Miaka hiyo ya nyuma kama ni kutocheza vizuri, unaona ni timu moja au mbili ila nyingine kubwa zinacheza mpira. Ila mwaka huu wakubwa wote naona kama wanachechemea. Labda tuone gemu zinazofuata.
Ila hoja ya masilahi natofautiana na wewe. Huku national team huwa ni posho tu na huwa hawachukulii kama national team ni sehemu ya kujipatia hela. Hamna mchezaji asiyependa kuimbwa na wakwao. Hata huyo Salah kuna gemu kadhaa muhimu huwa analia wakishindwa. Hivyo hoja ya kutokufanya vizuri kisa masilahi haina mashiko. Labda ungesema mfumo pamoja na wachezaji wanaowazunguka wakiwa national team, sawa.