kuna ukweli. Mkenda alisubiri ili ''kufukia'' ukweli kwanza, ndiyo akaja na hili. Ila mkataba tu siyo unaothibitisha kuwa huyu ni mfanyakazi wa ndani wa fulani. Kuna wengi sana wanafanya bila mkataba au niseme kwa kutumia mkataba wa mdomo.
 


Hakuna mtu anaweza fukia ukweli. Acha porojo.
 
Akili ndezi hizi nazo....

Kwamba wewe ukitoa maoni kwamba: Mbowe aliiba hela za chadema akajenga nyumba ukatangaza publicly na una ushahidi, Mbowe anaweza kufukia ushahidi? Wewe basis ya kusema hayo kama ni nini? Si unapaswa uwe nazo?
 
Badala ua kuongea mambo ya msingi na wizi unaoendelea nchini mnakimbilia mbowe😕
 
Haya ni madai binafsi iweje akamatwe na polisi?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…