Afariki kisa kupunguza tumbo

Afariki kisa kupunguza tumbo

carnage21

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
591
Reaction score
1,382
Habarini

Mojawapo ya tatizo linalosumbua wadada hasa wa mjini ni matumbo makubwa,kuna muuguzi amefariki tu kisa kujaribu kupunguza tumbo.Kwahiyo wale wadada wenye viribatumbo please nawashauri mpende uumbaji wa Mungu.

Hata sisi wanaume tuwapende bas hawa wenzetu,wataolewa na nani jaman tukiwatenga

Source:
Millard ayo
The New York post

======
Jarida la The New York Post, limeripoti kuwa Muuguzi mmoja kutokea Nchini Mexico amefariki baada ya kukutwa akiwa amepoteza fahamu katika Ofisi ya Daktari baada ya kujaribu kujifanyia upasuaji wa kupunguza tumbo.

Daktari Rolando Samper Mendoza, ambaye ni Mmiliki wa Hospitali hiyo iitwayo ‘Clinica Amper’ ya Mexico amesema Mwanamke huyo alijichoma sindano ya ganzi ili kujifanyia upasuaji huo ambao hana nao ujuzi wala uzoefu wowote.

Muuguzi huyo alifariki kwa kupata mshtuko wa moyo muda mfupi baada ya kukutwa na Mfanyakazi mwenzake ambaye aliwapa taarifa Wahudumu wa afya na kujaribu kumsaidia.

Mwanamke huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Carina, alijaribu kutekeleza upasuaji huo ili kupunguza tumbo lake Hospitalini hapo, kitendo ambacho kilisababisha Muuguzi huyo kujichoma kiasi kikubwa cha ganzi ambayo ilimsababishia madhara.

images

Andaa mil 65 [emoji23][emoji23][emoji23]
Yanini wakati nasikia huko bongo puto mil 3 tuu...

Halafu tumbo ni kujidhibiti na ulaji, mazoezi baas...

Tengeneza juice ya Ginger, Cucumber, lemon na pineapple blend kunywa kila asubuhi ujionee.
 
Yanini wakati nasikia huko bongo puto mil 3 tuu...

Halafu tumbo ni kujidhibiti na ulaji, mazoezi baas...

Tengeneza juice ya Ginger, Cucumber, lemon na pineapple blend kunywa kila asubuhi ujionee.

Sasa mtu kama mm asbh n saa nane mchana hiyo dawa itafanya kaz sangap
 
Yanini wakati nasikia huko bongo puto mil 3 tuu...

Halafu tumbo ni kujidhibiti na ulaji, mazoezi baas...

Tengeneza juice ya Ginger, Cucumber, lemon na pineapple blend kunywa kila asubuhi ujionee.
Kakidanganya nan [emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom