Afanye nini apate haki zake?

Afanye nini apate haki zake?

kotapini

Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
92
Reaction score
158
Nina ndugu yangu alipata kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja na kampuni x, mkataba ukaisha, lakini hakuwahi kupewa namba ya uanachama ya mfuko wa jamii pamoja na kuwa akikatwa mchango kila mwezi.

Hawakupewa notice wala cheti cha kumaliza mkataba na hata alipoenda NSSF wakamwambia lete barua ya kusitisha mkataba na hakuwa nayo, wakati anafuatilia wakahamishiwa kwa muajiri mwingine ingawa stahiki zote zilikuwa zinatoka kampuni x iliyomuajiri mwanzoni, lakini pia mkataba umeisha na hakuna michango iliyowasilishwa wala notice ya kumaliza mkataba wala barua ya kusitisha mkataba.

Je, afanye nini kupata haki zake? Anaweza kuishtaki kampuni x na ile nyingine kivuli iliyompa mkataba wa pili?

Msaada tafadhari
 
Kama mikataba ya kazi anayo na alikuwa anakatwa makato ya NSSF anaweza kuwashtaki ndio. Awe na salary slips zake tu.

Kuwashtaki sio ishu, ishu ni je atapewa hayo mafao hata kama yangekuwa yanapelekwa?
 
Nina ndugu yangu alipata kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja na kampuni x, mkataba ukaisha, lakini hakuwahi kupewa namba ya uanachama ya mfuko wa jamii pamoja na kuwa akikatwa mchango kila mwezi.

Hawakupewa notice wala cheti cha kumaliza mkataba na hata alipoenda NSSF wakamwambia lete barua ya kusitisha mkataba na hakuwa nayo, wakati anafuatilia wakahamishiwa kwa muajiri mwingine ingawa stahiki zote zilikuwa zinatoka kampuni x iliyomuajiri mwanzoni, lakini pia mkataba umeisha na hakuna michango iliyowasilishwa wala notice ya kumaliza mkataba wala barua ya kusitisha mkataba.

Je, afanye nini kupata haki zake? Anaweza kuishtaki kampuni x na ile nyingine kivuli iliyompa mkataba wa pili?

Msaada tafadhari
Bilasha unataka kujua utaratibu na uwezekano wakupata haki yako ya mfuko wa hifadhi.

Swala la mfuko wa hifadhi kwa mwajiriwa ni swala lililopo kisheria. Hivyo sio fadhira ni hakiyako kupata mafao. Iwe yaliwasilishwa ama laa

utaratibu kama nikampuni binafsi.

Unapeleka malalamiko yako (CMA) Tume ya upatanishi na usuluhishi wa migogoro mahali pakazi.

ndani ya siku 30 ikiwa niswala linalo husu kufutwa kazi. Na ndani ya cku sitini tangu tukio lilipo tokea nje ya tukio la kufutwa kazi.

unajaza CMA form no 1.

ikiwa upo njee ya muda. Unaomba ruhusa ya kufungua malalamiko nje ya muda kwa form no CMA Form no 2.

ambatanisha mkataba wako wa ajira na nyaraka za malipo.

ikiwa unahitaji mwongozo zaidi njoo inbox
 
Back
Top Bottom