Afande Mwema "Amchimbia Mkwala" Rais Karume

Afande Mwema "Amchimbia Mkwala" Rais Karume

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
3,181
Reaction score
144
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali, Said Mwema amefanya ziara ya siku mbili katika Visiwa vya Unguja na Pemba kufuatia ghasia za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura zinazoendelea katika visiwa hivyo.

Awali Mwema alikutaka na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha na kufanya nao mazungumzo kabla ya kuonana na watendaji wa jeshi hilo, wanasiasa, viongozi wa dini na viongozi wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Wakati akizungumza na Rais Amani na Waziri Kiongozi Nahodha aliwaahidi kwamba jeshi lake litafanya kazi kwa misingi ya haki na kufuata sheria zote za jeshi hilo na kuwataka viongozi kushirikiana na jeshi lake katika kuweka hali ya amani katika visiwa vya Zanzibar.

Alisema suala lililojitokeza ni malalamiko ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi hivyo aliwaomba viongozi hao kutatua kasoro zinazojitokeza katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepusha nchi kuingia katika machafuko kwani ikumbukwe kuleta uvunjifu wa amani ni rahisi lakini kuirejeshs hali katika mani ni kazi kubwa..

Katika ziara yake hiyo ya siku moja katika kila kisiwa Mwema alitaka kujua tatizo la uvunjifu wa amani litakabiliwa vipi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo hivi sasa alisema hali imeanza kuonesha kuwa na dalili mbaya kiusalama.

Alisema inaonesha amani inaanza kuharibika na aliwataka viongozi hao kuwa makini na kuvunjika kwa amani kwani kupotea kwa amani katika nchi ni kazi nyepesi lakini kuirejesha amani ni kazi kubwa na ina gharama kubwa katika nchi yoyote.

Ispekta Jenerali alisema vitendo vya uchomaji moto nyuma haviendaji na siasa, dini wala kabila na ni sawa vitendo vyengine vya kihalifu hivyo jeshi la polisi halitawavumilia watu wenye kuendesha vitendo vya iana hiyo kuwataka wananchi kuwafichua watu hao ili wachukuliwe hatua kali dhidi yao.

Alilitaka jeshi la polisi kutosita kuwachukulia hatua wananchi wenye kuendesha harakati za uvunjifu wa amani na kuwataka viongozi wa dini, siasa na wananchi kuzungumzia lugha moja ya amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo vitendo vya uvunjifu wa amani vimeanza kujitokeza.

Awali kabla ya kuja kisiwani Pemba, Inspekta Said Mwema alikutaka na viongozi mbali mbali kufanya kazi kwa pamoja ili kuduisha amani kwani hali inajionesha kuwa sio nzuri kutokana na dalili za uvunjifu wa amani kuaza kutokea.


SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
 
Mwema asingeishia hapo tu alitakiwa aseme na kumshika sikio kamishna wake zanzibar aache ukereketwa wake na afanye kazi bila ya upendeleo.
 
Pemba sasa hivi ni ubabe tu dhidi ya yeyote yule anaejitokeza kuikingia kifua CCM ,huyo wanamwita ni adui nambari moja na hawatamvumilia watamshughulikia na kufa nae.
 
Mwema asingeishia hapo tu alitakiwa aseme na kumshika sikio kamishna wake zanzibar aache ukereketwa wake na afanye kazi bila ya upendeleo.
Jee kama IGP Mwema,
angekuwa amekutana na Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad. Unahisi Mwema angelazimika kumuasa na kumtaka kitu gani afanye kiumbe huyo? Fair analysis please!!!
 
Makala hii haioneshi wapi IGP Mwema amechimba mkwara kwa Raisi Karume. Labda kama hio ziara yake imekuwa ni ya aina yake.
 
Mwema amekuwa mnafiki.
Njia sahihi ya kuhakikisha amani inaendelea kuwepo ni watu kupata haki zao. Penye haki pana amani na pasipo na haki tegemea uvunjifu wa amani kwani watu watadai haki zao kwa njia yoyote ile.
Ukimshughulikia aliyechoma nyumba, umeshughulikia matokeo ya tatizo; inabidi ujiulize kwanini kachoma nyumba? - ushughulike kuondoa hiyo sababu.
 
Junius je unaelewa maana ya kuchimba mkwara? Hii thread yako haina kitu kama hicho. Nionavyo mimi, Mwema ni mzugaji kama Ngunguri na anajaribu kuwatisha Wapemba na wana CUF ili CCM waone anafanya kazi. Haya mambo ya hati za ukaazi kule Zanzibar ni political nonsense. Mbona Mafia au Ukerewe watu hawaulizwi hati za ukaazi za wazalendo wakule wakati wa kujiandikisha kupiga kura? Pili mbona Wazanzibari walio Tanganyika hawaulizwi hati ya ukaazi wakati wa kujiandikisha kupiga kura? Naogopa huenda mambo ya 2001 yanaweza tokea tena 2010.
 
.......Alisema inaonesha amani inaanza kuharibika na aliwataka viongozi hao kuwa makini na kuvunjika kwa amani kwani kupotea kwa amani katika nchi ni kazi nyepesi lakini kuirejesha amani ni kazi kubwa na ina gharama kubwa katika nchi yoyote..

huu ndio mkwara?
 
Makala hii haioneshi wapi IGP Mwema amechimba mkwara kwa Raisi Karume. Labda kama hio ziara yake imekuwa ni ya aina yake.
Umesoma maneno tu na si maudhui ya habari, mkutano wa Mwema na Karume na wajinga wenzake haukuwa wa kawaida saaaaana maana Mwema alikuwa akiongea kama anaamrisha gwaride vile, natamani ungekuwapo.
Junius je unaelewa maana ya kuchimba mkwara? Hii thread yako haina kitu kama hicho. Nionavyo mimi, Mwema ni mzugaji kama Ngunguri na anajaribu kuwatisha Wapemba na wana CUF ili CCM waone anafanya kazi. Haya mambo ya hati za ukaazi kule Zanzibar ni political nonsense. Mbona Mafia au Ukerewe watu hawaulizwi hati za ukaazi za wazalendo wakule wakati wa kujiandikisha kupiga kura? Pili mbona Wazanzibari walio Tanganyika hawaulizwi hati ya ukaazi wakati wa kujiandikisha kupiga kura? Naogopa huenda mambo ya 2001 yanaweza tokea tena 2010.
Yale yale...umesoma maneno...siyo hati za ukaazi ni vitambulisho vya ukaazi na kama ukerewe hakuna, kuna wazanzibar wapo bara uropa na amerika kadhalika hawana vitambulisho hivyo bado tunawahesabu kuwa ni wazanzibari lakini si wakaazi kadhalika na baadhi ya hao unaosema wapo tanganyika kwa taarifa yako vitambulisho hivi vinatumika katika mambo mengi tu ya kitaifa zanzibar hili la kuvitumia katika mambo ya kura ni ujanja wa CCM zanzibar tu kuiba kura.
heading na habari lol hata mie sijauona huo mkwala
soma vizuri maudhui ya habari.
huu ndio mkwara?
kadhalika na ww mkuu.
 
Jee kama IGP Mwema,
angekuwa amekutana na Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad. Unahisi Mwema angelazimika kumuasa na kumtaka kitu gani afanye kiumbe huyo? Fair analysis please!!!
Pakacha Maalim wala hakusubiri Mwema afanye usanii wake tayari CUF walishawatwanga barua wahusika wote kutahadharisha hali ya uvunjifu wa amani zanzibar inayofanywa na CCM kwa kutumia usalama wa taifa na avikosi vya ulinzi, kisingizio kikiwa ni daftari la kupiga kura, Maalim kwa bahati nzuri tu ameelezea wazi wazi tokea mwanzo mzizi wa tatizo kutaka dosari zirekebishwe mapema kabla zoezi hili halijaanza ili wale woote ambao hawajapatiwa avitambulisho vya ukaazi na wanastahili kupatiwa kwanza wapatiwe, kama hayo yangefanyika kusengekuwa na zogo lolote na hata vikosi vya ulinzi visingelihitajika kutumika na pengine afande Mwema angebakia na stress za majambazi na Zombe tu.
 
Jamani kuuliza sio ujinga.
Wengine tupo nyuma sana na hizi habali za ZNZ. Kwahivyo napenda kuuliza yafuatayo:
kwani hizi ZNZ ID zilitoka lini na kwanini wengine wamepata na wengine hawakupata?
Kulikuwa kuna deadline ili kuzipata?
Watu walijulishwa mapema kuwa wakaazi tu wenye hizi IDs ndio watapiga kura?
Watu wakijua pia kama hawana hizi IDs basi wao sio wakaazi wa ZNZ bali ni wapita njia tu?
Anaejua atueleze kwa urefu bila ya party feelings, kwasababu bila ya kufahamika vibaya ndugu zetu Wapemba nao ni wakaiidi kidogo na wanapenda kushindana bure bure, inawezekana kuwa huko nyuma wamekataa kwa makusudi kuchukuwa hizi IDs.
Anyway, kama unajua nini kilitokea huko nyuma tafazali tuereze.
Naomba samahani na tena kama nimetukana!
 
Mwema hana ubavu kisheria kumpiga mkwara Rais wa Zanzibar. Hata KIKWETE mwenyewe hawezi.
 
Jamani kuuliza sio ujinga.
Zan ID haihusiani na nasaba wala eneo la mtu kuzaliwa. Inahusiana na Mkaazi halali wa Zanzibar kwa mujibu wa sheria ya U-zanzibari. Hivyo unaweza kuwa wewe ni Mpemba wa kujinasibu, ambaye wazazi wako wamezaliwa Chokocho, lakini ukawa hustahili kuwa na Zan ID kwa vile wewe ni mkaazi wa kudumu wa Buguruni
 
kwa kweli hali ya vitambulisho iko kisiasa zaidi na wote hao ni wahuni wanacheza mchezo wao kisiasa na kuangalia ni jinsi gani wataweza kushinda election ijayo

ila la kusikitisha wananchi wanaumia na kutseka kwa upumbavu wa watu wachache kuweka maslahi yao mbele

inaumiza sana maana hata wazanzibari wote wanaonekana wajinga kwa mslahi ya hao wapuuzi
 
Back
Top Bottom