Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mwanamuziki mkongwe wa bongo wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele amemuomba spika wa Bunge, Tulia Ackson awaombe hospitali ya Mirembe iliyopo mjini Dodoma wapeleke usafiri bungeni na kuchukua watu wao akidai waliopo Mirembe ni wazima ila wana msongo wa mawazo wa maisha magumu uliosababishwa na watu waliopo Bungeni.
Afande kasema kichaa wa kwanza ni waliopo bungeni akitolea mfano jinsi viongozi wa Serikali wanavyoacha gari linaunguruma ilhali wenyewe wapo kwenye vikao bila kujali kiasi cha mafuta kinachotumika na kuharibika mapema.
Amesema wahusika wameajiriwa na Serikali, wanalipwa na wengine wamesomeshwa na Serikali hiyohiyo. Afande amesema Serikali sio jitu kubwa linalogawa mahela bila sababu bali ni watu wanaohangaika na kuteseka kupitia kodi zao.
Seleman Msindi amesema unaweza kujiona uko 'Smart' kumbe kipa kashaacha goli kitambo