Afariki katika ugomvi wa kugombea simu ya marehemu

Afariki katika ugomvi wa kugombea simu ya marehemu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mtatiro Kitinkwi.jpg
Mtu mmoja alieyefahamika kwa jina la Mwidini SaidI (30) Mkazi wa Kitongoji cha Kitumbini, Kata ya Kivinje Wilayani Kilwa Mkoani Lindi amefariki mara baada ya kupigwa na kitu kizito Kichwani walipokuwa wanagombea simu ya marehemu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi amesema tukio hilo limetokea Juni 27, 2022 majira ya saa nne asubuhi ambapo marehemu alipigwa na watu wawili na mtuhumiwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Ally Kilingo (29) anashikiliwa na jeshi hilo huku mtuhumiwa wa pili akiendelea kutafutwa.

Kitinkwi ameeleza kuwa ripoti ya hospitali imeonesha damu ilivuja kwa ndani ya fuvu la kichwa kisha kuchanganyika na ubongo.

Source: Mashujaa FM
 
Ninawaambia vijana kuwa pigeni dili za maana umaskini uwaondoke. Sasa ona simu tu tena yawezekana ni ya 20000-50000 imetoa uhai
 
Km kawa asee
Mohamed na mwamedi
Muhidin na mwidini
Muharrami na mwalami
Hawa wa "mw" ni wale choka mbaya always.
 
Jamani apumzike kwa amani mwendazake kafa kizembe sana sasa simu ya marehemu ya nini jamani? ona sasa
 
[emoji16][emoji16][emoji16].unagombea Simu ya marehemu na haujui marehemu kaipata vipi hyo simu
 
Back
Top Bottom