DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Ni kuhusu Jimbo la Kigoma mjini.
Ukweli wa ukweli ni kwamba, Zitto analihitaji zaidi Jimbo la Kigoma mjini kuliko wakati wowote ule wa maisha yake ya kisiasa, lakini Jimbo la Kigoma mjini, linamuhitaji zaidi Baba Levo kwa maslahi ya watu wote wa mkoa wa Kigoma na sio Kigoma mjini pekee kuliko wakati wowote ule.
Baba Levo ana nafasi ya ubunge ndio malengo yake makubwa zaid ya kisiasa ingawa bado kwa neema za Mungu wake anaweza kupata nafasi kubwa zaidi kwenye safari yake kisiasa siku zijazo, lakini kwasababu mpaka sasa yeye mwenyewe hana matamanio mengine ya kisiasa nje ya ubunge, maana yake Baba Levo wakati wote wa ubunge wake atakua anajua ana deni kubwa kwa ndugu zake wa Kigoma na atakua anaogopa asipotimiza watamuadhibu kama walivyowaadhibu watangulizi wake ambao hawakutimiza ahadi zao baada ya kuchaguliwa akiwemo Zitto mwenyewe.
Ziito anataka ubunge kama mtu anaetaka kuoa mke wa pili wa kumburudisha, lakini Baba Levo yeye anataka ubunge, kama mtu anaetaka kuoa mke wa kwanza wa maisha.
Kwa Baba Levo ubunge ndio kila kitu,lakini kwa Zito ubunge ni kitu cha ziada.
Kwa bahati njema, mimi binafsi nafahamu Kigoma mjini na pia nawafahamu Zitto na Baba Levo, kwasababu wote tulikua miongoni mwa waasisi wa ACT-Wazalendo ambapo kupitia ACT, Zitto alipata ubunge wa Kigoma mjini na Baba Levo alipata udiwani wa kata ya Mwanga iliyopo Jimbo la Kigoma mjini.
Na katika miaka mitano ya ubunge wa Zitto aliendelea kuwa ni mwanasiasa asiyeeleweka kama ni mpinzani au ni chama tawala kutokana na kutojitoa kuwapigania wapiga kura wake, lakini Baba Levo katika miaka mitano ya udiwani wake, alionyesha msimamo wake kiasi cha hadi kwenda jela kwasababu ya kuwapigania wapiga kura wake.