Aendelee ama asiendelee.

Aendelee ama asiendelee.

fundiaminy

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2009
Posts
354
Reaction score
52
je?kama mke uliye nae kwa wakati huu mlikuwa mkienda pamoja disco na sehemu mbalimbali za starehe kabla hamjaoana,ni sawa uzidi kwenda nae ama mke nyumbani mume ulabu na marafiki?na je,unaweza kumruhusu aende pekee sehemu hizo nilizotaja?sinema,ukumbi wa disco n.k.
 
Kama ulikuwa unaenda naye kabla hamjaoana kwa nini baada ya kuoana uache kwenda naye?? Itakiwa uendelee kwenda naye kwani ndiyo kikolezo cha upendo wenu. Ukianza kubadilika kihasi basi ni alama ya kuanza kupungua kwa upendo, vinginevo una sababu ya kweli ya kutokwenda. Na hapo anaweza kwenda mwenyewe. Yafaa kumwamini.
 
Hivi kama mke mwenyewe nilikutana naye Club, kweli nimruhusu aende kujirusha mwenyewe bila kuhofu kuwa anaweza kukutana na wengine kama alivyokutana na mimi?

Just thinking aloud...
 
hapo ndugu ndio panapoleta balaa.aende peke yake.?na vile hizo sehemu hazitambui nani kaoleka nani bado,kwangu inakaa ngumu.
 
ukisha kuwa na familia, mambo ya kujirusha inabidi uyaangalie sana - imagine una watoto - mnamwachie mfanyakazi - mnaenda kujirusha - kwanza watoto wakikuwa wanajifunza nini kwa parents??? isitoshe unakuta familia mfanyakazi ndio kiongozi wa familia - wenye nyumba busy kujirusha - hadi lini?? ni vyema ukiamua kujenga familia - ujenge familia yenye maadili mema - kama ni kutoka - mtoke wote wawili - kwa mpango maalumu - otherwise - ndio mwanzo wa mafarakano katika familia - watoto kutopata mapenzi na malezi ya wazazi - nao wanajiingiza kwenye mambo ya ajabu ajabu na kupata upendo kwa marafiki ambao saa ingine wanaweza kuwa-mislead - e.g. kuvuta bangi, drugs - kutofanya vizuri kwenye masomo etc. MUME na MKE ni wajenzi wa familia - baada ya kuamua kuishi pamoja - Mungu atawale maisha yenu full time - hapo mtawin
 
je?kama mke uliye nae kwa wakati huu mlikuwa mkienda pamoja disco na sehemu mbalimbali za starehe kabla hamjaoana,ni sawa uzidi kwenda nae ama mke nyumbani mume ulabu na marafiki?na je,unaweza kumruhusu aende pekee sehemu hizo nilizotaja?sinema,ukumbi wa disco n.k.


Endeleeni ila kwa sasa mke isiwe mara nyingiii sana ili akae home na kuangalia totos. Unataka kwenda peke yako kila siku ili ukachukue mizigo au?
 
Unapaswa utofautishe maisha ya ujana na utu uzuma.huwezi kuwa kila siku wewe ni kijana tu.kama kutoka ni mipango maalum siyo eti uwe kama zamani kutoka kila siku.wakati huu ukumbuke kuwa una familia ya kuangalia.

Ally kilunguzo salum
 
Haitakiwi kupunguza mapenzi baada ya kuoana, maana kitendo cha kumuacha mwenzio home kila unapotoka out ni sehemu mojawapo ya mapenzi kupungua. Inapaswa utoke na wife wako ndio inaleta heshima hata kwa wale wanaopenda kuharibu mahusiano ya watu wanashindwa waanzie wapi.
 
ni kweli kuna wakati wa ujana na uzee.lakini hebu tizama wakati mkichumbiana ama hata mlipo oana pengine hukuwa na kazi.wakati huu uko na kazi na marafiki wapya kazini.hivi 2seme kweli bila kuficha unapoamua kukutana na marafiki wikendi,je mtakuwa mnabebana na wyf kila mahala?na 2kumbuke sio marafiki wote 2lio nao wameshaoa jameni.na hata kama ndio wameoa je,nao watatoka na wake zao?
 
Back
Top Bottom