Adui wa legacy ya Rais Magufuli: Kuminya Demokrasi au kushindwa kudhibiti maambukizi ya Corona?

Tulifanya maombi ya siku tatu Mungufull akaiondoa Corona
 
Hiyo siyo mada.

Ni kawaida sana kwa watu wajinga na wapumbavu kudhani kuwa wengine ndio wapumbavu zaid yao!. Maneno yako ni reflection hiyo. Uliambiwa kuwa unapomnyooesha mwenzako kidole chapete, vile vingine vyote vinakuwa vinakuoonyesha wewe mwenyewe. Ukishakuwa na busara hiyo utabadili lugha zako kuhusu watu wengine.
Sasa mtu anaedanganya umma wa JF kuwa wapinzani wanadai kuwa Tanzania hakuna demokrasia kwa sababu hawakushinda uchaguzi ilihali wapinzani waliweka wazi kabisa madai yao kwamba uchaguzi haukuwa wa kidemokrasia kwa sababu mawakala hawakuruhusiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura,mawakala walitekwa na kadhalika;mtu wa namna hiyo siyo mpumbavu?Unataka mtu wa namna hiyo nimwite kuwa ni mtu mwerevu na makini?
 
Kuna sheria za kufuata iwapo mtu hakubaliani na matokeo ya uchaguzi, na zimeshatumika sana nchini hapa; ziliwavua ubunge akina Kihiyo, Wassira, Mramba, na wengineo wengi. Hakuna mgombea yeyote ambaye mpaka wakati huu ameshafungua kesi kupinga matokeo yale kama unavyodai, kwani uwepo wa mawakala kwenye vituo ni jambo la kisheria, na mtu yeyote anayezuia mawakala anakuwa amevunja sheria. In fact kwenye jimbo la Hai Mbowe alikuwa na wmawakali katika vituo vyote na bado alishindwa kwa wingi wa kura.

Unaishi Tanzania hii hii ambayo pia wengine tunaishi au una Tanzania yako unayoishi?!Unawezaje kufungua kesi katika mazingira kama haya?!Upo serious kabisa na unachoandika au unafanya tu mzaha?
5678901.jpg
87659087.jpg
 
Unaishi Tanzania hii hii ambayo wengine tunaishi au una Tanzania yako unayoishi?!Unawezaje kufungua kesi katika mazingira kama haya?!Upo serious kabisa na unachoandika au unafanya tu mzaha?
View attachment 1683181View attachment 1683189

Vikaragosi ni mawazo ya mchoraji, siyo sheria na wala usiendeshea maisha yako au kutoa mawazo yako kwa kusoma vikaragosi.

Kuogopa kuomba haki yako mahakamani siyo utetezi; fungua kesi halafu ulalamikie uamuzi lakini siyo kulalamika chinichini bila kwenda mahakamani ambako utaonyesha ushahidi wako. Marehemu Mtikila aliishitaki sana serikali mahakamani na kuna mahala alishinda na kule ambako hakuridhika na uamuzi alikata rufaa; ndiyo utaratibu wa sheria
 
Toka mwanzo watu hawakuwa wakichukulia serious kujikinga na corona. Watu walikuwa wanafanya shughuli zao kama kawaida,daladala ilikuwa level seat ila wao walikuwa wanapanda na kukaa chini wanajificha wasionekane na traffic sio kuogopa corona,kwenye kuzikana wanajazana kama kawaida walikuwa wanaogopa polisi tu sio corona,nyumba za ibada watu walikuwa wanaenda kama kawaida. Sasa katika mazingira kama hayo mnaona tatizo ni Magufuli kusema hakuna corona wakati hao watu wenyewe toka mwanzo walikuwa wanaishi kama hakuna corona,unakuta mtu alikuwa anasifia nyomi za kampeni halafu baada ya uchaguzi kuisha nae analaumu serikali kusema hakuna corona sasa.
 
Watu wengi kwenye kambi ya upinzani wamekuwa wanadai kuwa Magufuli kabinya demokrasi ilihali huwa wanashiriki uchaguzi na ama wanashinda au wanashindwa kama ilivyo ada ya demokrasia. demokrasia haiana maana kuwa upinzani ndio ushinde tu.

Viongozi huwa hawapimwi kwa mambo ya kawaida bali yale ya kupita (transitional). Jambo transitional ambalo litamhukumu sana Maguful ni jinsi alivyosimamia maambukizi ya Korona. Amelisimamia vibaya sana kiasi kuwa hata wafuasi wake wanaweza kuwa wanakufa bila kujua kuwa wana virusi vya korona. Alizima information yoyote inayohusu korona, na kusahahu kuwa information is power.

Wakati wa ujana wetu (pamoja na yeye) tulipewa information zote kuhusu AIDS na ilitusaidia sana kujua jinsi ya kuikwepa. Sasa hivi information ya Corona haipo kabisa, na watu hawajui namna ya kuikwepa.

Watu wanajoifanya kuwa wanajua kusimamia interests za Watanzania wote wanapiga kelele kwa mambo yanayowahusu interests zao tu, kama kuruhusiwa kufanya maandamano, ambacho siyo kipimo kabisa che demokrasia, lakini sijasikia hata mmoja akizungumzia uongozi wa hili la korona linalohusu umma wa Watanzania wote. Hata wanaoliongelea, wanatumia njia hiyo hiyo ya kuhimiza maslahi yao binafsi.
Utakuwa umekunywa maji ya chooni tu si bure.
 
Vikaragosi ni mawazo ya mchoraji, siyo sheria na wala usiendeshea maisha yako au kutoa mawazo yako kwa kusoma vikaragosi.

Kuogopa kuomba haki yako mahakamani siyo utetezi; fungua kesi halafu ulalamikie uamuzi lakini siyo kulalamika chinichini bila kwenda mahakamani ambako utaonyesha ushahidi wako. Marehemu Mtikila aliishitaki sana serikali mahakamani na kuna mahala alishinda na kule ambako hakuridhika na uamuzi alikata rufaa; ndiyo utaratibu wa sheria
Mahakama za Tanzania zilishajithibitisha zenyewe kuwa hazipo tayari kutenda haki na zimewekwa mfukoni na serekali pamoja na chama cha mapinduzi.

Hili linajidhihirisha wazi kwa mahakama hizi kushikilia wakosoaji wa serekali bila dhamana kwa kuyapokea makosa ya uongo ya kesi za uhujumu uchumi ambazo wanabambikiwa wahanga.Mahakama hizi pia zilishajidhihirisha mbele ya Watanzania kuwa hazipo tayari kutenda haki kwa wapinzani wa Magufuli kwani tumeona wapinzani nchi nzima wakiwekwa ndani kiholela na kufunguliwa mashtaka ya uongo ya uhujumu uchumi.Sasa kwa nini chama cha siasa kipoteze muda pamoja na rasilimali-pesa kwenda kufungua kesi katika mahakama ambazo zimejidhihirisha waziwazi kuwa zipo upande wa chama cha mapinduzi pamoja na serekali iliyopo madarakani?
 
Watu wengi kwenye kambi ya upinzani wamekuwa wanadai kuwa Magufuli kabinya demokrasi ilihali huwa wanashiriki uchaguzi na ama wanashinda au wanashindwa kama ilivyo ada ya demokrasia. demokrasia haiana maana kuwa upinzani ndio ushinde tu.

Viongozi huwa hawapimwi kwa mambo ya kawaida bali yale ya kupita (transitional). Jambo transitional ambalo litamhukumu sana Maguful ni jinsi alivyosimamia maambukizi ya Korona. Amelisimamia vibaya sana kiasi kuwa hata wafuasi wake wanaweza kuwa wanakufa bila kujua kuwa wana virusi vya korona. Alizima information yoyote inayohusu korona, na kusahahu kuwa information is power.

Wakati wa ujana wetu (pamoja na yeye) tulipewa information zote kuhusu AIDS na ilitusaidia sana kujua jinsi ya kuikwepa. Sasa hivi information ya Corona haipo kabisa, na watu hawajui namna ya kuikwepa.

Watu wanajoifanya kuwa wanajua kusimamia interests za Watanzania wote wanapiga kelele kwa mambo yanayowahusu interests zao tu, kama kuruhusiwa kufanya maandamano, ambacho siyo kipimo kabisa che demokrasia, lakini sijasikia hata mmoja akizungumzia uongozi wa hili la korona linalohusu umma wa Watanzania wote. Hata wanaoliongelea, wanatumia njia hiyo hiyo ya kuhimiza maslahi yao binafsi.
Na Umbumbumbu wa masuala ya Kitaifa/Kimataifa pia
 
Kuna sheria za kufuata iwapo mtu hakubaliani na matokeo ya uchaguzi, na zimeshatumika sana nchini hapa; ziliwavua ubunge akina Kihiyo, Wassira, Mramba, na wengineo wengi. Hakuna mgombea yeyote ambaye mpaka wakati huu ameshafungua kesi kupinga matokeo yale kama unavyodai, kwani uwepo wa mawakala kwenye vituo ni jambo la kisheria, na mtu yeyote anayezuia mawakala anakuwa amevunja sheria. In fact kwenye jimbo la Hai Mbowe alikuwa na wmawakali katika vituo vyote na bado alishindwa kwa wingi wa kura.

Ukiona jambazi anakwambia "kama unadhani nilivyokupora nimekosa nenda mahakamani" basi ujue kuwa mahakama hiyo pia iko kwenye syindicate ya ujambazi.

Tanzania mahakama haiko huru, imewekwa mfukoni na jiwe
 
Watu wengi kwenye kambi ya upinzani wamekuwa wanadai kuwa Magufuli kabinya demokrasi ilihali huwa wanashiriki uchaguzi na ama wanashinda au wanashindwa kama ilivyo ada ya demokrasia. demokrasia haiana maana kuwa upinzani ndio ushinde tu.

Viongozi huwa hawapimwi kwa mambo ya kawaida bali yale ya kupita (transitional). Jambo transitional ambalo litamhukumu sana Maguful ni jinsi alivyosimamia maambukizi ya Korona. Amelisimamia vibaya sana kiasi kuwa hata wafuasi wake wanaweza kuwa wanakufa bila kujua kuwa wana virusi vya korona. Alizima information yoyote inayohusu korona, na kusahahu kuwa information is power.

Wakati wa ujana wetu (pamoja na yeye) tulipewa information zote kuhusu AIDS na ilitusaidia sana kujua jinsi ya kuikwepa. Sasa hivi information ya Corona haipo kabisa, na watu hawajui namna ya kuikwepa.

Watu wanajoifanya kuwa wanajua kusimamia interests za Watanzania wote wanapiga kelele kwa mambo yanayowahusu interests zao tu, kama kuruhusiwa kufanya maandamano, ambacho siyo kipimo kabisa che demokrasia, lakini sijasikia hata mmoja akizungumzia uongozi wa hili la korona linalohusu umma wa Watanzania wote. Hata wanaoliongelea, wanatumia njia hiyo hiyo ya kuhimiza maslahi yao binafsi.
Ukiongelea demokrasia unaongelea uhuru wa habari. Sio uhuru wa habari za Corona tu. Uhuru wa habari zote siku zote.

Sielewi kwa nini unaona hivi ni vitu tofauti.
 
Vikaragosi ni mawazo ya mchoraji, siyo sheria na wala usiendeshea maisha yako au kutoa mawazo yako kwa kusoma vikaragosi.

Kuogopa kuomba haki yako mahakamani siyo utetezi; fungua kesi halafu ulalamikie uamuzi lakini siyo kulalamika chinichini bila kwenda mahakamani ambako utaonyesha ushahidi wako. Marehemu Mtikila aliishitaki sana serikali mahakamani na kuna mahala alishinda na kule ambako hakuridhika na uamuzi alikata rufaa; ndiyo utaratibu wa sheria

..tatizo ktk utawala wa Jpm mahakama nayo imetumika kama nyenzo ya kuwakomesha na kuwaonea wapinzani na kukandamiza demokrasia.

..miaka ya nyuma wapinzani walikuwa wanalalamikia utendaji wa vyombo vya dola haswa jeshi la polisi kutumiwa na ccm kupambana na wapinzani. lakini ktk awamu hii, kwa mtizamo wa wapinzani, mahakama nayo imejiunga upande wa ccm dhidi ya wapinzani na demokrasia.

..ni katika mazingira hayo ndiyo unaona hakuna ile hamasa ya miaka ya kina Mtikila, Masumbuko Lamwai, na wanaharakati wengine wa demokrasia, kwenda mahakamani kutafuta haki zao. kwa kifupi wapinzani wamepoteza imani kwamba mahakama za tanzania zinaweza kuwatendea haki.
 
Unfortunately, legacy yake baada ya miaka miwili tu ijayo itakuwa ni hii ya Covid-19. Sijajua watu watatafsiri vipi ila ndiyo litakuwa gumzo kuhusu Magufuli. Kulikuwa na maneno machache tu ya kutumika: " wananchi; gongwa hili lipo, na ili yujikinge nalo, wote tutumiea barakoa, tuoshe mikono yetu mara kwa mara, na tusikaribiana sana na watu wengine." Halafu yeye angeongoza kwa kuonyesha mfano huo, lakini alipinga na wala hakuonyesha mfano huo!!!
 
Katika sehemu ulizowahi kutofautiana na Magufuli ni kwenye namna alivyohandle issue ya COVID-19, Unfortunately ubishi wake, na ego yake vimemcost
 
Sijui kama ubishi huo umemcost maisha yake kama uanavyosma kwani hatuna uhakika kuwa kifo chake kimetokana na janga hilo, lakini nadhani hakui-handle vizuri kama kiongozi. Ninajua kuwa alitaka kuwapa watu matumaini na kuwaondolea woga, lakini vile vile alishindwa kuwafundisha kujihadhari.
 
Unfortunately, legacy yake baada ya miaka miwili tu ijayo itakuwa ni hii ya Covid-19. Sijajua watu watatafsiri vipi ila ndiyo litakuwa gumzo kuhusu Magufuli. Kulikuwa na maneno machache tu ya kutumika: " wananchi; gongwa hili lipo, na ili yujikinge nalo, wote tutumiea barakoa, tuoshe mikono yetu mara kwa mara, na tusikaribiana sana na watu wengine." Halafu yeye angeongoza kwa kuonyesha mfano huo, lakini alipinga na wala hakuonyesha mfano huo!!!

..kwanini tusimlaumu Tundu Lissu?

..Lissu ndiye aliyeanza kuropoka-ropoka kuhusu kujikinga, na kupelekea Magufuli kuchukua mtizamo wa kutojikinga.

..Lissu angefuka bakuli lake, leo hii Watanzania tungekuwa na hali nzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom