Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Hakika ni kweli kabisa... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Niliwahi kumwombia mke wangu kama nimekukosea haswa hupaswi kunisemea kwenu ni Bora unisemee kwetu
 
Unajua mahusiano yanachangamoto nyingi sana, na hazifanani. Kila mmoja kwa sehemu yake anapitia changamoto katika mahusiano. Sasa inapotokea umefanyiwa mabaya na mtu uliyenae kwenye mahusiano, sio jambo zuri kuyaweka wazi mabaya yake hasa kwa ndugu zako au watu wako wa karibu sana.

Unajua mapenzi yana nguvu sana, kuna baadhi ya scenarios zinatokea kwa watu hadi unajisemea kwamba "its over between these two" lakini unakuja kuwa surprised after awhile unakuta wako pamoja as if nothing happened.

Nina jamaa yangu ashawahi mkuta mpenz wake amebananishwa uchochoroni na jamaa, ilikuwa usiku tunatoka kuangalia mpira, na kama tungechelewa kidogo tungekuta wanafanya mapenzi. Jamaa alikuwa disappointed sana kiasi kwamba nikajua ndo mwisho wa penzi lao, ila after siku kadhaa naona wako pamoja as if nothing happened. Sikumshangaa jamaa,japo yule Shem wangu Wala simchangamkii kama ilivyokuwa zamani.

Point ya kuandika huu uzi ni kwamba, ikitokea umegombana na mtu ambae uko nae katika serious relationship, tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki, nakusihi hutakiwi kuyaanika mabaya yake Kila sehemu, maana kesho ni fumbo.

Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana.

Kuna wale watu ambao kipindi upo kwenye mapito ndio waliokuwa faraja Yako, ndio waliokuwa wanahakikisha hujidhuru, wanahakikisha furaha yako inarudi, so ikitokea wewe umemsamehe, wao wanaweza wasimsamehe. Na kutomsamehe kwao kunatokana na kumbukumbu zao jinsi ulivyokuwa unapitia hali ngumu sababu ya huyo mtu wako. Au jinsi wao walivyokuwa hawafanyi mambo yao kwa uhuru ilimradi kuhakikisha wanakufariji wewe.

Wewe utampa second chance,ila wao hawatakaa wampe hiyo nafasi. Na inawezekana wasimpe tena ule uzito waliokuwa wanampa awali.


That's All (Ni hayo Tu).

Analyse
Great thinker
 
Kuna mchizi nilikua nakaa nae geto. Hali ngumu msoto wa hali ya juu, msoto pro max hata hela ya kula ni kwa manati.

Sasa kuna kipindi dem wake alikua anataka ada, akanitonya juu juu tu ikaisha. Kwa mawazo yangu niakjua kabisa bw mdogo hana hiyo hela na pia sidhani kama anaweza mlipia ada ya chuo dem wake.
Alooo mapenzi yana nguvu sana, baada ya ule msoto wetu kupungua na dem kumpiga tukio la kihistoria jamaa(aliolewa na mchizi mwingine) ndo jamaa akaanza kunipa story.

Kiufupi jamaa alimsaidia dem laki 5 ya ada, alichangisha mchango ndgu zake huko akamtumia dem pesa.

Kwakua msoto ulishapita sikusikitika sana ila niliona jamaa ni hamnazo kabisa, yaani yeye hela ya kula ni kwa manati halafu anahonga namna hiyo. Anaingiza 0 anahonga laki alooo.

NB. Huyo dem yuko nae mpaka leo.
 
Back
Top Bottom