subiri uone
JF-Expert Member
- Sep 12, 2024
- 753
- 624
Naomba unifafanulie haya maandiko umeyaelewa vipi =>Yesu ni Mungu.Kuna watu baada ya akili zao kushindwa ungamuzi wakaandika kuwa Yesu alikimbia na jamaa wakamsurubisha mtu mwingine🤣🤣.
Kaa fikiria hii....kwenye Quran Mungu wenu anasema sisi (sisi -sio mmoja manake ni zaidi ya mtu mmoja wakitoa kauli kama mtu mmoja) Al-Hijr
Kuna vitu nikivisema hapa ambavyo ata kwa jicho na sikio la kawaidia .ntaonekana nakufuru! Nakuombea kwa Yesu akufunulie Moyo wake na roho wake akakujalie kujua Ukweli ambao huo utakuweka huru
Mimi nakukubali sana kwa kutuelimisha, hiyo hoja ya matokeo sihalali kwasababu hata uchawi una matokeo/ushuhuda.Weka shuhuda hapa za maombi yaliyojibiwa
Zingatia njia ya unachokipata kwa mfano mwizi naye anapata hela Je huo wizi tuu halalishe kwasababu anapata pesa.Kama maombi yanajibiwa Kwa nini tusiendelee?
Akili yako ipo sawa?Weka shuhuda hapa za maombi yaliyojibiwa
Mariamu, Mary, Maria nk. Yote ni majina yake katika lugha tofautiKuna Kanisa moja maarufu kusali bila kumtaja Maria basi sala haijakamilika:
Yaani kila kusanyiko la sala ni lazima Maria atajwe:
Sasa huwa najiuliza huyo Maria ni nani ?
Maana Mama wa Yesu anaitwa Mariamu:
Sijawahi jibiwa hili swali
Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Na sala itajibiwa na yeye akiwemo! Kama yeye ni msabato ninamwelewa kwa sababu hata wakati wa Yesu wayahudi waliheshimu sabato kuliko mafundisho ya YesuWewe kama mpentekoste ni sawa wala hatuna haja unasali vip na kwanamna gani
Tutasali hivyo hivyo utake usitake Mkuu
Hii sala nilisali juzi nipo hosptali kwa matibabu. Tunaomuamini na kumuomba mama Maria tuendelee kumuamini na kumuomba.Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina
W.a.j.i.n.g.a nyinyi, Romana causa finita lucutaUtapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo:
Kibiblia, hakuna sehemu inayoonyesha kuwa Bikira Maria amepewa jukumu la kuwa mlinzi wa taifa lolote. Mungu pekee ndiye anayeweza kuwa Mlinzi wa taifa, iwapo taifa hilo linamwamini na kumkubali.
Zaburi 33:12
"Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu.”
Je, Bikira Maria ana uwezo wa kuwaombea watu huko aliko? Biblia haitufundishi popote kwamba wafu wanaweza kuwaombea walio hai. Badala yake, Biblia inaeleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea(Warumi 8:26). Ukisoma pia Ebr 7:25 imeandikwa kuwa Yesu anatuombea.
Naye[Yesu], kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Ingawa Maria aliheshimiwa na Mungu kwa kuchaguliwa kumzaa Yesu, hana mamlaka ya kuombea watu baada ya kifo chake.
Bikira Maria hakuwa Mkingiwa dhambi ya asili. Kuna watu wanafundisha kwamba Bikira Maria "alikingiwa" dhambi ya asili(the dogma of the Immaculate Conception); yaani kwamba alizaliwa bila dhambi ya asili.
Mafundisho hayo sio sahihi kwa sababu Maandiko yanasema:
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” — Warumi 3:23
Andiko hilo halibagui. Watu wote wanahitaji wokovu kwa njia ya Yesu, hata Maria mwenyewe alisema:
“Roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” — Luka 1:47
Bikira Maria alimtambua Mungu kuwa ndiye Mwokozi wake, hivyo naye pia alihitaji neema ya Mungu kama wengine.
Bikira Maria anastahili heshima kama mama aliyemzaa Bwana Yesu, lakini kama tulivyoona, hatupaswi kumwita mlinzi wa taifa. Kwahiyo ukifunga na kumsihi Bikira Maria akuombee, utapoteza muda wako bure. Afadhali ushike jembe ukalime!
Kama hukubaliani na hoja hizo, weka hapa Maandiko yanayokuambia kwamba "Bikira Maria ni Mlinzi wa Taifa lako, na kwamba yeye ni Mkingiwa dhambi ya asili."
Na kuhusu Maria kwamba anaweza kukuombea, usijitetee kwa kutaja lile tukio la arusi ya Kana ambapo Maria alimwambia Yesu "hawana divai" kisha Yesu akatenda muujiza divai njema ikapatikana. Hilo tukio lilifanyika Maria alipokuwa hai duniani. Sasa hivi Maria hayupo tena. Waliofariki hawasikii wala hawajui chochote kinachoendelea kwa walio hai duniani. Soma Mhubiri 9:6
"lakini wafu hawajui chochote...upendo wao, chuki yao na wivu wao vimetoweka tangu kitambo, kamwe hawatakuwa tena na sehemu katika lolote linalotendeka chini ya jua."
Na wewe unasemajeSisi wana wa dunia tukumbuke maneno aliyosema Bikira Maria, Alipowatokea watoto wa Fatima, Lucia, Franciska na Yasinta. Alisema tusali, Tusali Rozari, Tupate Amani. Na pia tuwaombee wakosefu na walegevu mwasiomuamini Yesu kristu 🎵🎶
Yesu amekufundisha umuombe mama yake, hivi huogopi kukataliwa na Yesu kwa kuacha mafundisho yake, mwenzenu anawapenda ndiyo maana anawakumbusha , hayo ni mafundisho ya Yesu au nani.Hii sala nilisali juzi nipo hosptali kwa matibabu. Tunaomuamini na kumuomba mama Maria tuendelee kumuamini na kumuomba.
Ndiyo, Ni mafundisho ya YesuNa wewe unasemaje
Yesu amekufundisha umuombe mama yake, hivi huogopi kukataliwa na Yesu kwa kuacha mafundisho yake, mwenzenu anawapenda ndiyo maana anawakumbusha , hayo ni mafundisho ya Yesu au nani.
Leta maandiko tujifunzeNdiyo, Ni mafundisho ya Yesu
.
Kwa Wa katoliki Majini ni Malaika waliolaniwa.Aiingii akilini kuwa yapo yanaoswaliNaomba unifafanulie haya maandiko umeyaelewa vipi =>
Yohana 14:1-6 - Yesu anasema, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu kuna makao mengi..."
Yohana 17:3 - Yesu anasema, "Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma."
Mathayo 6:9-13 - Katika sala ya Baba Yetu, Yesu anafundisha jinsi ya kuomba na kumwomba Mungu.
Kuhusu Mungu kusema sisi =>Hakika ni kuwa hakuna utata wowote katika hilo kwani ni tabia ya utumizi wa lugha nyingi ikiwemo Kiarabu, Kiingereza na hata Kiswahili. Wingi huu katika Lugha ya Kiarabu unaitwa Jam’u Litta’dhwiym (wingi wa utukufu na ukubwa). Wingi umegawanyika sehemu mbili – wingi kama wingi na wingi wa utukufu. Wingi unaotumika katika Qur-aan kwa Allaah Aliyetukuka ni huu wingi wa utukufu na ukubwa.
Katika lugha ya Kiingereza inaitwa The Majestic We. Mara nyingi wakubwa na watukufu kama Raisi, Mfalme, Malkia, Waziri mkuu anapoandika barua au anapohutubia watu husema sisi ilhali makusudio ni yeye peke yake. Sasa hawa sisi ni kina nani na ilhali ni yeye peke yake? Bila shaka ndiyo hayo hayo matumizi ya kutumia wingu wa utukufu. Kwa urefu na kujifunza zaidi=>Kwa Nini Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatumia Neno ‘Sisi’, Au ‘Tuta...’ Na Hali Yeye Hana Mshirika? | Alhidaaya.com kama unamengine naomba uyalete ili tupate kujifunza.
Sio kuziabudu tuNi hivi akuna aneabudu sanamu kwenye Ukatoliki- wewe sio Dini yako so usijisumbuwe nayo.Pia Bibilia unayo toa vifungu na kulalamika hapa ni Kitabu cha hao Wakatoliki.Aingii akilini mtunga Sheria akavyunja adharani Sheria alizotunga mwenyewe.Lete maandishi nje ya Bibilia kutetea hoja yako.Jambo ukristo utaendelea kuwapusa kichwa milele yote kwa sababu ....una majibu yote.
Lete andiko lako usilete yaliomo kwenye Bibilia kwani sio Kitabu chakoSio kuziabudu tu
Bali hata kuzisujudia sanamu na kuzitumikia imekatazwa:
Hivi unataka kuniambia sanamu za Maria hazisujudiwi na Wakatoriki ?
Sema tu ukweli brother:
Hakuna Kanisa ambalo halina sanamu la Maria ambalo waumini kama wote wanaliaujudia mala kwa mala:
Mfano wewe ni mkubwa unaweza kuliona kama sanamu tu:
Vipi kuhusu watoto wanaotazama wakubwa wakipiga magoti na kusujidia hizo sanamu ?
Mimi ni Mkatoriki pia ila sithubutu kuzisujudia hizo sanamu, wala kuelekeza maombi yangu kwa Maria:
Mwisho kama muumini unajuaje hiyo sanamu ni ya Maria ?
Je aliitengeneza unamjua ?
Au hujui kuwa Ibirisi anaweza kuishi ndani ya ndani ya sanamu na akasujudiwa na maelfu ya watu kwa kujua ?
Ndio maana ikaandikwa usisujudie sanamu wala kuzitumikia:
Ushaona vinyago vya mganga wa mchawi ?
Ni vinyago vyenye roho kamili ya Shetani ndani yake:
Utapoteza muda wako bure ukisali hivi: "Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili, Mlinzi wa Taifa letu. Utuombee." Sala hiyo haina mashiko kwa sababu zifuatazo: