Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Michezo ya kundi C AFCON U20 kupigwa hii leo, ambapo Morocco itakutana na Tanzania huku Ghana ikikipiga dhidi ya Gambia.
Hii ni michezo ya mwisho ambayo itaamua ni timu zipi zitasonga mbele katika hatua ya robo fainali.
Ikiwa Tanzania itashinda mchezo dhidi ya Morocco na Gambia kuishinda Ghana, timu zote katika kundi hilo zitalingana alama ambapo zitakuwa na alama nne.
Kwahiyo kitakachoangaliwa ni tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Hivyo timu 3 yaani nafasi ya 1 mpaka 3 zitafuzu robo fainali hii ni baada ya matokeo ya mechi za leo
Hii ni kwa sababu Timu mbili za juu za kila kundi hutinga robo fainali pamoja na timu mbili bora za nafasi ya tatu.
Kwa upande wa kundi A timu mbili tayari zimefuzu yaani Cameroon na Uganda. Huku kundi B Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati zikisonga mbele kupitia nafasi ya kwanza na pili wakati Tunisia ikifuzu kwa nafasi ya 3 bora.