Nyundo_tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
</SPAN>
Cha Sa-soon muda mfupi baada ya kufaulu mtihani wa kuandika wa udereva
Sunday, November 08, 2009 2:05 AM
Mwanamke mmoja wa nchini Korea Kusini ambaye alikuwa akifeli mtihani wa udereva wa kuandika kila alipokuwa akiingia kufanya mtihani huo, amefanikiwa kufaulu mtihani huo baada ya kufeli mara 949.
Cha Sa-soon mwenye umri wa miaka 68, alianza majaribio yake ya kufaulu mtihani wa udereva mwezi aprili mwaka 2005 lakini alikuwa akifeli mtihani huo kila alipojaribu bahati yake.
Cha alikuwa akifeli mtihani wa mwanzo wa udereva wa kuandika akipata maksi 30-50 wakati maksi zinazohitajika ni 60-100.
Baada ya kufanya mtihani huo karibia kila siku kuanzia mwaka 2005, Cha amefanikiwa kufaulu mtihani huo kwa kupata maksi 60 katika mara yake ya 950 ya kuingia kwenye mtihani huo.
Hivi sasa Cha ana kazi ngumu ya kufaulu mtihani wa vitendo wa udereva ili aweze kupata leseni ya udereva.
Cha anafanya biashara ya kuuza chakula na vifaa vya majumbani akiuza bidhaa zake kwa kuzipitisha mlango kwa mlango kwenye maendeo ya watu wenye fedha. Kutokana na sababu hiyo Cha alisema anahitaji gari kwaajili ya biashara zake.
"Ni kitendo cha kuvunja rekodi ya dunia " alisema Choi Yong-Cheol polisi anayesimamia mitihani ya udereva katika mji wa Deokjingu.
Polisi wanakadiria Cha ameishatumia zaidi ya dola 4,000 katika jitihada zake za kufaulu mtihani huo.
Source: AFP