Afande aliyetajwa kwenye kesi ya 'Binti wa Yombo', sio mwanamke

Afande aliyetajwa kwenye kesi ya 'Binti wa Yombo', sio mwanamke

Wakili Edwin Mugambila, Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Kitaifa wa Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu, amesema:

"Kwanini huyu Afande anayehusika kwanini hajashtakiwa? Tumefanya vikao sana na mwendesha mashtaka Dodoma yaani mpaka kesi inakamilika sisi tulipiga kambi Dodoma Mimi na mwenzangu wa Mkuki. Katika majadiliano ili mtuhumiwa yoyote apelekwe mahakamani sheria ilivyo sasa hivi ni lazima ufanyike uchunguzi na ushahidi wa kutosheleza kumpeleka mtuhumiwa mahakamani. Sasa connection ya huyu mama, huyu Afande anayetajwa ingetokea wakati gani?

Pia, Soma: 'Afande Fatma' afika Mahakamani, Hakimu aahirisha Kesi ya 'Binti wa Yombo' hadi Oktoba 7, 2024

"Wakati uchunguzi unaendelea wakati wanawahoji wale washtakiwa pamoja na binti mwenyewe hakuna yoyote kati ya wale aliyemwingiza yule Afande tunayemsikia yule Afande Fatma Kigondo. Hakuna aliyemuingiza kwenye ule mchezo.

"Binti alivyohojiwa alisema alikuwa akionyeshwa picha anasema aliambiwa aombe radhi kwa Afande lakini picha aliyokuwa akionyeshwa ni picha ya mwanaume aliyevaa magwanda ya kijeshi"- Wakili Edwin Mugambila

#PbCloudsFM | Oktoba 3
View attachment 3114568
Soma: Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela
Kwa hiyo afande polisi mwanaume ameolewa na mwanaume?
 
Inafikirisha inawezekana hii kauli ya wakili yupo sahihi maana huyo mwanajeshi ndio aliwatoa hao vijana kafara ingekua njagu angewatoa manjagu wenzie kafara pia pana vitu vimefunikwa hapo..
 
Bahari mbaya inabidi tusikilize hata wapumbavu, sasa kama hakuna ushahidi, ulitaka apelekwe Mahakamani kufanya nini?
Watanzania wengi hawajui nini maana ya ushahidi wa kimahakama,wao wanazani maneno matupu yanatosha kua ushahidi, wakati ushahidi ni zaidi ya maneno matupu!!
 
Inanichanganya, huku wanasema KESI HADI OKTOBA 7 na leo ni 4


Huku wamehukumiwa kifungo cha maisha


Wanahukumiwaje maisha kabla ya hiyo October 7?
Ni Kesi mbili tofauti, usichanganyikiwe
 
ukifikiria ni uongo kuna nama kuna ukweli ila bado wanatuficha labda uyo dada aliwachanganya washikaji hao wakaamua kwenda kumpiga mtungo
Hata mim nilishangaa inawezekanaje polis kumtuma mwanajeshi wa jwtz na askari wa magereza wakati ana watoto wajinga wengi tu karibu yake na wanaomtii zaidi
 
Picha ya huyo afande wa kiume ipo wapi?

Police Wanavyopenda kulindana wangeshaiachia kumsafisha ACP wao.
 
Spinning kama Spinning, na waTZ walivyo na vichwa kama kuku wana spin kwelikweli.
 
Binti alivyohojiwa alisema alikuwa akionyeshwa picha anasema aliambiwa aombe radhi kwa Afande lakini picha aliyokuwa akionyeshwa ni picha ya mwanaume aliyevaa magwanda ya kijeshi"- Wakili Edwin Mugambila😂😂😂
Kwamba huyo afwande ni ngangaripoa?🥺🙌🏿🙌🏿🏃🏿
Amelidharirisha jeshi huyu wakili anataka kusema nini kwamba mambo ya Pdidy yapo mpaka jeshini?
 
Hadi hapo inaonekana hakuna uchunguzi wowote uliofanyika.kwasababu ungefanyika uchunguzi hizo hoja zote zingepata majibu sahihi kwasababu watuhumiwa tayari wako korokoroni na aliyefanyiwa hicho kitendo wako naye.
 
Hii case inazidi kutuchanganyaa? Ile video kule mwisho wale washenzii walikua wanasema wamuombe msamaha Afande,

Kunae mwingine alidakia, "usirudie tena kutembea na waume za watu" sasa huyu afande wa kiume nae ana mume wake?

Kheeeeh mbna hayaa mapyaaaa, Woiiiiiiii!!!!
 
"Aroo Afande Chapombe inuka bwana usije ukapasuliwa yai ukatia aibu jeshi" Kali P
Inaonekana afande wamemstahi kuepuka kutia aibu jeshi
 
Back
Top Bottom