Afadhali niendelee kuitwa Mzee kuliko kuvaa nguo zisizo na staha

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habarini waungwana

Nimebadili mtindo wa mavazi lakini bado napewa salamu na wadogo zangu mtaani.

Uzi wangu wa kwanza hapa JF nilisema kwamba wengi wanakosea kutafsiri umri wangu mitaani, wanadhani nina umri mkubwa kumbe bado sijafika huko.

Nilipata maoni na wengi walinishauri nibadili style ya mavazi yangu, nilijaribu kufanya hivyo lakini sikuona matokeo yoyote.

Nimeshindwa kuvaa nguo za vijana wa mjini hasa jins za kubana, T shirt zenye picha ya 2 pac, vipensi vifupi mapaja yote nje, au zile suruali pana mithili ya kitambaa cha mashine ya kusaga unga.

Nimeamua kuendelea kuvaa kama mwazo tu, yaani simple shati na suruali ya kitambaa au cadet. Japo still naitwa mzee lakini sina budi kukubaliana na hali halisi.

Ni heri niitwe mzee lakini sio niitwe barobaro au bishoo.

Rejea: Watu wanadhani umri wangu ni mkubwa tofauti na umri wangu halisi, je sababu yaweza kuwa nini?
 
images (26).jpeg

Kwahiyo kamanda unavaa hivi ?
 
Habarini waungwana

Nimebadili mtindo wa mavazi lakini bado napewa salamu na wadogo zangu mtaani.

Uzi wangu wa kwanza hapa Jf nilisema kwamba wengi wanakosea kutafsiri umri wangu mitaani, wanadhani nina umri mkubwa kumbe bado sijafika huko.

Nilipata maoni na wengi walinishauri nibadili style ya mavazi yangu, nilijaribu kufanya hivyo lakini sikuona matokeo yoyote.

Nimeshindwa kuvaa nguo za vijana wa mjini hasa jins za kubana, T shirt zenye picha ya 2 pac, vipensi vifupi mapaja yote nje, au zile suruali pana mithili ya kitambaa cha mashine ya kusaga unga.

Nimeamua kuendelea kuvaa kama mwazo tu, yaani simple shati na suruali ya kitambaa au cadet. Japo still naitwa mzee lakini sina budi kukubaliana na hali halisi.

Ni heri niitwe mzee lakini sio niitwe barobaro au bishoo.

Rejea: Watu wanadhani umri wangu ni mkubwa tofauti na umri wangu halisi, je sababu yaweza kuwa nini?
mkuu wewe kama mimi. kwanza natafuta cardet ambazo hazibani sana miguuni nimekosa. nimeenda hadi msasani mall, sijapata maana mimi visuali vya kubana kwa kweli vinanikosesha raha
 
Nguo za kubana kiukweli hazipendezi, hasa kwa mtu ambaye unajali heshima ya muonekano wako.

Ila endelea kutafuta unaweza ukapata size nzuri itakayo kutosha
 
Kwani mashavu yameanza kushuka au? Mbona mimi nipo kwenye early 30's lakini vitoto vya early 20's ama hata around 17 vinaniambia mambo bro ama niaje kaka.

Utakuwa una muonekano wa kizee ndugu yangu. Lakini kwani kuamkiwa inakukera nini hasa mkuu?

Mimi hata mtu wa rika langu ama mkubwa kwangu akiniambia shikamoo ningeitikia kiroho safi kabisa 'marhaba mdogo wangu'.
 
Back
Top Bottom