Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Msanii Afande Sele ametoka hadharani na kumtaka Rais wa amhuri ya Muugano wa Tanzania kutumia busara, imani yake na malezi kuona ni kwa namna gani atalifariji taifa kwa kile kilichotokea katika kipidni cha uchaguzi.
===
Mwanamuziki na mfalme wa mashairi Tanzania, Selemani Msindi, maarufu kama Afande Sele, ametoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutumia busara na hekima katika kuunganisha taifa na kuponya majeraha yaliyosababishwa na matukio yaliyotokea kipindi cha uchaguzi mkuu.
Akizungumza na Jambo TV, Novemba 5, 2025 mkoani Morogoro, Afande Sele amesema taifa linahitaji mshikamano na upendo ili kurejesha hali ya amani na matumaini miongoni mwa wananchi waliojikuta katika majonzi tangu Oktoba 29, 2025.
Msanii huyo mwenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa Hip Hop nchini ameongeza kuwa wasanii na vijana wanapaswa pia kushiriki katika juhudi za kudumisha umoja na amani, akisema ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha taifa linaendelea kusimama pamoja licha ya changamoto zilizojitokeza.
Source Jambo TV
Soma pia