Adui wa legacy ya Rais Magufuli: Kuminya Demokrasi au kushindwa kudhibiti maambukizi ya Corona?

Adui wa legacy ya Rais Magufuli: Kuminya Demokrasi au kushindwa kudhibiti maambukizi ya Corona?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Watu wengi kwenye kambi ya upinzani wamekuwa wanadai kuwa Magufuli kabinya demokrasi ilihali huwa wanashiriki uchaguzi na ama wanashinda au wanashindwa kama ilivyo ada ya demokrasia. demokrasia haiana maana kuwa upinzani ndio ushinde tu.

Viongozi huwa hawapimwi kwa mambo ya kawaida bali yale ya kupita (transitional). Jambo transitional ambalo litamhukumu sana Maguful ni jinsi alivyosimamia maambukizi ya Korona. Amelisimamia vibaya sana kiasi kuwa hata wafuasi wake wanaweza kuwa wanakufa bila kujua kuwa wana virusi vya korona. Alizima information yoyote inayohusu korona, na kusahahu kuwa information is power.

Wakati wa ujana wetu (pamoja na yeye) tulipewa information zote kuhusu AIDS na ilitusaidia sana kujua jinsi ya kuikwepa. Sasa hivi information ya Corona haipo kabisa, na watu hawajui namna ya kuikwepa.

Watu wanajoifanya kuwa wanajua kusimamia interests za Watanzania wote wanapiga kelele kwa mambo yanayowahusu interests zao tu, kama kuruhusiwa kufanya maandamano, ambacho siyo kipimo kabisa che demokrasia, lakini sijasikia hata mmoja akizungumzia uongozi wa hili la korona linalohusu umma wa Watanzania wote. Hata wanaoliongelea, wanatumia njia hiyo hiyo ya kuhimiza maslahi yao binafsi.
 
Ni kwasababu hatujuani ila inaonyesha huna akili.

Hakuna chombo Cha habari kitaripoti ishu ya korona itakayosemwa na opposition.

Kiufupi tuko 2021 ila tumelazimishwa kuishi miaka ya 1943.

Adui wa JPM ni yeye mwenyewe. Hashauriki na hapangiwi watu pekee anaowagwaya ni jwtz kwasababu anawaelewa.
 
Mleta mada COVID si issue Tanzania, ilishaombewa na Mungu anesikiliza sala zetu kuliko hata sala za Baba Mtakatifu kule Rome aliyasikia maombi yetu. Italy pamoja na idadi ya watawa waliokua nao lakini COVID iliwachapa haswa.

Demokrasia Tanzania ni kubwa sana. Viongozi wa juu karibu wote walipita bila kupingwa katika majimbo yao ilhali wapinzani wao wakibambikiwa kesi za jinai.
 
Mleta mada COVID si issue Tanzania, ilishaombew na Mungu anesikiliza sala zetu kuliko hata sala za Baba Mtakatifu kule Rome aliyasikia maombi yetu. Italy pamoja na idadi ya watawa waliokua nao lakini COVID iliwachapa haswa.

Demokrasia Tanzania ni kubwa sana. Viongozi wa juu karibu wote walipita bila kupingwa katika majimbo yao ilhali wapinzani wao wakibambikiwa kesi za jinai.
Umesahau pia eti betina pale mbeya alimshinda sugu na mbowe kule hai eti nae alishindwa msigwa iringa halafu viongozi wa dini wakapongeza ushindi.
 
Hiki kichuguu kitakuwa cha sisimizi.

Magufuli adui wa legacy yake wapo kibao

1. Mauaji ya raia kibao.
2. Wanasiasa kupigwa risasi na kitekwa.
3. Kubambikia kesi wafanyabiashara na kuwapora mali zao.
4. Kupendelea kijijini kwao anakotokea.
5. Kufanya ufisadi wa kutisha kwa kutofuata taratibu za manunuzi.
6. Kuipa tenda kampuni yake kwenye kila mradi wa ujenzi.
7.Kuuwa mamia ya watanzania kwa Corona.

Sijui ungependa niendelee.

Huyo mungu wako siyo kiongozi ni muuaji, dikteta, mshirikina
 
Miaka sita sasa kwa wafanyakazi, na wengine wana miaka saba! Hapandishi madaraja. Ila kwenye majeshi, TRA, Wabunge, na yeye mwenyewe, maisha yanaendelea kama kawaida.

Lissu aliporudi kutoka Ubelgiji mwaka wa jana, aliliongelea hili mara nyingi tu. Lakini waliishia kumkejeli. Halafu mtoa mada anataka hao wanasiasa wa upinzani waongee nini!

Anayafahamu kweli maumivu wanayopitia baada ya kudhulumiwa matokeo yao? Halafu aliyemuambia maswala yahusuyo Utaifa basi yanatakiwa yazungumzwe na wapinzani ni nani?

Kwa nini ndani ya chama chao hamna ujasiri wa kumuambia Mwenyekiti wao kuhusu kuto kupenda kushaurika? Mkuu uko sahihi. Mtoa mada atakua ni Kichuguu cha sisimizi! Halafu eti ni Platinum member!
 
Kichuguu
Legacy ya Jiwe ni mbovu kupindukia.

1. Kutoheshimu katiba ya nchi na sheria isipokuwa pale zinapomfavor yeye

2. Kupora na kuiba uchaguzi waziwazi, kuanzia chaguzi za marudio, za serikali za mitaa na za uchaguzi mkuu

3. Kutekwa na kupotezwa watu.

4. Miradi hewa isiyo na faida kwa nchi na inayopitishwa bila kufuata taratibu za kisheria mfano miradi ya Ndege.

5. Rushwa ya waziwazi, mfano kununua wapinzani waunge mkono Juhudi.

6. Udini uliokubuhu, teuzi zake zinanuka udini kupindukia.

7. Kauli mbaya na za udhalilishaji kwa wanawake.

8. Kuharibu maisha ya watu mfano kupora korosho za wananchi Mtwara.

9. Kuliingilia bunge na kuiabuse mahakama kwa kupeleka kesi za "uhujumu uchumi" kwa watu asiowapenda.

10. Kuua free press.

11. Lingine ni hili uliolitaja la Korona. Ukataa kwake uwepo wa Korona na kutangaza waziwazi ni kuhatarisha usalama wa umma

Kufupi huyo mtu hakupaswa kuwa kiongozi, anavunja kanuni zote za utawala boda na respnsible leadership
 
Kwani watawa kuwa Italy ndio kusema hawafanyi dhambi? Mbona wanaongoza kufanya sodomy. Acha kuwa na akili mgando,kuona kuwa Mungu haipendi Tanzania kisa tu hakuna watawa.

Viongozi walichaguliwa kwa kura, kama hamtaki nendeni Italia na ubelgiji mkaolewe na wazungu wafumue system zote huko nyuma.

kuna sababu gani ya kutumia lugha ya matusi ....na kushambulia watu moja kwa moja...jaribu kuwa na staha na ujibu hoja siyo kutukana watu
 
Mkongwe mwenzangu naomba upumzike tu!, Yaani kati ya Wakongwe ambao nikitaka kupata walau mambo ya maana ninawatafuta ni Kichuguu.

Lakini naona unazeeka vibaya sana.
Ninavyofahamu mimi;
Mpofuka ukongweni hapotewi na njia.
na Ya kale ni dhahabu .
au Mbuzi mzee hapigi chafya bure.
 
Bahati mbaya Covid19 ni kama Cholera. Huwezi kuificha pale inapokutandika na lazima watu wako wa karibu wajue

Alichofanya Magufuli kuhusu COVID19 somehow hajakosea sana maana options zilikuwa chache.
 
Mambo mengi mnayotaja yananweza kuwa ni mambo makubwa kweli lakini siyo mambo transitional yaliyojitokeza ghafla bila control ya serikali yake; hayaingii kwenye record ya legacy ya kiongozi yeyote. Legacy ya George Bush marekani siyo wizi wa kura uliompa madaraka, uingiliaji wa uhuru wa watu alioleta kutokana na patriot act, au tengano aliojenga baina ya democrats na republicans; la! Legacy yake inapimwa na mambo mawili tu, alivyosimamia nchi wakati wa janga la katrina, na alivyoongoza nchi baada ya 9/11 ikiwa ni pamoja na kupeleka nchi vitani.
 
Watu wengi kwenye kambi ya upinzani wamekuwa wanadai kuwa Magufuli kabinya demokrasi ilihali huwa wanashiriki uchaguzi na ama wanashinda au wanashindwa kama ilivyo ada ya demokrasia. demokrasia haiana maana kuwa upinzani ndio ushinde tu.

Viongozi huwa hawapimwi kwa mambo ya kawaida bali yale ya kupita (transitional). Jambo transitional ambalo litamhukumu sana Maguful ni jinsi alivyosimamia maambukizi ya Korona. Amelisimamia vibaya sana kiasi kuwa hata wafuasi wake wanaweza kuwa wanakufa bila kujua kuwa wana virusi vya korona. Alizima information yoyote inayohusu korona, na kusahahu kuwa information is power.

Wakati wa ujana wetu (pamoja na yeye) tulipewa information zote kuhusu AIDS na ilitusaidia sana kujua jinsi ya kuikwepa. Sasa hivi information ya Corona haipo kabisa, na watu hawajui namna ya kuikwepa.

Watu wanajoifanya kuwa wanajua kusimamia interests za Watanzania wote wanapiga kelele kwa mambo yanayowahusu interests zao tu, kama kuruhusiwa kufanya maandamano, ambacho siyo kipimo kabisa che demokrasia, lakini sijasikia hata mmoja akizungumzia uongozi wa hili la korona linalohusu umma wa Watanzania wote. Hata wanaoliongelea, wanatumia njia hiyo hiyo ya kuhimiza maslahi yao binafsi.
Nyoosha maelezo yako na uache kurukaruka,tangy lini rangi nyeusi ikalazimishwa kuonekana nyeupe.
 
Bahati mbaya Covid19 ni kama Cholera. Huwezi kuificha pale inapokutandika na lazima watu wako wa karibu wajue

Alichofanya Magufuli kuhusu COVID19 sonehow hajakosea sana maana options zilikuwa chache.
Sahihi kabisa. Kaugonjwa kapo, mahospitalini kuna influx sana this time
 
Back
Top Bottom