Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali, Said Mwema amefanya ziara ya siku mbili katika Visiwa vya Unguja na Pemba kufuatia ghasia za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura zinazoendelea katika visiwa hivyo.
Awali Mwema alikutaka na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha na kufanya nao mazungumzo kabla ya kuonana na watendaji wa jeshi hilo, wanasiasa, viongozi wa dini na viongozi wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Wakati akizungumza na Rais Amani na Waziri Kiongozi Nahodha aliwaahidi kwamba jeshi lake litafanya kazi kwa misingi ya haki na kufuata sheria zote za jeshi hilo na kuwataka viongozi kushirikiana na jeshi lake katika kuweka hali ya amani katika visiwa vya Zanzibar.
Alisema suala lililojitokeza ni malalamiko ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi hivyo aliwaomba viongozi hao kutatua kasoro zinazojitokeza katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepusha nchi kuingia katika machafuko kwani ikumbukwe kuleta uvunjifu wa amani ni rahisi lakini kuirejeshs hali katika mani ni kazi kubwa..
Katika ziara yake hiyo ya siku moja katika kila kisiwa Mwema alitaka kujua tatizo la uvunjifu wa amani litakabiliwa vipi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo hivi sasa alisema hali imeanza kuonesha kuwa na dalili mbaya kiusalama.
Alisema inaonesha amani inaanza kuharibika na aliwataka viongozi hao kuwa makini na kuvunjika kwa amani kwani kupotea kwa amani katika nchi ni kazi nyepesi lakini kuirejesha amani ni kazi kubwa na ina gharama kubwa katika nchi yoyote.
Ispekta Jenerali alisema vitendo vya uchomaji moto nyuma haviendaji na siasa, dini wala kabila na ni sawa vitendo vyengine vya kihalifu hivyo jeshi la polisi halitawavumilia watu wenye kuendesha vitendo vya iana hiyo kuwataka wananchi kuwafichua watu hao ili wachukuliwe hatua kali dhidi yao.
Alilitaka jeshi la polisi kutosita kuwachukulia hatua wananchi wenye kuendesha harakati za uvunjifu wa amani na kuwataka viongozi wa dini, siasa na wananchi kuzungumzia lugha moja ya amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo vitendo vya uvunjifu wa amani vimeanza kujitokeza.
Awali kabla ya kuja kisiwani Pemba, Inspekta Said Mwema alikutaka na viongozi mbali mbali kufanya kazi kwa pamoja ili kuduisha amani kwani hali inajionesha kuwa sio nzuri kutokana na dalili za uvunjifu wa amani kuaza kutokea.
SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.