'Afande' aliyeagiza binti wa Yombo abakwe pamoja na mtuhumiwa wa 5 wako wapi? Kwanini wanamlinda kiasi hiki?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu mpo salama? Jana (August 19) tulishuhudia mengi back to back, huku RPC akahamishwa nkule watuhumiwa wakafikishwa mahakamani, lakini kwaini watuhumiwa wanne?

Walikuwa 6 ikiwemo na yule aliyetambulishwa kama 'afande' pamoja na mtu wa 5, ambako kwenye video watano wote walionekana. Sasa huyu watano yuko wapi na afande yuko wapi? Vielelezo vyote mnavyo kwanini wawili wasifikishwe mbele ya sheria kuwajibika kwa udhalimu wao?

Soma Pia: Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Au ndio mnajipanga kutuletea watu wa mchongo kama yule jamaa aliyegongwa na mwendokasi? Uzuri ni kwamba wasamalia wema walishawasaidia kila kitu, mpaka kumtaja afande huyo, safari hii wananchi tunasimama kidete, lazima afande huyo awajibishwe kwa ukatili waliofanya.

Pia soma: Mrakibu Msaidizi wa Polisi Fatuma Kigondo afunguliwa shtaka la kutuma vijana kufanya ukatili kwa binti wa Yombo

Bila kuwajumuisha na wao Watanzania hatutaelewa, hili mkae mkijua.
 
Aliyeagiza yale yote yafanyike yuko wapi?, kwani sheria zetu ni za Watu fulani tu na wengine haziwagusi?, End Impunity, Afande akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hili tukio lilikuwa " A planned rape", haitoshi kuwakamata watekelezaji wa tukio huku mastermind akiachwa aendelee kudunda mtaani bila kuwajibishwa.

Kimsingi wale vijana huenda wana kosa dogo kumshinda "Afande" maana wao huenda walikuwa wanatii amri tu ya mkubwa wao.

Bila mastermind kukamatwa, itakuwa haina maana yeyote kuwafikishahao vijana mahalamani
 
Hivi huyo aliyewatuma ushahidi Gani utamtia hatiani?
Yaani awatume wabake na yeye asishitiki kubakwa af afungwe
Kwani walitumwa walikuwa watoto au wendawazimu watii amri za kuvunja sheria?
Me nadhani wahalifu wamekamatwa inatosha aliyewatuma hawezi kuthibitishwa kama ni kweli au la
 
"Master Planner Conspiracy."
 
Hivi huyo aliyewatuma ushahidi Gani utamtia hatiani?
Yaani awatume wabake na yeye asishitiki kubakwa af afungwe
Kwani walitumwa walikuwa watoto au wendawazimu watii amri za kuvunja sheria?
Me nadhani wahalifu wamekamatwa inatosha aliyewatuma hawezi kuthibitishwa kama ni kweli au la
Anapaswa kuunganishwa kwenye Kesi hiyo, ameshiriki kupanga njama za kutenda Uhalifu (Gang Raping).
 
Hivi huyo aliyewatuma ushahidi Gani utamtia hatiani?
Yaani awatume wabake na yeye asishitiki kubakwa af afungwe
Kwani walitumwa walikuwa watoto au wendawazimu watii amri za kuvunja sheria?
Me nadhani wahalifu wamekamatwa inatosha aliyewatuma hawezi kuthibitishwa kama ni kweli au la
Hili ndio swali ninalojiuliza hata mimi.
Kwa mfano ingekuwa ni kesi ya mauwaji halafu akawakabidhi silaha waende kuua hapo kweli angekamatwa lakini kwenye kesi ya kubaka kila mtu ana kikojoleo chake na anatakiwa kutumia akili jinsi ya kukitumia kikojoleo chake kwa usahihi na pahala sahihi.
 
Back
Top Bottom