Afadhali ushike jembe ukalime, kuliko kuomba sala hii

Nguvu alikuwa nayo na akili zake ni zaidi ya kwako wewe na inatoka kwa Mungu baba.
Hadi anachongewa Masanamu yake yanayo sujudiwa usiku na mchana:
Msijitoe ufahamu
Imeandikwa:

Kutoka 20:4
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
........
Tumia muda na nguvu za kusujudia sanamu za Maria kulima mchicha ambao una soko kila kona, ujiongezee kipato:
 
Kwani kushika jembe nakwenda kulima unakuchukuliae aiseee.....hivi unamiliki hata heka moja wewe,sasa endelea kujifanya mfia dini utaishia kuhubili katika vituo vya mabasi.
we na mleta mada mna matatizo ya matumizi ya r na l, mnachanganya herufi sahihi, kwenye l mnaweka r na kwenye r mnaweka l. Sijui mmesoma shule za wapi?
 
Nawapongeza kwa hili la kuwaokoa wenzenu katika Ushirikina ila bado moja, bado mnamuomba Yesu Naiko wazi Yesu alikuwa akimuomba Mungu Katika Luka 22:42, Yesu anasali hivi: "Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; lakini si mapenzi yangu, bali mapenzi yako yatendeke." na Yohana 17:1-5,6-19,20-26 na Mathayo 26:39. Mkisema kwasababu yeye ni njia na uzima je Musa hakuwa njia kwa watu wake. #setfree
 
Hakuna binadamu dunia aliyewahi kuongea haya maneno hadharani na watu wanaomzunguka wakamwamini, isipokuwa Masihi
Yohana 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
.....
Musa na wenzake hawajawahi kufikia cheo cha Masihi:
......
Tafakari
"Mtu haji kwa baba"
Na sio mtu haendi kwa baba
 
Yesu alikuwa akimuomba nani, maana hapa mnawakosoa wanao muomba Malia nasi jambo baya ni katika kuelimishana, Je hili la kumuomba Yesu siyo ushirikina?.
 
Je wewe huombi Yesu
 
Bikra inatolewa na mashine tu and not otherwise,mtoto mchanga habikiri
 
Amna kitu hapa.
Tuliza akili vizuri alaf utuletee uzi mwingine
 
ni ulofa na ubabaifu wa kiroho na kiimani kubabaika na anachoamini mwingine 🐒
 
Ni hivi akuna aneabudu sanamu kwenye Ukatoliki- wewe sio Dini yako so usijisumbuwe nayo.Pia Bibilia unayo toa vifungu na kulalamika hapa ni Kitabu cha hao Wakatoliki.Aingii akilini mtunga Sheria akavyunja adharani Sheria alizotunga mwenyewe.Lete maandishi nje ya Bibilia kutetea hoja yako.Jambo ukristo utaendelea kuwapusa kichwa milele yote kwa sababu ....una majibu yote.
 
Maisha yanahitaji nidhamu na bidii ya kujituma kazini... Huwezi kuumba uchumi kwa sala.
 
Yesu alikuwa akimuomba nani, maana hapa mnawakosoa wanao muomba Malia nasi jambo baya ni katika kuelimishana, Je hili la kumuomba Yesu siyo ushirikina?.
Yesu ni Mungu.Kuna watu baada ya akili zao kushindwa ungamuzi wakaandika kuwa Yesu alikimbia na jamaa wakamsurubisha mtu mwingine🤣🤣.
Kaa fikiria hii....kwenye Quran Mungu wenu anasema sisi (sisi -sio mmoja manake ni zaidi ya mtu mmoja wakitoa kauli kama mtu mmoja) Al-Hijr
Kuna vitu nikivisema hapa ambavyo ata kwa jicho na sikio la kawaidia .ntaonekana nakufuru! Nakuombea kwa Yesu akufunulie Moyo wake na roho wake akakujalie kujua Ukweli ambao huo utakuweka huru
 

Attachments

  • Screenshot_2025-06-21-09-05-35-979_com.android.chrome-edit.jpg
    331.4 KB · Views: 20
Huna ulijualo kuhusu Bikira Maria
 
Kwani tatizo lipo wapi wewe ndo unaetaka kulazimisha vitu ambavyo hujaambiwa
 
Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47
Luka 1:46-49
[46]Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
[47]Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
[48]Kwa kuwa ameutazama
Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
[49]Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu.
NB! Haya hakuyaongea mwenyewe Bali alijazwa na roho MTAKATIFU nae akapata kunena hayo



Dada usiwe unatoa mistali michache yenye kubeba Nini unataka watu wasikie, ila toa mistali iliyokamilika ili watu nao wakajifunze nje ya maudhui yako,




Luka 1:42-43,46-49
[42]akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
[43]Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
[46]Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
[47]Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
[48]Kwa kuwa ameutazama
Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
[49]Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu.




Lakini hata hivyo hakuna aliyewahi muomba maria ,ila nyie ambao mnatembea na maudhui zenu ndio Huwa mnaradhimisha ionekane Huwa tunamuomba,,, utaratibu wa kuomba atuombee ni mpana sana ambao nyie msiojifunza hamuwezi elewa kwa siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…