AFCON U-20: Je, Tanzania itafuzu hatua ya robo fainali?

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105

Michezo ya kundi C AFCON U20 kupigwa hii leo, ambapo Morocco itakutana na Tanzania huku Ghana ikikipiga dhidi ya Gambia.

Hii ni michezo ya mwisho ambayo itaamua ni timu zipi zitasonga mbele katika hatua ya robo fainali.

Ikiwa Tanzania itashinda mchezo dhidi ya Morocco na Gambia kuishinda Ghana, timu zote katika kundi hilo zitalingana alama ambapo zitakuwa na alama nne.

Kwahiyo kitakachoangaliwa ni tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Hivyo timu 3 yaani nafasi ya 1 mpaka 3 zitafuzu robo fainali hii ni baada ya matokeo ya mechi za leo

Hii ni kwa sababu Timu mbili za juu za kila kundi hutinga robo fainali pamoja na timu mbili bora za nafasi ya tatu.

Kwa upande wa kundi A timu mbili tayari zimefuzu yaani Cameroon na Uganda. Huku kundi B Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati zikisonga mbele kupitia nafasi ya kwanza na pili wakati Tunisia ikifuzu kwa nafasi ya 3 bora.
 
Kichwa cha mwendawazimu hakibebeki
 
Tanzania inaweza kufuzu na uwezekano ni miubwa sana kama itaifunga morocco hata goli moja.

Mpira wa ngorongoro sio mbaya sana, wana mpira mzuri sana.. Kocha akiwapanga vizuri wanatoboa.

1. Hakuna siku ambayo possesion imekua below 50%

2. Pass accuracy siku zote imekua above 50%

3. Wana talent za kutisha kama Kameta (Duchu) Laurent , Sopu , Kelvin, Vonatus Dismas ( timu yake ya wakubwa inacheza europa league), Ally Msengi, etc.

Wanacho hitaji ni kuongeza ushirikiano na akili ya maamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…