AFCON: Mambo yamebadilika?

Wachezaji wa timu za ulaya hawajitumi kuepuka majeruhi. Pesa wanazolipwa ni ndogo ukilinganisha na wanazolipwa ulaya. Afrika habari za uzalendo ni illusion tu kuanzia kwa viongozi, raia mpaka diasporas
 
Sasa unalinganisha ufaransa na afrika. Uko mifumo ya nchi ipo organized hauwezi kulinganisha hali ya ufaransa na huku. Uko hata raia wanaona kodi yao inatumika vozuri wanaona wanathaminiwa ni rahisi kujitolea hapa juzi juzi tu madogo wamerudi na milioni 180 wameishia kupewa 20k kila mmoja halafu next tournament unawaambia wawe wazalendo kweli.!
 
Siyo Ulaya tu hata Afrika
George Wea wakati anacheza alikuwa anajitolea kulipia tiketi ili isafiri, hivi Sadio Mane atahitaji alipwe kiasi gani timu ya taifa?
 
Mkubwa alietegemewa na akapenya mpaka sasa ni senegal pekee, wengine wote wamekaliwa kooni.

Na vile ni mechi 3 tu aisee tutashuuudia vigogo wengi wakiyaaga mashindano.
 
Kila kitu kizuri kilikua zamani! hapa ndio hua nachoka
Hahahaha halafu ukitaka evidence hakuna πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ukitazama mpira wao kwenye marudio ulikuwa wa ovyo tu πŸ˜‚πŸ˜‚ ila kutana na wazee wanavyousifia sasa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Siyo Ulaya tu hata Afrika
George Wea wakati anacheza alikuwa anajitolea kulipia tiketi ili isafiri, hivi Sadio Mane atahitaji alipwe kiasi gani timu ya taifa?
Ishu sio kutoa pesa ishu ni jitihada zao uwanjani. Pesa mtu anaweza kutoa tu kwa lengo la kujilinda na kupata watetezi pale ambapo jitihada zao uwanjani zitatiliwa mashaka. Hivi jitihada za mbappe ufaransa unaweza kulinganisha na jitihada za mo salah egypt. Mpira anaoupiga anguisa akiwa napoli unaweza kulinganisha na akiwa cameroon? Miaka michache iliyopita walikua na tabia ya kujifanya majeruhi ukifika muda wa afcon baada ya kushtukiwa sasa hivi wanakuja tu kucheza kuepuka lawama uko kwenye ligi wanazocheza hawayataki haya mashindano, rais wa napoli alishawahi kuiponda afcon
 
Hahahaha halafu ukitaka evidence hakuna [emoji23][emoji23][emoji23]
Ukitazama mpira wao kwenye marudio ulikuwa wa ovyo tu [emoji23][emoji23] ila kutana na wazee wanavyousifia sasa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Afcon ya zamani ilikua tamu sana ukilinganisha na hizi za miaka ya karibuni. Tafuta marudio ya mechi za afcon moja hivi kameruni walikua wanavaa jezi hazina mikono. Ingawa nilikua bado mdogo lakini nakumbuka ulipigwa mpira mkubwa sana kwenye ile michuano
 
Ndiyo maana nilisema tangu mwanzo kucheza timu ya taifa ni uzalendo zaidi kuliko malipo. Jitihada za Mbappe timu ya taifa siyo kwa sababu analipwa posho kubwa sana, haifiki hata robo ya kile anacholipwa PSG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…