Adv. Tenzi afungua kesi ya kumtaka Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aachie ofisi baada ya kusema kwamba alimwandikia rais barua kujiuzulu

Adv. Tenzi afungua kesi ya kumtaka Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aachie ofisi baada ya kusema kwamba alimwandikia rais barua kujiuzulu

Hii kesi imenikumbusha kesi ya Wakili mmoja Mhuni huko Kenya aliuefungua madai dhidi ya Mungu. Na Mahakama ikamkubalia ila kabla ya kusikiliza Kesi yake, mahakama ilitoa samansi ya kupelekwa kwa Mungu aje mahakamani kusikiliza Kesi dhidi yake. Mpaka leo yule Wakili Mhuni ana samansi anamtafuta Mungu! Ahahahahaha!!!
🤣🤣🤣
 
Sasa kama Rais anasema hadharani kuwa amepokea barua ya kuomba kujiuzuru ndugu makamu wa rais tuache kuamini. Mahakaa ingemuamuru rais alete hiyo barua. Maana kauli yake ilitolewa katika vikao rasmi. Vinginevyo tuendelee kupuuza maneno yeyote anayosema rais katika vikao/mikutano.
🤝
 
Kesi za kijinga kama hizi, mahakama ingekuwa inaziondoa kwa gharama (cost). Hii ingeondoa wimbi la majitu majinga kufungua mashauri kwa nia ya ku-embarrass
 
Kwani kutamka na kuandika barua na tarehe....kujiuzulu ambapo ni mwisho term hii kabla uchaguzi ni kosa ? Labda asingeandika muda ni lini tungesema siku alipotoa barua ndio siku anatakiwa kustaafu....kuacha ofisi
 
Kwani ukiandika barua ya kujiuzulu si ni lazima Rais aipokee, Aisomee na kikukubaria/Kukujibu.

Au mm ndo sielewei.

Pia nadhani mahakama ilikua na wajibu wa Kuomba barua iletwe mahakamani na Wawakilishi wa Rais ili iweze kutafsiri kisheria kama Hyo nafasi iko wazi.

Mwisho, Kivyovyote vile hili swala bado linaonesha we are very unprofessional n kama mambo yanaenda enda tu
 
Hivi karibuni Tarehe 19 January, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM alisema kwamba amekuwa akipata ombi kutoka kwa Makamu wa Rais Mh. Dr. Philip Mpango la yeye kujiuzulu nafasi yake ya Umakamu na hata baadaye Dr. Mpango alimpelekea Rais Barua rasmi ya kujiuzulu.

Sasa mwananchi mmoja ambaye pia ni Wakili kwa majina ya TENZI ANTHONY NYUNDULWA alikwenda Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma akiwashtaki Dr. Philip Mpango pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba wamevunja sheria za nchi pamoja na Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtu huyu alienda kuomba kibali cha mahakama ili aweze kuleta maombi ya mapitio ya kimahakama kwaajili ya Mahakama Kuu kutamka kwamba ofisi ya Makamu wa Rais ipo wazi tangu Makamu alipowasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais, Mahakama imwamuru Rais Samia kupendekeza jina la mtu mwingine ili awe Makamu wa Rais na zuio kwa Philip Mpango kusimama kama Makamu wa Rais kwakuwa nafasi yake iliondoka tangu alivyokabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Rais.

Mleta maombi haya Wakili Tenzi anaendelea kusema kwamba, kitendo cha Rais Samia kupokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa Dr. Mpango na kutotamka kwamba ofisi ya Makamu wa Rais ipo wazi ni uvunjifu wa katiba na kufanya ofisi ya Makamu wa Rais kuwa chini ya mtu ambaye nafasi yake ni tata na ya mashaka.

Sasa kikawaida ili kesi kama hizi (kesi za kibali cha mapitio ya kimahakama) zikubaliwe na mtu apewe kibali na Mahakama ni lazima athibitishe baadhi ya mambo kama, kuwa na hoja katika jambo hilo, kuwa na maslahi na jambo hilo, lazima pia uambatanishe nakala ya maamuzi kama unataka ku-challenge maamuzi ya taasisi au mtu fulani, pia maombi ya kibali yafailiwe ndani ya muda (miezi sita tangu uamuzi ufanyike) na kusiwe na nafuu nyingine nje ya mapitio ya kimahakama.

Sasa katika kesi hii Mleta maombi aliuilizwa na Mahakama atoe barua ambayo Dr. Philip Mpango alimwandikia Rais Samia kujiuzulu ili mahakama iamini kama hilo swala lipo na kulitolea maamuzi kama anavyotaka., maana tofauti na hapo mahakama itakuwa inacheza kamari au kubeti sw

ala ambalo haipo tayari kulifanya.

Mleta maombi hata hivyo alishindwa kuileta barua hiyo mahakamani na hatimaye maombi yake yakaondolewa mahakamani kwakuwa madai yake ni fununu tu ambazo ameshindwa kuthibitisha.
Ila kiukweli CCM hawana Mwenyekiti anayejua Katiba hata ya chama chake .
Mgombea urais aliyepitishwa kichawa chawa bila hata kuomba kura wala kuchukua fomu ndani ya chama.
Yaani tunaambiwa tu kuwa huyu amefanya mambo mazito hivyo asitokee mtu mwingine kugombea . Lakini wakati huo huo hajui chochote mpaka asaidiwe na watu wengine ikiwemo machawa na wastaafu .
Kama angefanya mambo makubwa jambo la kwanza tungeona waziri wake mmoja tu mzalendo ,mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia na kulinda mali za umma kwa gharama yoyote hata kutoa uhai wake na kuamini katika uadilifu badala ya kushindana kula kwa urefu wa kamba zao na kujilimbikizia mali Fasta Fasta , kama ilivyokua kwa watangulize wake kama JPM , JK, BM , AHM na JK Nyerere:-
Wakati wa Nyerere tulimuona :-
Sokoine ,
Mwinyi ,
Salm Ahmedi Salim .
C. Msuya na Warioba

Mwinyi tukamuona
Mrema ,
Horasi Kolilba
Mkapa ,
Kikwete alienda akafunga akauti za Mzaramo mmoja aliyeficha pesa huko ulaya .

Wakati wa Mkapa wakatokea akina ,
Magufuli ,
Lowasa waziri wa maji mwenye maamuzi magumu sio hizi sanaa za kusifia sifia za Leo ,

Utawala wa JK hakuibua mtu mpya hata mmoja lakini aliendelea na majembe kama:-
JP Magufu
Lowasa tena kwa sababu ya wananchi kuwakubali hao watu.
Angalau na
Anna Tibaijuka
Asharose Migiro
Bernard Membe n.k.

Wakati wa Awamu ya Tano ya JPM ;
Tukawa na Wazalendo pia walioibuliwa na utawala wa awamu hiyo kama vile :-
Kasimu Majaliwa .
Luhana Mpina .
Bashiru Ally .
Kabudi
Halfrey Polepole.
Paulo Makonda
Philip Mpango
Spika Ndugai
angalau na
Tulia Akson pamoja na kwamba kwa sasa amekengeuka kwa kujiingiza kwenye ufisadi na kushinda kukemea Uovu na kuiwajibisha serikali kwa kulinda ugali wake . Lakini ameibuliwa from ziro to Hiro.

Tuangalie baada ya kuwekwa kwa mtawala wa Awamu ya Dr. Samia ya asiye na uchungu wa kuomba Kura hata ndani ya Chama chake . Yaani amepata umakamu kwa michongo na urais kwa nguvu ya Kakikundi kusikojulikana ndani ya CCM na sasa kakikundi hako hako kanampitisha bila kura bila utaratibu utafikiri anaenda kusimamia kikao cha kicheni Party kumbi ni Mustakabali wa taifa lenye watu mil. 60.
Yaani Rais wa mchongo kwenye Ulimwengu uliozungukwa na marais wababe wa dunia kama Trump, Kiduku,Putin, Kagame ,Ibrahim Traore, Natanyahu ,Museveni , Husein Mwinyi n.k.
Anatuletea wasaidizi wake kwa kuangalia upana wa vifua na uso wa kutisha kama vile ;
Mchengerwa
Wasira
Wapambe kama Mwijaku.
Hamonaizi.
Na List ya watu wakorofi wakorofi tu na wenye Shari shari kwa kuwatisha wapiga kura na wapinzani basi . Lakini hakufanikiwa kabisa kutuletea hata mtu mmoja mzalendo na anayepinga ufisadi kuanzia ndani ya baraza la mawaziri mpaka nje .
Angalau kidogo CDF ni mzalendo japo hasikilizwi maana hana mtandao wa kifisadi na wapambe mafisadi mwingine ni Kaganda yule wa Polisi ambaye pia ameshamtoa kupisha mafisadi ndani ya mfumo

Ni wazi kuwa Mama ni mzizi mkuu wa mafisadi ndio maana hana marafiki wazalendo wala mtandao huo hana katika teuzi zake .

Tumebakiwa na Mtu mmoja tu Watanganyika katika Duniani hii inayokaliwa na waovu na kuneemeka juu ya neema za Mwenyezi Mungu alizowaumbia watu wema . Huyu ni Tundu Antipas Lisu .
Wazalendo wote na wanyonge wa nchi hii tumuunge mkono kwani lengo la mafisadi ni nafsi zao tuu na familia zao kupitia rushwa na vitisho na kuua. Tukatae huu mfumo wa kuweka watawala kihuni kwa kutumia risasi na mabomu kwa mgongo wa uchaguzi feki unaogharimu pesa nyingi.
Leo hii majeshi yanahangaishwa na kwenye maandalizi ya kutumia nguvu kupora uchaguzi wakati hawalipwi hata pesa za kusafirisha familia zao baada ya kustaafu wala pesa za kula wanapokuwa kwenye safari za kijeshi.

RIP JPM .
Karibu TUNDU Antipas Lisu utuletee mifumo imara ya kiutawala na uongozi katika taifa kwa vizazi vilivyopo na vile vijavyo.
 
Tunaomba hiyo barua kwanza ili sote tujiridhishe, isijekuwa Daktari Filipo anachafuliwa bure.
Au wakati anaongea(Philip Mpango)alikuwa intoxicated/under influence of kikombe/alilewa.Hilo nalo litazamwe.Na hata yawezekana AI ilitumika.
 
Jamaa Alifungua Kesi Kutumia Hisia Zake 🤣🤣
Na Matamshi ya Rais Akasahau mahakamani Kunapelkwa Ushahidi sio maneno
Hivi mtu akikutukana matusi au kukutishia kuondoa uhai wako, huwezi kumfungulia kesi hadi hilo tishio au matusi viwe katika maandishi?
 
Hii kesi imenikumbusha kesi ya Wakili mmoja Mhuni huko Kenya aliuefungua madai dhidi ya Mungu. Na Mahakama ikamkubalia ila kabla ya kusikiliza Kesi yake, mahakama ilitoa samansi ya kupelekwa kwa Mungu aje mahakamani kusikiliza Kesi dhidi yake. Mpaka leo yule Wakili Mhuni ana samansi anamtafuta Mungu! Ahahahahaha!!!
..haya mambo inatakiwa Akili kubwa kuyaelewa...Wakili amefanya hivyo kuonesha udhaifu wa yanayoendelea huko juu.Mungu akimpenfa namba Moja ndio utaelewa kilicho chini ya zulia .
 
Hii kesi imenikumbusha kesi ya Wakili mmoja Mhuni huko Kenya aliuefungua madai dhidi ya Mungu. Na Mahakama ikamkubalia ila kabla ya kusikiliza Kesi yake, mahakama ilitoa samansi ya kupelekwa kwa Mungu aje mahakamani kusikiliza Kesi dhidi yake. Mpaka leo yule Wakili Mhuni ana samansi anamtafuta Mungu! Ahahahahaha!!!
😂😂😂
 
Hivi mtu akikutukana matusi au kukutishia kuondoa uhai wako, huwezi kumfungulia kesi hadi hilo tishio au matusi viwe katika maandishi?
Kama Utapeleka Mashahidi ambao watathibitisha Kweli Maneno yale ya Kutishia aliyasema Mbele yao Wakisikia Basi unaweza Kumfungulia Kesi
 
Back
Top Bottom