hitler2006
JF-Expert Member
- Sep 1, 2014
- 489
- 454
Yanayoendelea katika sakata la ubakaji na ulawiti la clip iliyosambaa mitandaoni yanatafakarisha inawezekanaje haya kutokea katika nchi ambayo kiongozi ni mwanamke, Waziri wa ulinzi mwanamke, Spika wa bunge mwanamke, RPC wa mkoa husika lilikotokea tukio mwanamke
Lakini kinachoshangaza zaidi ni ukimya wa viongozi wote wa wanawake wawe wanasiasa, wanataaluma kama wanahabari na wanasheria.
Kama jamii hatupaswi kuhalalisha na kufumbia macho, matukio kama haya ambayo yanaondoa heshima na kutudunisha kimaadili lakini pia ni lazima jamii isimamie utawala wa sheria na usawa mbele ya sheria kwa mustakabali wa umoja na amani ya jamii yetu
Lakini pia tukumbushane kulea watoto katika maadili yanayomkumbusha mtoto wa kiume kumlinda, kumuheshimu mtoto wa kike maana ni mama au dada huyo
Tukumbushane women are the custodian of life they must be protected.
Over