AFANDE SELE NI RASTA,MWANAHIP HOP AU MPAGANI?

AFANDE SELE NI RASTA,MWANAHIP HOP AU MPAGANI?

N'gwanantugwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
347
Reaction score
345
AFANDE SELE NI RASTA,MWANAHIP HOP AU MPAGANI !!!!?

*kila mstari wake aliotaja Mungu weka Jua.

Imani ni kuwa nayohakika kwa mambo yanayoonekana nayasiyooneka.Kila utamaduni una imani yake.Hakuna utamaduni usiokuwa na Imani.Napata shaka sana na utamaduni anaoishi nao kaka mkubwa Suleiman Msindi a.k.a Afande sele ambae ni Msanii Mkongwe katika muziki wakufoka foka na mwanasiasa wa chama cha A.C.T.Nasema hivi kwa sababu Afande mara nyingi anapokuwa anahojiwa na vyombo vya habari anaongea vitu visivyoeleweka kabisa juu ya aishivyo yeye,utamaduni wake na Imani yake.

Nyimbo nyingi za Afande Sele amekuwa akighani(akichana) na anatumia midundo ya hip hop hivyo moja kwa moja Afande Sele ni Mchanaji. Mashairi yake yamebeba ujumbe unaogusa jamii moja kwa moja.
kwenye vyombo vya habari mara nyingi amekuwa akikana yeye si mwanaitikadi wa [HASHTAG]#hiphop[/HASHTAG] .Yeye ni rastafarian.Lakini inapotokea kategori ya hip hop jamaa huwa anashiriki fresh tu.Ila kipindi kile cha sakata la Sugu la maralia alisema yeye hana itikad za kihip hop.

Hii ilinipa ufikirish nijue hii imekaaje?

Afande ni msanii wa hip hop mwenye imani ya Rastafarian.

Je,kunatofauti gani kati ya rastariani na mwana hip hop katika Imani yao juu ya uwepo waMungu?

Ilinichukua muda mfupi kupata jibu.
Nilipojifunza Iman ya rastafarian Mungu wao ni Jah.Mungu wao haonekani.Niyule aliyeumba Mbingu na ardhi.Nihuyu aliyempa Maarifa Mfalme Suleiman wa Israel akazaa na Malkia Sheba wa khush ambae kizazi chake kilimleta mfalme Tafal Makonen wa Ethiopia
Na hip hop inaamini Mungu haonekani.Wanahip hop wengi wanasisitiza watu wasome vitabu vitakatifu kama msahafu au biblia,vitabu vinavyosisitiza kuwa Mungu haonekani.
nikagundua katika Imani,Itikadi hadi Misingi Hip hop na rastafarian nitamaduni zinazofanana sana.

Nilizidi kupigwa na butwaa pale nilipomuona na kumsikia Afande Sele akihojiwa na Ayo tv kuwa Mungu anaemuamini yeye ni Jua.Jua ndio limeunda arhi na mbingu.Kila kitu kinatokana na jua.Kwake anaposema Mungu au kutaja Mungu hata kwenye mistari yake anamaanisha jua.
Jamaa huwa anasema anasoma sana biblia lakini biblia inasema Hata jua liliumbwa Na Mungu.Sasa sijui Afande hiyo biblia anaisoma akiwa katika hali gani anashindwa kuelewa Mungu ni nan?
Nayasema haya kwasababu Afande anapotosha ukweli.Anashindwa kuishi kwenye misingi ya Hip hop au Rastafarian.Amebaki kuwa mpotoshaji kwenye uma.Afande ni msanii mkubwa.Kama ameamua kua muabudu jua aseme tu.Asiwe anataja anaishi katika utamaduni asioweza kuishi ktk misingi ya tamaduni hizo.Anaaibisha tamaduni za watu.

Siku zote wanaoabudu jua ni wapagani ambao wanaishi kwa kutoa sadaka ya damu ya binadam kwa huyo Mungu wao.

AFANDE NI RAPER ANAEAMINI JUA.
NAWAAMINI JUA NIWAFUASI WA SHETANI.
ASIIMBE KWA KUTAJA JINA LAMUNGU AWE ANATAJA JUA TUJUE MUNGU AMTAJAE NI JUA

[emoji767]mdaijasho
[HASHTAG]#platemaarifa[/HASHTAG] na mali
 

Attachments

  • 1473939912859.jpg
    1473939912859.jpg
    43.2 KB · Views: 59
Back
Top Bottom