Afadhali niendelee kuitwa Mzee kuliko kuvaa nguo zisizo na staha

Afadhali niendelee kuitwa Mzee kuliko kuvaa nguo zisizo na staha

Habarini waungwana

Nimebadili mtindo wa mavazi lakini bado napewa salamu na wadogo zangu mtaani.

Uzi wangu wa kwanza hapa JF nilisema kwamba wengi wanakosea kutafsiri umri wangu mitaani, wanadhani nina umri mkubwa kumbe bado sijafika huko.

Nilipata maoni na wengi walinishauri nibadili style ya mavazi yangu, nilijaribu kufanya hivyo lakini sikuona matokeo yoyote.

Nimeshindwa kuvaa nguo za vijana wa mjini hasa jins za kubana, T shirt zenye picha ya 2 pac, vipensi vifupi mapaja yote nje, au zile suruali pana mithili ya kitambaa cha mashine ya kusaga unga.

Nimeamua kuendelea kuvaa kama mwazo tu, yaani simple shati na suruali ya kitambaa au cadet. Japo still naitwa mzee lakini sina budi kukubaliana na hali halisi.

Ni heri niitwe mzee lakini sio niitwe barobaro au bishoo.

Rejea: Watu wanadhani umri wangu ni mkubwa tofauti na umri wangu halisi, je sababu yaweza kuwa nini?
Una paja?
 
Huyo alie kwenye avatar ni wewe Mkuu?

Kama ndio wew mbona kama kweli umezeeka hivi
 
Mbona muonekano wako unakupendeza
1724063704128.jpg
 
Back
Top Bottom