Adui wa pamoja hujenga umoja wa maadui

Adui wa pamoja hujenga umoja wa maadui

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Nyakati na baada ya kifo cha hayati Magufuli, nchi imekuwa na makundi ama yaliyonufaika au kuumizwa:

1) Makundi ya wafayabiashara yaliyoumizwa na ubambikiaji kesi za uhujumu uchumi, na hata kufungiwa accounts zao za benki.

2) Makundi ya wanaCCM ya kale walioumizwa kwa kuachwa nje ya utawala wakati wa marehemu

3) Makundi ya wanasiasa na wakuu wa taasisi wapya, wengi walioteuliwa kutoka kanda moja, walionufaika na utawala wa marehemu

4) Makundi ya wanasiasa wa upinzani walioumizwa na utawala wa marehemu kwa kunyimwa uhuru wa kufanya siasa, kufilisiwa, kubambikiwa kesi, na wengine kufungwa kwa uonevu.

Kuingia kwa awamu ya 6, kuliwapa faraja kubwa makundi karibia yote yaliyoumizwa, isipokuwa lile kundia la 3.

Serikali ya awamu ya 6, kwa kufurahia uungwaji mkono wa makundi yaliyoumizwa ambao haukutegemea sana uwezo wa Rais wa awamu ya 6 bali zaidi ni ile tu kusema, bora tumeondokana na awamu ya 5 iliyotupa madhira mbalimbali, uliweza kufanya lolote itakalo bila ya hofu yoyote.

Taratibu maswali yakaanza kujitokeza juu ya dhamira hasa ya Rais wa awamu ya 6:

1) Mashekhe waliokaa miaka mingi kwa tuhuma za ugaidi wakaachiwa. Baadhi ya waliobambikiwa kesi wakaachiwa. Swali likawa, kama watu wanaweza kuachiwa kwa agizo tu la Rais, je, hakuna uwezekano pia wa kufungwa kwa agizo la Rais pia? Mfumo wetu wa mahakama, kweli upo huru?

2) Rais Samia, bila ya kunukuu kifungu chochote cha katiba wala sheria yoyote, akatoa kauli kuwa hakuna mikutano ya vyama vya upinzani ya hadhara, lakini gizani huenda kulikuwa na maagizo mengine. NCCR wakawa wa wanzoni kuonja shubiri ya Samia. Mama Tanzania akang'aka kweli lakini haikusaidia. Washirika wasio rasmi wa CCM, kama Mbatia nao wakaghadhabika.

3) Rais Samia mara akaonesha chuki kubwa kwa watu wanaohoji maamuzi yake. Wanasiasa walipooanza kudai kurejelewa kwa mjadala wa katiba mpya, akasema wameanza chokochoko, na watu wajue kuwa yeye ni Rais wa jinsia ya kike, tena akasema atakayemzingua, atamzingua. Baada ya agizo lile lisilo la lugha ya moja kwa moja, aliyemzingua, Bwana Freeman Mbowe alikamatwa na kuwekwa mahabusu alipoharibu kutaka kufanya mkutano wa ndani kuhusiana na madai ya katiba mpya. Alimtoa Mdude, wapenzi wa haki wakafurahi kumbe ilikuwa ni kumwachie senene ili twiga apate kuliwa. Wapenzi wa CHADEMA na wapenzi wa haki, wote wakamchukia na kujilaumu kwa kuwa wajinga.

4) Kutoka kundi la wanufaika wa awamu ya 5, mmoja mmoja, wakaanza kupukutishwa. Na kila anayepukutishwa, replacement yake ni kanda nyingine, na imani nyingine. Ni coincidence au mkakati, mjadala upo mtaani.

4) Katikati ya mtifuano wa wanaosononeka, kesi ikiwa katikati, anayesikiliza kesi ambayo serikali ni mlalamikaji, msikilizaji na mtoaji wa hukumu ya kesi anapaishwa cheo kwa vigezo vile vile (wenye akili wanavijua)

5) Mara ikafuata hukumu kwa Sabaya, watazamaji wa mambo juu juu, vigelegele vikapaa, bila kujua kuwa kuna wakati unaweza kufurahia kuchinjiwa kuku, kumbe kuku huyo ndani yake ana sumu. Hapa akapunguza nguvu ya waliomchukia kutokana na Mbowe kuwekwa ndani, akiwaacha wafia imani za awamu ya 5 wakisononeka. Haukupita muda, akawapoza kwa kuhakikisha hasimu wao, Mr Mbowe, anaendelee kuteseka lupango. Kisha akafanikiwa kuwafanya wasononekaji wa Sabaya na Mbowe, waparuane wenyewe kwa wenyewe, huku anaowataka wakisogezwa kuchukua nafasi muhimu kwenye mifumo ya utawala.

HALI YA SASA

1) Wafia imani za awamu ya 5 wananung'unika

2) Wapenda haki wananung'unika

3) Wanaotaka katiba iheshimiwe wananung'unika kuhusu nafasi ambazo siyo za muungano

4) Vyama vya upinzani vyote, hasimu na marafiki wa CCM, vimeudhiwa na maagizo ya Rais ya kuzuia shughuli halali za kisiasa.

Linalotazamwa kwa sasa ni kanuni ile ya adui wa pamoja, itafanya kazi?

"A common enemy of enemies unites enemies against the enemy"

Ikumbukwe kuwa ni wakati wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, ndipo kundi la G55 liliibuka. Zaidi kuibuka kwake kukichochewa na hisia kuwa nafasi ya Urais ilikuwa inawapa nafasi zaidi wazanzibari hasa kwenye vitu visivyo stahili yao kwenye muungano. Teuzi za Wazanzibari kwenye nafasi zisizo za muungano, zikiwa mojawapo. Yale yale ya wakati wa Mwinyi yanaanza polepole kuibuka, lakini je, yataibua G55 nyingine? Tuendelee kufuatilia kwa weledi.
 
Kama kweli vile kumbe umetumiwa kisiasa pia ,nyumbua hoja kisomi zaidi tukutane 2025
 
Ulichokizoea unaweza kudhani kila mmoja anafanya hivyo. Kukubali kutumika ni kukubali kuwa ubinadamu wako haujakamilika. Namshukuru Mungu kwa kuwa ameniumba kamili. Ubinadamu wangu haiwi compromised na kitu chochote.
 
Sawa endelea kujidanganya Aliyekamilika ni Mungu pekee
 
Bandiko pambe.

Tunakoelekea siko.

Hakika tutamkumbuka JPM sasa hivi nchi badala ya kusonga mbele na kuibua miradi mipya iko bize kutengeneza makundi,watu wanatoka mashimoni walikojificha baada ya jemedari kuwakomesha wanataka sasa kujifanya watu huru.

Tusisahau kuliombea Taifa.
 
Sawa endelea kujidanganya Aliyekamilika ni Mungu pekee
Ukamilifu wa mwanadamu ni tofauti na ukamilifu au ukuu wa Mungu. Binadamu ana uwezo lakini uwezo wa mwanadamu hauna ulinganisho na uwezo wa Mungu.

Ukamilifu wa mwamadamu ni pamoja na kukiri kuwa hupo perfect wakati wote. Mwanadamu atakayesema anajua kila kitu, anaweza kila kitu, ubinadamu wake haujakamilika kwa sababu hajui ukomo wa uwezo wa mwanadamu.

Ukamilifu wangu ni katika kujua niyawezayo na nisiyoyaweza, kujua natakiwa kumtumikia Mungu siyo mwanadamu mwenzangu, mwanadamu mwenzangu simtumikii bali naweza kushirikiana maye katika wajibu fulani.
 
Sawa endlea kuwatumikia cdm na vigogo uchwara wanaokulipa
 
Nyakati na baada ya kifo cha hayati Magufuli, nchi imekuwa na makundi ama yaliyonufaika au kuumizwa:

1) Makundi ya wafayabiashara yaliyoumizwa na ubambikiaji kesi za uhujumu uchumi, na hata kufungiwa accounts zao za benki.

2) Makundi ya wanaCCM ya kale walioumizwa kwa kuachwa nje ya utawala wakati wa marehemu

3) Makundi ya wanasiasa na wakuu wa taasisi wapya, wengi walioteuliwa kutoka kanda moja, walionufaika na utawala wa marehemu

4) Makundi ya wanasiasa wa upinzani walioumizwa na utawala wa marehemu kwa kunyimwa uhuru wa kufanya siasa, kufilisiwa, kubambikiwa kesi, na wengine kufungwa kwa uonevu.

Kuingia kwa awamu ya 6, kuliwapa faraja kubwa makundi karibia yote yaliyoumizwa, isipokuwa lile kundia la 3.

Serikali ya awamu ya 6, kwa kufurahia uungwaji mkono wa makundi yaliyoumizwa ambao haukutegemea sana uwezo wa Rais wa awamu ya 6 bali zaidi ni ile tu kusema, bora tumeondokana na awamu ya 5 iliyotupa madhira mbalimbali, uliweza kufanya lolote itakalo bila ya hofu yoyote.

Taratibu maswali yakaanza kujitokeza juu ya dhamira hasa ya Rais wa awamu ya 6:

1) Mashekhe waliokaa miaka mingi kwa tuhuma za ugaidi wakaachiwa. Baadhi ya waliobambikiwa kesi wakaachiwa. Swali likawa, kama watu wanaweza kuachiwa kwa agizo tu la Rais, je, hakuna uwezekano pia wa kufungwa kwa agizo la Rais pia? Mfumo wetu wa mahakama, kweli upo huru?

2) Rais Samia, bila ya kunukuu kifungu chochote cha katiba wala sheria yoyote, akatoa kauli kuwa hakuna mikutano ya vyama vya upinzani ya hadhara, lakini gizani huenda kulikuwa na maagizo mengine. NCCR wakawa wa wanzoni kuonja shubiri ya Samia. Mama Tanzania akang'aka kweli lakini haikusaidia. Washirika wasio rasmi wa CCM, kama Mbatia nao wakaghadhabika.

3) Rais Samia mara akaonesha chuki kubwa kwa watu wanaohoji maamuzi yake. Wanasiasa walipooanza kudai kurejelewa kwa mjadala wa katiba mpya, akasema wameanza chokochoko, na watu wajue kuwa yeye ni Rais wa jinsia ya kike, tena akasema atakayemzingua, atamzingua. Baada ya agizo lile lisilo la lugha ya moja kwa moja, aliyemzingua, Bwana Freeman Mbowe alikamatwa na kuwekwa mahabusu alipoharibu kutaka kufanya mkutano wa ndani kuhusiana na madai ya katiba mpya. Alimtoa Mdude, wapenzi wa haki wakafurahi kumbe ilikuwa ni kumwachie senene ili twiga apate kuliwa. Wapenzi wa CHADEMA na wapenzi wa haki, wote wakamchukia na kujilaumu kwa kuwa wajinga.

4) Kutoka kundi la wanufaika wa awamu ya 5, mmoja mmoja, wakaanza kupukutishwa. Na kila anayepukutishwa, replacement yake ni kanda nyingine, na imani nyingine. Ni coincidence au mkakati, mjadala upo mtaani.

4) Katikati ya mtifuano wa wanaosononeka, kesi ikiwa katikati, anayesikiliza kesi ambayo serikali ni mlalamikaji, msikilizaji na mtoaji wa hukumu ya kesi anapaishwa cheo kwa vigezo vile vile (wenye akili wanavijua)

5) Mara ikafuata hukumu kwa Sabaya, watazamaji wa mambo juu juu, vigelegele vikapaa, bila kujua kuwa kuna wakati unaweza kufurahia kuchinjiwa kuku, kumbe kuku huyo ndani yake ana sumu. Hapa akapunguza nguvu ya waliomchukia kutokana na Mbowe kuwekwa ndani, akiwaacha wafia imani za awamu ya 5 wakisononeka. Haukupita muda, akawapoza kwa kuhakikisha hasimu wao, Mr Mbowe, anaendelee kuteseka lupango. Kisha akafanikiwa kuwafanya wasononekaji wa Sabaya na Mbowe, waparuane wenyewe kwa wenyewe, huku anaowataka wakisogezwa kuchukua nafasi muhimu kwenye mifumo ya utawala.

HALI YA SASA

1) Wafia imani za awamu ya 5 wananung'unika

2) Wapenda haki wananung'unika

3) Wanaotaka katiba iheshimiwe wananung'unika kuhusu nafasi ambazo siyo za muungano

4) Vyama vya upinzani vyote, hasimu na marafiki wa CCM, vimeudhiwa na maagizo ya Rais ya kuzuia shughuli halali za kisiasa.

Linalotazamwa kwa sasa ni kanuni ile ya adui wa pamoja, itafanya kazi?

"A common enemy of enemies unites enemies against the enemy"

Ikumbukwe kuwa ni wakati wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, ndipo kundi la G55 liliibuka. Zaidi kuibuka kwake kukichochewa na hisia kuwa nafasi ya Urais ilikuwa inawapa nafasi zaidi wazanzibari hasa kwenye vitu visivyo stahili yao kwenye muungano. Teuzi za Wazanzibari kwenye nafasi zisizo za muungano, zikiwa mojawapo. Yale yale ya wakati wa Mwinyi yanaanza polepole kuibuka, lakini je, yataibua G55 nyingine? Tuendelee kufuatilia kwa weledi.
Maneno mazuri ila mama yupo. Rais ndiye huteua mawaziri na watendaji wengine. Watanzania wataendelea kuteuliwa kwani ni haki yao. Namna kila mmoja anavyoyaona mambo inatofautiana sana ila wote ni Watanzania na wanayo haki kuyaona wanavyoyaona. Sisi tujadiliane tu. Nimekumbuka: G55 ni historia na historia hutukumbusha ya nyuma ili tupange vyema yajayo.
 
It is not necessarily true that ' the enemy of my enemy is my friend'
 
Unamjua low IQ wew,umesaidia nn Tz zaidi ya kuropoka tu ndugu yangu
Siyo tu nina mchango Tanzania tu bali hata katika Dunia kupitia profession yangu. Ndiyo maana nimefanya na ninaendelea kufanya kazi katika mabara yote, isipokuwa bara moja tu.

Sitegemee kufanya kazi yoyote ya kuteuliwa wala kuchaguliwa. Napenda kuwa na independent mind.
 
Independent mind with poor strategies how can you talk nonsense.
 
4) Kutoka kundi la wanufaika wa awamu ya 5, mmoja mmoja, wakaanza kupukutishwa. Na kila anayepukutishwa, replacement yake ni kanda nyingine, na imani nyingine. Ni coincidence au mkakati, mjadala upo mtaani.
Ikumbukwe kuwa ni wakati wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, ndipo kundi la G55 liliibuka. Zaidi kuibuka kwake kukichochewa na hisia kuwa nafasi ya Urais ilikuwa inawapa nafasi zaidi wazanzibari hasa kwenye vitu visivyo stahili yao kwenye muungano. Teuzi za Wazanzibari kwenye nafasi zisizo za muungano, zikiwa mojawapo. Yale yale ya wakati wa Mwinyi yanaanza polepole kuibuka

Tuambie uwiano wa baraza la mawaziri la mfu.....
Unaamini imani zinazotenganisha watu kwa majina yao, thats is useless.......
I am Pagan by the way.......
 
Back
Top Bottom