Afande Sele: Mama Kanumba hana sifa ya kuwa mzazi,anafurahia Lulu kufungwa kwa ajili ya ubazazi wa mtoto wake

At 27 Mungu alimpa pesa na umaarufu lkn jamaa alishindwa kutulia na kuanzisha familia, warembo wote waliokuwepo town ameshindwa kuchagua mmoja akaoa akatulia badala yake akaona ahangaike na kitoto cha watu cha mama Eliza. Japo marehemu hasemwi kwa mabaya lkn acha tuseme iwe fundisho kwa wengine wote waliojaaliwa na Mungu lkn wakazichezea neema zake.
 
Then nahisi ataweza kushinda rufaa akarudi mtaani.
Lulu alijichanganya kidogo kwenye kutoa utetezi wake, ila swali la kujiuliza ni nani mwenye ushahidi kuwa kanumba alisukumwa? Na kama alisukumwa alianguka kutoka umbali gani hadi kufika chini sakafuni?

Mwili wake ulifanyiwa autopsy? Je alikuwa na kiwango gani cha kilevi wakati amefariki? Je alikuwa intoxicated? Alikuwa na majeraha yoyote? Ya ndani au nje ya mwili?

Hapo kuna utata mkubwa sana, ushahidi wa kimazingira pekee hautoshi. Ripoti kamili ya daktari inasemaje kuhusu kisababishi cha kifo chake?
 
Ila ata mi huyu mama alinishangaza alipofurahi live........km mzazi angekaa kwa kutulia,akashukuru kimoyomoyo haki imetendeka ama alilolitaka limetimia.akampumzisha mwanae kwa ibada zilizoenda skul
 
BAADHI YA WAZAZI WA WASANII WA BONGO MOVIE NAO MAISHA YAO NI YA KISANII TU! WANAISHI KIMOVIE MOVIE TU!
 
Uchache wa elimu ukichanganyika na wingi wa maneno ni hatari kuliko nyuklia.
 
Umeongea kama mzazi wa mtoto wa kike Je afande una mtoto wa kiume??
 
Wamuache huyu mama wa watu jamani mtoto wake ndio alikuwa tegemeo lake
 
Umeongea point sana pia mimi nilikua najiuliza kwanini hawakufanya autopsy mana wangejua chanzo cha mauti na kama alisukumwa au pombe au alindondoka ingejulikana wasingesumbuka na ushahid wa kujieleza ingekua nchi za wenzetu wasingetaka tabu...
 
Ukiwa na mtoto wa kike lazima uwaze hivi

Afande sele mlee mwanao vizuri

wazazi wote hapo wana makosa usilalie upande mmoja
 
Umeongea point sana pia mimi nilikua najiuliza kwanini hawakufanya autopsy mana wangejua chanzo cha mauti na kama alisukumwa au pombe au alindondoka ingejulikana wasingesumbuka na ushahid wa kujieleza ingekua nchi za wenzetu wasingetaka tabu...
Jambo la kushangaza sana, yani hakuna mwenye ripoti kamili ya kitabibu juu ya kifo chake. Tunabaki kusema tu alikuwa na lulu na kulikuwa na chupa ya pombe ndani! Seriously hiyo inatosha kumfunga mtu?
 
Nakumbuka vizuri saana mwaka 2006 yaani miaka miwili tu baada ya mimi kushinda taji la ufalme wa rhymes Tz na kukabidhiwa ile gari maridadi sana ya zawadi aina ya toyota sera yenye milango ya kubinuka kama mabawa ya ndege anaejiandaa kuruka....Jumamosi moja ktk mwaka ule nikiwa kwenye ubora wangu wa hali ya juu na ushawishi mkuu kuliko msanii yeyote Tz nilialikwa kutumbuiza Tabata kwenye ukumbi wa Dar West uliokua maarufu sana nyakati zile...Lkn wakati nikiwa back stage kabla sijapanda jukwaani huku usiku ukiwa umetamalaki yaani ule usiku wa manani au usiku wa manane kama wengi tulivyozoea kusema ingawa tunakosea nikashangaa nashikwa begani na mtu aliyekua nyuma yangu ambapo kulikua na watu wengi tu ...nilipogeuka niangalie ninani aliyenishika bega''Hammad"nikamuona Lulu michael aliyekua bado ni bint mdogo sana ingawa tayari alikua na umaarufu si haba labda kwa sababu ya hayo maigizo yao ambayo baadae wakayaita filamu au bongo movie...nilipomuona akaniamkia kwa bashasha namimi nikaitikia huku sura yangu nikiikunja na kuwa ya kuogofya kisha nikaamuuliza kwa ukali kidogo ni kwanini yupo pale ukumbini ktk muda ule ambao kwa umri wake hakupaswa kuwepo?..lulu hakua na majibu ya maana na papo hapo nikamtoa nje ya ukumbi na kisha nikamtuma dereva wangu wkt ule alikua home boy wangu ephraim nguzo aka bad card amrudishe nyumbani kwao haraka na ahakikishe mama yake amempokea...Bad alifanya hivyo kiroho safi akarejea ukumbini na akanimbia kuwa alitimiza yote niliyomuagiza ukizingatia na yeye badi tayari alikua na familia hivyo aliujua vyema uchungu wa mwana...lkn miezi michache baadae nikaja kupigwa butwaa baada ya kusikia kuwa et kale kabint lulu kumbe tayari kalikua na ukaribu usio wa kawaida na baadhi ya hao wasanii mabazazi wa maigizo wasiokua na utu wala aibu ...niliumia sana moyoni nikiwa kama mzazi wa mtoto wa kike ninaempenda sana na kutamani kumuona akitimiza ndoto zake muhimu kwenye maisha kama kupata elimu kwa wkt muafaka...lkn niliumia zaid baada ya matatizo aliyoyapata lulu kupitia kanumba na kwa hakika sikua miongoni mwa waliohuzunika wala kushiriki kivyovyote ule msiba wa kanumba ingawa wkt wote wa pilika za msiba ule mimi nilikua dar tena palepale sinza msiba ulipokuwepo...sikutaka kuvaa joho la unafki kama ilivyo kwa waTz wengi...kwangu hata sasa kanumba ni mtu mbaya na alifanya kitendo kibaya kabisa dhidi ya bint mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio.kumtumia kwa sababu ya umaarufu wake...leo kanumba amepumzika au anapambana na Mola wake kwa kutofuata yale maandiko yasemayo kuwa'TAMAA Ikichukua Mimba Huzaa Dhambi na Dhambi Ikishakukomaa Huzaa MAUTI...Kanumba amevuna alichopanda lkn Lulu unyonge wa kiumri na udhaifu wa kisichana vimebakia kuwa mateso ktk maisha yake...MUNGU ni mwema atamuafu Lulu amalize kifungo chake salama kama alivyompa kanumba haki ya matendo yake mabaya kwa kumlaza mapema...Mwisho wa siku wote wawili wabarikiwe kwa kutufundisha tuliobakia ili tuchague njia sahihi za kupita....DUNIA..GUNIA...
 
UKIMUANGALIA LULU UTAGUNDUA SHE IS A VERY YOUNG GIRL COMPARED TO KANUMBA..........

SITUATION KAMA HII ILITAKIWA MAMA KANUMBA AIFUTE KESI TUU ILI ISSUE YA LULU IMALIZIKE KIFAMILIA NA ASEMEHE KUTOKA MOYONI ANGEKUJA KUISHI KWA AMANI.

KUFURAHIA LULU KUFUGWA SIO ISSUE ILA ISSUE JE NI KWELI MAMA KANUMBA ATAWEZA KUISHI KWA AMANII BAADA YA LULU KUFUGWA GEREZANI.

IKUMBUKWE YA KWAMBA MIAKA 2 SIO MINGI SANA LULU ATATOKA GEREZANI.

JE BAADA YA LULU KUMALIZA KIFUNGO CHAKE NA KUTOKA GEREZANI MAMA KANUMBA ATAKUWA KATIKA HALI GANI ?

NA IKUMBUKWE YA KWAMBA LULU NI STAR NA AKITOKA MAISHA YAKE YATAENDELEA KUWA MAZULI TUUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…