Afa baada ya kumaliza kuchimba kaburi la rafikiye

Afa baada ya kumaliza kuchimba kaburi la rafikiye

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KATIKA hali isiyo ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Kalinywa (35-40) mkazi wa Mlandizi amefariki dunia wakati akichimba kaburi la rafiki yake aliyetambulika kwa jina moja la Rajabu.

Mkasa huo uliotokea Mlandizi Kibaha Pwani juzi, wakati marehemu Kalinywa akiwa na wenzake watatu wakichimba kaburi hilo.

Akisimulia mkasa huo, mmoja wa waombolezaji, mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Shaabani Mguta, alisema siku ya tukio marehemu Kalinywa akiwa na wenzake watatu aliowataja kwa majina ya Bw. Bosco Bosco, Bw. Mohamed Juma maarufu kwa jina la 'Mtanzania' na Bw. Juma Mabunduki, walipewa jukumu la kuchimba kaburi hilo baada marehemu Rajabu kufariki.

Kabla ya kuanza kazi hiyo, waliomba pesa za kununulia gongo ili wanywe kwanza kabla ya kuanza kazi hiyo kwa maelezo kwamba marehemu kabla ya kifo chake, aliwaachia wosia kwamba akifa, watakaochimba kaburi lake, lazima wanywe kwanza pombe hiyo.

Ombi hilo lilikataliwa na waombolezaji, ndipo walipoamua kuchangishana wao na kupata sh. 9,000 zilizowawezesha kununua lita tano za gongo.

"Walifika eneo la msiba na kueleza kwamba marehemu rafiki yao (Rajabu) aliwaachia wosia kwamba akifa, kaburi lichimbwe na rafiki zake wa karibu na wote wawe wamekunywa gongo," alisema Bw. Mguta.

Alisema marehemu Rajabu kabla ya kifo chake, alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Kalinywa na walishirikiana katika mambo mengi ikiwa pamoja na kunywa.

Mwombolezaji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Hamis Koroboto aliliambia Majira kuwa kabla ya marafiki hao wa marehemu kwenda kuchimba kaburi, aliwaomba wanywe chai na kiporo cha ubwabwa kwanza lakini walikataa jambo hilo.

"Walikuwa wakipokezana, anayetoka shimo anakwenda kuchukua gongo na kunywa huku akisubiri zamu ya kuingia tena kuendelea kuchimba," alisema Bw. Kiroboto.

Alisema baada ya kukamilisha shughuli hiyo
marehemu Kalinywa alikuwa wa kwanza kutoka na kujipumzisha juu ya kaburi lililokuwa pembeni yake.

Baadaye wenzake walitoka na kujipumzisha kando na kutuma taarifa msibani kuwa kaburi limekamilika hivyo mwili wa marehemu Rajab uletwe kuzikwa.

Alisema waombolezaji walipofika na mwili huo makaburini walikumbwa mshangao kukuta wachimba kaburi wote watatu wamelala fofofo na hawajitambui.

"Tulipigwa butwaa ndipo tulijaribu kuwanyanyua kujua kilichowasibu, hatukuamini Kalinywa alikuwa amekufa na wenzake walikuwa taabani wakipumua kwa mbali," alisema Bw. Kiroboto.

Alisema walichoamua ni kumzika kwanza marehemu Rajab na baada ya hapo waliuchukua mwili wa marehemu Kalinywa kuurejesha nyumbani kwa Rajabu kuanza msiba mpya.

"Wakati tukizika wengine waliendelea kupewa huduma ya kwanza, kwa bahati nzuri walizinduka. Baada ya mazishi tulibeba mwili wa marehemu Kalinywa kurudisha nyumbani" alisema.

Mmoja wa waombolezaji waliobaki nyumbani kwa marehemu Rajabu aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Mcharazo, alisema baada ya waombolezaji hao kufika wakiwa na machela iliyochukua mwili wa Kalinywa, watu walitaharuki huku baadhi ya akina mama wakijaribu kukimbia kuhofia kulikoni kilichojiri makaburini hadi kurudi na mwili wa marehemu nyumbani.

Habari zaidi kutoka kwa jamaa wa marehemu Kalinywa zilieleza kwamba baada ya mwili huo kuwekwa kwa muda nyumbani kwa msibani hapo ulipelekwa kijijini jirani cha Marangaranga Mzenga alikokuwa akiishi marehemu Kalinywa.

Kamanda wa Polisi MKoa wa Pwani, Bw. Henry Salewi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema amepata taarifa hizo na jeshi lake linaendelea kufuatilia kupata taarifa zaidi.
 
-MAISHA YA KUBANGAIZA..DHIKI ILIYOKITHIRI...UKOSEFU WA ELIMU...Ama kweli nawaonea huruma hawa watu..Inasikitisha!
 
Mungu aziweke roho ya marehemu hao mahali pema peponi
 
innalilahi wainna ilayhi raajiiun,afana audhubilahi mindhalika,mungu atunusuru kufa katika hali hiyo.
 
DAH!raha ya milele uwape ee bwana!..NA MWANGA WA MILELE UWAANGAZIE.wapumzike kwa amani-AMINA
 
Dah inasikitisha sana wamekufa pamoja na wangezikwa kaburi moja.
Poleni jamani
 
Gongo lita 5 halafu unafanya kazi ya kutumia nguvu na mapafu. Sitetei mnywa gongo. Kukosa elimu na umaskini ni kifo. Hivi nyie mafisadi mnaokarabati nyumba kwa bilions of money mnafahamu kuwa kuna watanzania wanaishi katika hali ya kubahatisha?? Nina hasira.
 
Tanzania hatuna ma director wazuri kama hollwood tungeongoza kwa movie zenye hisia kali duniani.

RIP
 
Poleni wafiwa wote
Kifo ni kifo jamani na kila mmoja ana aina yake ya kifo
RIP Rajabu na Kalinywa. Hakika nyie mlikuwa marafiki wa kweli
 
Gongo lita 5 halafu unafanya kazi ya kutumia nguvu na mapafu. Sitetei mnywa gongo. Kukosa elimu na umaskini ni kifo. Hivi nyie mafisadi mnaokarabati nyumba kwa bilions of money mnafahamu kuwa kuna watanzania wanaishi katika hali ya kubahatisha?? Nina hasira.
Tukimbilie wapi sisi maskini,sisi ndo tuwachague na sisi ndo tunyanyasike.R.I.P bwana Ramadhani Kalinywa
 
Mungu aziweke roho ya marehemu hao mahali pema peponi
Mungu hapokei rushwa.
kama waliamua kutenda dhambi wakidhani watarehemeka ujue wamecheza potea.
Mungu awafariji wafiwa
Amen
 
So sad... haya ndio maisha ya watanzania wengi

RIP
 
Mungu hapokei rushwa.
kama waliamua kutenda dhambi wakidhani watarehemeka ujue wamecheza potea.
Mungu awafariji wafiwa
Amen

...Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, nani angesimama...
 
Back
Top Bottom