Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Umoja ni nguvu ili kuing'oa CCM,
Tatizo letu kubwa au labda niseme tatizo kubwa la vyama vya Upinzani katika juhudi za kuitoa Tanzania kwenye madhila inayoyakabili ni kwamba THEY ARE SO PREDICTABLE. Mara zote Vyama vya upinzani na nina maana ya mara zote tangu uchaguzi wa vyama vingi au mfumo to date ni kwamba wanafanya yale ambayo CCM na serikali zake wanawategemea wafanye. Wanazungumza maneno yale yale, wanafanya vitendo vile vile na wanakwenda kwa watu wale wale kutaka msaada na ushauri na zaidi wanawategemea watu au jumuia zile zile.
Kwa hivyo imefika pahala leo CCM na serikali zake hata hawashughulishwi au kutishwa na Vyama vya upinzani tena. Upinzani umepoteza ile surprising factor yake. Umepoteza ule mvuto wake. Kwa maoni yangu inabidi Vyama vya upinzani vianze kufikiri nje ya box. Vinapaswa vijivumbue upya. In other words, must come with new strategies and they must approach CCM in a different way. They must use new tactics and strategies. They must look at CCM and its two government in a different way. Kwa kuanzia wasikubali tena upuuzi eti wapinzani wao ni CCM. CCM ni kundi la watu wachache wanaotafuta kila njia ya kujitajirisha wenyewe bila kujali maslahi ya wanachama wao na raia wote kwa ujumla. Hili ni jambo moja ambalo Upinzani wanaweza kulitumia na mifano iko mingi ya kuonyesha kwamba CCM hawana nia ya kuwaondoshea Watanzania kwa ujumla matatizo yanayo wakabili- hili suala la ufisadi ni mfano mmoja lakini kuna na mifano mingi mengine.
Pili ni lazima waiambie dunia na Watanzania kwa ujumla kwamba mpizani wao ni SMT na SMZ na sio CCM. Kwani CCM ni kichaka tu wanachojifichia. Ukweli ni kwamba CCM wanatumia vyombo vya serikali kufanikisha malengo yao. Hili ni jambo ambalo linaweza kupelekwa hata mahakamani ili ionyeshwe ni vipi SMT/SMZ zimekuwa ni matawi ya CCM. Mfano ni kwamba polisi, JWTZ, usalama, ofisi ya rais wote wa ZNZ na TZ zinatumika kuendeleza maslahi ya CCM.
Tatu tume zote za uchaguzi sio huru. Zimeundwa kwa kutumia wanachama au wapenzi wa CCM. Kwa nini Wapinzani wasidai kwamba tume hizo ama ziundwe kwa kuwa na wajumbe sawa kutoka kila chama au wajumbe wake wasiwe wanachama au wapenzi wa chama chochote. Na zaidi kwa nini wasidai kwamba wajumbe wa tume ya uchaguzi wasiwe wanajibu kwa rais yoyote yule. Iwe mathalan wanawajibika kwa baraza la wawakilishi na bunge? Bora zaidi kwa nini wasidai muundo wa tume ya uchaguzi uwe kama vile ilivyo fanywa Afaghanistan i.e. tume yenyewe wajumbe wake ni WaTZ lakini juu yake kuna Tume ya rufaa ya uchaguzi ambayo inaundwa na wajumbe kutoka nje ya TZ, mfano EU, UN, Commonwealth n.k.
Upinzani unatakiwa uhakikishe kwamba kila inalolifanya/kusema inaweza kulitekeleza. Wasiwe kama CCM kutoa ahadi ambazo hawawezi kuzitekeleza. Ni lazima matendo yao na kauli zao zionyeshe tafauti ya wazi baina yao na CCM. Kwani hivi sasa hakuna tafauti yoyote. Pia wakubali kukoselewa na wapokee maoni ya wengine. Ni muhimu sana kwa manufaa ya Tanzania na WaTanzania wote kwamba wawakilishi/wabunge ambao lengo lao ni kujinufaisha wao binafsi waachwe na iwe ni kawaida kwa wabunge/wawakilishi wa upinzani kukutana na raia wa majimbo yao ya uchaguzi bila kujali wanatoka chama gani. Wawe na siku maalum na ofisi maalum katika majimbo yao ambapo wanakutana na raia kusikiliza matazo yao na shida zao. Isiwe biashara ya kuonana kila unapofika uchaguzi au wanapopita na magari yao makubwa huku wakiwarushia mavumbi wale walio wachagua.
Ama kuhusu suala la muungano na Zanzibar, ninadhani kwamba wajumbe wa ukumbi huu na hata wasio wajumbe, as long as we share same beliefs and principles, tunaweza kulipeleka suala hili kwenye vyombo vya kimataifa kutaka ufumbuzi na zaidi kuudadisi uhalali wa Muungano. Kwani the so called Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio muungano wa ridhaa, at least hivi sasa ridhaa haipo tena, yaliyobakia ni mabavu tu. Huu sasa ni ukoloni na sisi kama WaTanzania hatuna budi kuupinga.Kwa kutumia vyama vyetu vya upinzani ,sio tunaburuzwa na itikadi za kiCCM.
Naomba kuwasilisha hoja ukumbi wa JF.