SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Huwa nina mawazo wakati mwingine nakaa nayo muda mrefu hadi wakati sahihi wa kuyatoa. Niwie radhi kwa uzi mrefu kidogo.
Katika miaka ambayo nimeangalia performances za timu za Africa katika Kombe la Dunia, nimekuwa najiuliza swali moja. Ingekuwaje timu za Afrika zingeunda mfumo wake wa kupata wachezaji wa timu zao za taifa ambao utatoa fursa ya kusajili wachezaji bora kutoka mataifa mengine ya Afrika ili kupata vikosi bora vya Afrika vinavyoweza kushindana na kweli kushinda kombe hilo? Wazo hilo lilinipelekea kuwaza kuwa na Ligi ya Mataifa ya Afrika.
Vilabu vya Afrika Kaskazini vimehodhi mpira wa Afrika, hasa katika ngazi ya vilabu. Kwanza vina vyanzo vikubwa zaidi vya pesa na pili vina watu katika ngazi zote za CAF kuhakikisha maslahi yao ndani na nje ya uwanja yanalindwa. Timu za Kaskazini zinashiriki hadi ligi ya Uarabuni ambayo inawaongezea pia misuli ya fedha.
Miaka fulani nchi kama Tanzania tulipata wazo la kupenyeza watu huko CAF tukawapeleka watu kama kina Said El-Maamry lakini binafsi sikuona mabadiliko chanya yenye faida kwetu maana sina uhakika kama alikuwa na ushawishi.
Nini kifanyike?
Moja ya njia zinazoweza kuleta usawa na ushindani wa kweli katika mpira wa Afrika, ni kuyafanya mashindano ya nchi ambayo sasa yanaitwa AFCON kuwa ndiyo ligi rasmi kuu ya soka Afrika. Ligi hii iwe kila mwaka ikianzia makundi na kwenda ngazi za mtoano hadi fainali. Baada ya makundi, ngazi za mtoano ziwe ni kwa timu kucheza mechi 3 (timu moja akishinda mechi mbili mfululizo, mechi ya 3 haifanyiki).
Faida zake ni nini? Nitataja kwa uharaka faida mbili tatu:
Kwanza, kawaida raia wa nchi automatically ni wapenzi wa timu ya nchi husika. Kwa maana hiyo, theoretically timu za nchi zina fan base kubwa kuliko vilabu. Kwa hiyo timu za nchi zikibustiwa, zikapewa sapoti za kifedha na wananchi wakapewa hamasa ya kusapoti kwa kununua jezi na kuja viwanjani, timu za nchi zina vyanzo zaidi ya kuzifanya kufanikiwa kuliko vilabu na hamasa itakuwa kubwa. Ukitaka kulijua hili angalia NFL (American Football) au NBA, ingawa baadhi ya majimbo hasa makubwa yana timu zaidi ya moja.
Pili, mfumo ninaopendekeza inabidi uondoe suala la uraia kwa wachezaji. Kwa maana hiyo nchi inaweza kusajili mchezaji raia wa nchi yoyote ya Afrika bila kuhitaji kubadili uraia wa mchezaji huyo. Restriction iliyopo sasa ambayo nadhani ni ya FIFA ambayo mtu akishachezea nchi fulani hawezi tena kuchezea nchi nyingine iondolewe au isitumike katika ligi hiyo, at least katika mashindano haya ya ndani ya Afrika.
In the long run, nadhani hii wazo itawaunganisha zaidi Waafrika na huko kwenye Kombe la Dunia tutaweza kupeleka timu imara zaidi.
Shida ni kuwa Afrika tunategemea sana pesa za FIFA na baadhi ya haya ninayopendeleza yanahitaji mabadiliko ya sheria za FIFA. Wakati mwingine Waafrika tunawekewa mitego halafu hizi nguvu za pesa zinatupumbaza tunashindwa kufikiri kile kilicho bora kwa maslahi yetu.