The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Haji Manara anaweza kudhani ana maadui wengi wanaomfanyia fitina, lakini ukweli ni kwamba adui wake mkuu kwa sasa ni wakati. Wakati unapobadilika dhidi yako, unaweza kushangazwa na mambo yanayotokea na kudhani watu wanakufanyia fitina.
Kwa upande wa Ally Kamwe, wakati unamfaa sana. Kila anachofanya kinakuwa rahisi na kukubalika kwake si jambo gumu. Ukweli ni kuwa, kwa kazi yoyote inayohitaji mitandao, kijana wa kizazi cha Z kama Ally anaweza kufanya kazi kwa urahisi zaidi kuliko watu wenye umri kama wa Manara, bila kujali uzoefu. Teknolojia inawapa nafasi vijana wanaoibukia pamoja na maendeleo ya teknolojia yenyewe.
Kama kazi ya usemaji ingekuwa bado inategemea zaidi redio na magazeti kama zamani, Manara angebaki kuwa bora. Lakini ukichanganya na matumizi ya mitandao ya kijamii, vijana kama Ally Kamwe ndio wanaoweza kustawi na kutamba zaidi. Inawezekana viongozi kama Hersi wanapata changamoto ya kujua nafasi sahihi ya kumweka Manara kwa sababu wakati umekuwa kikwazo kikubwa kwake. Zama zimeshabadili
ka.