Afande Sele: Daz Baba hatumii Madawa ya Kulevya, anakunywa pombe kupita kiasi

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Afande Sele amedai kuwa Daz Baba havuti unga kama watu wengi wanavyodhani bali amekuwa akinywa pombe bila kuzingatia kula hali inayomfanya akonde


Akiongea na Bongo5, Afande amesema huu ni wakati wa wasanii na wadau wa muziki nchini kuonyesha juhudi za kumuokoa katika hali hiyo ili kunusuru maisha yake.

“Tatizo sisi wabongo tunapenda kusema vitu vya unafiki hasa hasa sisi wasanii,” amesema Afande. “Tunashindwa kusema vitu vya ukweli mwisho wake tunaathirika zaidi. Mbona wasanii wengine wa nje wakifilisika wanasema wamefilisika ili waweze kuishi maisha ya kawaida?” amehoji Afande.

“Tatizo watu wanajikweza wakati hawana kitu. Kusema kweli hali halisi ya Daz Baba ni mtu ambaye kama kachanganikiwa hivi. Daz Baba havuti unga. Wasanii acheni kuongea huu ndio wakati wa kumsaidia. Daz Baba akinywa pombe hata bia mbili tu anabadilika kabisa na tatizo lake Daz akinywa pombe hawezi kula, kwahiyo mara nyingi anakesha anakunywa pombe, hachagui pombe. Kusema kweli Daz Baba ni mtu ambaye kachakaa.

Mimi naapa Daz havuti unga ila ni mlevi kupita kiasi. Hana muda wa kulala. Ukikutana naye sehemu unamwomba msamaha wewe kwa sababu bila hivyo atakusumbua na haelewi anachoongea, kama vile chizi tu. Wapo wadau ambao wanajua Daz katoka wapi. Mimi mwenyewe binafsi nimeshahangaika na Daz na kwa namna ya pekee lakini watu wengine hawafikirii kama hili jambo ni la serious.”

“Toka naanza kubadilika mimi najaribu kumweka sawa. Kwasababu kama hali ngumu hata sisi hali ngumu tunahangaika tu. Watu wengi wanasubiria mtu amekufa halafu waanze kutoa magari na michango. Kwanini kama mnaweza kufanya juhudi hizo msifanye sasa hivi? Kwenye mazishi watu wanajifanya kukodi magari kwenda kuzika, mtu kama Daz kipindi hiki ndio cha kumsaidia. Wapo marafiki wa Daz, wasanii wadau wanaweza kumsaidia sasa hivi.”
 
kama havuti bwimbwi basi anakunywa chang'aa....
 
Afande kuna wimbo alikushirikisha Daz Mwalimu,anzisha movement za kumsaidia.
 
Huu ni wakati, huu ni wakati..yani wanapenda haka kamsemo...
Alikua wapi wakati woote yamaa anabugia hizo pombe? Yani mpaka mwana JF a raise concern, ndo nao wakumbuke kwa Dazbaba yuko vibaya...? Yani ngojeni story za michango kudadadadekiii...
 
Kwa afya hii au ameshaunganishwa kwenye grid ya taifa? Jamaa hali yake mbaya.
 
Aache uongo uyo jamaa anakula unga yaani ilo alina ubishi
 
Honestly...hali ni mbaya na wasanii kashfa za dawa zinawamaliza kabsa....haiitaji darubin kubaini hilo....umoja wa wasanii tatueni hili....msiwakubalie wafanyabiashara na wanasiasa kuwatumia kama punda wa mizigo na kuwa dump
 
Daz baba " cvuti unga wala sinywi pombe na soon naachia nyimbo zangu 2 na video "

Aliyasema aya alipoojiwa na Choka Dj
 
Jamani mie nadhani kuna umuhimu wa pombe yoyote kwenye chupa yake kuwa na maandishi haya "Drinking alcohol is dangerous to your health", kama ilivyo kwenye sigara. Hii itatuepushia na lawama za kutowapa msaada walevi walioathirika na ulevi wao. Haingii akilini mtu anywe mipombe kwa starehe zake, ukijaribu kumshauri anakujibu "maisha yangu hayakuhusu", akianza kuathirika sie ndio tumpe msaada. Aise, mie sitoi hata senti, ni bora nikamlipie ada mwanafunzi aliyefukuzwa shule kwa sababu ya kukosa ada.
 
Maneno ya afande sele yamenitia uchungu simanzi sana

Watu wanaishi maisha ya kuigiza wakati hawana kitu
 
Wabongo tulivyo wanafiki tunasubiri afe tukachukue pointi3!!
 
Ni wakati muafaka pia wa kunyoa hizo rasta, nazo nasikia huwa zinakula sana mwili.
 
Duh ingekua enzi za operesheni Kimbunga hakika swahiba angejikuta anarudishwa Somali kimakosa maana mule mule kama mtabe wa kwenye muvi ya Captain Philips.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…