Adui wa watanzania sio umasikini, ujinga na maradhi bali ni kuridhika haraka

Adui wa watanzania sio umasikini, ujinga na maradhi bali ni kuridhika haraka

Kuzaliwa wengi rahisi kutajirika kupata cheap labor au free labaur

ulijuaje kama watu weusi wanawahi kuridhika wakati wewe siyo mweusi na wala wewe siyo mtanzania?Na vipi umeweka factors zingine pembeni?
 
hivi nikuulize kwenu mkiwa mmezaliwa 2 na kwa jirani kuna familia ya watu 10,wapi wapo kwenye nafasi ya ku tengeneza maisha?
Usitafute sababu mkuu...ogopa sana mtu anayetoa excuse kwa kila kitu mkuu...!...utatoasababu za nchiyako...serikali, hali ya hewa, , ukoo wako..yaan kila kitu utatoa excuses tegemea kutofanikiwa mpendwa!
 
Miaka ya sabini mwanzoni Mkulima wa kabila la Wahehe Mzee Mamwindi alimua kwa kumpiga risasi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr Kreluu,kisa Mkulima huyo aliendelea kulima shamba kujiongezea mazao kitu ambacho Mkuu wa mkoa hakutaka, tena siku ya Xmas.
Kilichofuata wakulima wa eneo hilo la Isimani walinyanganywa ardhi,mwisho wake ilipiga njaa kubwa nchini sababu ya upungufu wa mahindi yaliyokuwa yakizalishwa Isimani.Wakati huo Isimani ilikuwa eneo lililozalisha mahidi kwa wingi Africa Mashariki.
Mimi nafikiri kuwa sera za serikali ndio zimekatisha tamaa mtu kujiongeza.
 
Bongo ukimiliki Toyota Athletic, I phone na una kijumba chako Goba unaona dunia yote yako.
 
Miaka nenda rudi tumeimbishwa na wanasiasa kuwa adui mkubwa wa watanzania wengi ni umaskini, ujinga na maradhi Mimi nilichogundua sio kweli tatizo kubwa ni kuridhika haraka

Mfano tumeridhika na dawa za wazungu ndio maana hatugundui zetu, tumeridhika na elimu ya wazungu ndio maana hatuna yetu , tumeridhika na kakilimo ketu na kakipato ketu na makazi yetu Mungu atupe nini

Mainchi matajiri watu wake hawaridhiki haraka ndio maana kutwa hugundua na hutaka kwenda mbele zaidi kwenye maeneo yote ya maisha iwe kilimo,biashara,kipato,ufundi,elimu nk.

Akina bakhresa Ni mabilionea sababu hawaridhiki kiwango Chao Cha kutoridhika Kiko juu

Kiwango Cha kuridhika watanzania wengi haraka kwa watanzania wengi ngozi nyeusi kiko juu kuliko wahindi,waarabu na wazungu
Mkuu Yehodaya, suala ni "perception" tu, tulipopata uhuru na hatimaye kuishi chini ya mfumo wa chama kimoja, maradhi, ujinga na umaskini vilihebika kama maadui wakubwa watatu wa taifa letu ambalo lilikuwa changa. Hiyo ilikuwa ni ajenda ya kitaifa na tuliaminishwa hivyo na wale wazalendo wa kweli wakiongozwa na Baba wa Taifa.

Lakini baada ya kuongezeka kwa adui wa nne, yaani "uduni wa sayansi na teknolojia" na huku tukiachwa nyuma sana na maendeleo ya kidunia. Basi chama tawala kimeamua ku "capitalize" ndani ya maadui hawa. Kimkakati chama hiki kimeamua kugeuza maadui hawa kuwa ndiyo ngome na mtaji wake wa kura zao nyakati za uchaguzi na hata kuzidi kupata ridhaa ya kuitawala nchi hii kidemokrasia.

Kwa kuwa kimeamua kwa makusudi kupata kuungwa mkono na wajinga wengi, huku ikikabiliana na wenye akili na maono wachache ili kuzidi kuficha udhaifu wao. Ebu jaribu tu kuangalia wabunge wengi wa upinzani walipotokea, kwa kulinganisha na wale wa chama tawala. Jambo moja ambalo utaliona ni kwamba CCM inafaidika sana na mtaji wa lindi la umaskini wa kutupwa na ujinga wa wapiga kura wasiojielewa.

Nafikiri hata ktk hili gonjwa la COVID-19, utaona kwa jinsi gani viongozi wake wanavyotafuta njia za kijinga na kimaskini ili kufarahisha nafsi zao, huku wakipingana na kukwepa kwa makusudi masharti muhimu sana afya kuendana na miongozo ya WHO.
 
Miaka nenda rudi tumeimbishwa na wanasiasa kuwa adui mkubwa wa watanzania wengi ni umaskini, ujinga na maradhi Mimi nilichogundua sio kweli tatizo kubwa ni kuridhika haraka

Mfano tumeridhika na dawa za wazungu ndio maana hatugundui zetu, tumeridhika na elimu ya wazungu ndio maana hatuna yetu , tumeridhika na kakilimo ketu na kakipato ketu na makazi yetu Mungu atupe nini

Mainchi matajiri watu wake hawaridhiki haraka ndio maana kutwa hugundua na hutaka kwenda mbele zaidi kwenye maeneo yote ya maisha iwe kilimo,biashara,kipato,ufundi,elimu nk.

Akina bakhresa Ni mabilionea sababu hawaridhiki kiwango Chao Cha kutoridhika Kiko juu

Kiwango Cha kuridhika watanzania wengi haraka kwa watanzania wengi ngozi nyeusi kiko juu kuliko wahindi,waarabu na wazungu
Kumbe una akili bwawa mdogo
 
Back
Top Bottom