Afghanistan: Mamia wajitokeza ofisi ya kutoa passport baada ya Taliban kutangaza kurejesha huduma

Afghanistan wana deposit kubwa ya lithium duniani yenye thamani maelfu ya trilioni. Hao wamechukua nchi sasa hivi tu, mchina akiingia hapo soon utasikia watu wanazamia Afghanistan kutafuta maisha.
Unaweza kutuambia wapi mchina aliingia watu wakazamia kutafuta maisha, hata China kwenyewe hakuna anayeendapo na wenyewe tu wanakimbilia kwa wengine.
 
Marekakani ndiyo wamereta shida na co tareban ambayo nchi wameikuta iko na hali mbaya kiuchumi.
Lini Afghanistan ilikuwa na hali nzuri ya uchumi ukiondoa kipindi wamarekani walipokuwepo.

Hata wakati wa utawala wa kwanza wa Taliban kulikuwa na shida kibao, njaa na watu takriban milioni mbili walikuwa ni wakimbizi. Taliban ni shida.
 
Unaweza kutuambia wapi mchina aliingia watu wakazamia kutafuta maisha, hata China kwenyewe hakuna anayeendapo na wenyewe tu wanakimbilia kwa wengine.
Unafikiri nani anachimba mafuta Nchi za kiarabu? China ni major player kwenye Kampuni za uchimbaji. Ni kwamba tu hao jamaa wajanja wanajua kutumia rasilimali zao.

Hio lithium thamani yake ni matrilioni ya Dola hata kama kuna ufisadi kwa kanchi kadogo kama Afghanistan watatoboa.
 
Hujajibu nilicho kiongelea, uwepo wa China popote haumnufaishi mtu ni wao wenyewe kwa sababu ni watu wabinafsi sana.
 
Hujajibu nilicho kiongelea, uwepo wa China popote haumnufaishi mtu ni wao wenyewe kwa sababu ni watu wabinafsi sana.
Mkuu unaijua Trillioni dollar lakini? Trilioni kama 2300 za Kitanzania.

Tanzania budget yetu ni trilioni 30,
GDP ya Nchi kwa mwaka ni kama trilioni 150

Hivyo unaongelea budget ya Tanzania karibia miaka 70. Ni hela kubwa sana.

Wakiwa na mchimbaji muda utatuambia, watakuwa sio wenzentu.
 
Taliban wanaweza kuendesha nchi vizuri tu kama wataruhusu mambo ya kawaida ya maisha yaende bila kutumia ubabe.
 
Talibans kama Wana akili wangeruhusu watu kuondoka.Huenda hao diaspora wangeanza kutuma Hela nyumbani na kusaidia uchumi wa nchi.Ethiopia na Somalia zinajengwa na diasporas!
 
Amekwambia umwambie ni nchi gani China imewekeza watu ama Raia wakakimbilia kwenda kupata fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amekwambia umwambie ni nchi gani China imewekeza watu ama Raia wakakimbilia kwenda kupata fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali ambalo nimemjibu middle east.

China kampuni yao ya Serikali ya Mafuta inaitwa Sinopec unaweza kui Google ipo karibia Nchi zote Za mafuta, kuanzia za Kiarabu mpaka za Asia kama Brunei.

Nafkiri unafahamu Kampuni kubwa Kabisa ya mafuta Duniani ambayo pia inachuana na makampuni kama Apple, Saudi Aramco, sasa Aramco na Sinopec Zina Muungano unaitwa Yanbu Aramco kwa ajili ya Ku refine Mafuta,

Same kwa Nchi nyengine Soma huu Uzi jinsi China anavyo dominate refiners
 
Unachanganya madesa chief. Oil refinery unaweza kufanya popote pale sio lazima iwe nchi inayotoa mafuta. Makampuni ya uchimbaji mafuta ya magharibi ndio yaliyowekeza middle east na kuzifanya zile nchi kuwa matajiri, si hivyo tu hadi leo ukanda ule makampuni ya magharibi ndio yamewekeza sana na utalii asilimia kubwa wanategemea nchi za magharibi sio China.

Ni ukweli ulio wazi maeneo mengi aliyowekeza China wenyeji huwa hawaoni faida, anza na Afrika tu hapa Namibia kuna migomo inayoendelea kwenye migodi ya uranium waliyowekeza, Congo wamefunga migodi miwili kwa kukiuka sheria za mazingira na za kazi, Zambia ndio hao na Tanzania hapa sijaona uwekezaji wowote wa maana wa mchina zaidi ya yeboyebo, Myanmar na Cambodia kuna uwekezaji mkubwa wa China lakini bado wamechoka.

Tunataka mchina awe mbadala wa nchi za magharibi lakini ni wazi China wanajirudisha nyuma wenyewe.
 
Najua kuna narrative unataka kuiweka hapo, kwani haiwezekani China aka invest Nchi A wakafanikiwa na Nchi B wasifanikiwe?

Personally nawafahamu watu na makampuni ya Uchimbaji Mafuta Oman ya Kichina miaka na Miaka. Na naweza ku backup kwa data kibao


Pia hata hizo kampuni za West mfano BP nazo kwa asilimia kadhaa zinamilikiwa na wachina Huko middle East.

Na ni muda sana Makampuni ya Kichina ya Petroli yame overtake hayo ya magharibi



Kama una data zinazopingana na hizi zilete, ila sio hizi za kina Zambia.
 
Wanatia sana huruma, wakimbizi kwenye nchi yao wenyewe...

Ila wana roho ngumu hawa watu wakishafika nchi za wengine...
 
Mzee mafanikio ya Middle East hayatokani na China, hata hizo takwimu za makampuni makubwa huelezi kama hao petrochina na sinopec ndio wawekezaji wakubwa kwenye huo ukanda kwa leo. Hizo takwimu hazitaji operations za hizo kampuni ni wapi, na hiyo kampuni uliyoitaja inachimba mafuta Oman hatujui ina nguvu gani au ukubwa gani kwenye hiyo nchi. Tafuta takwimu zinazojibu maswali yaliyopo.

Labda nikukumbushe swali uliloulizwa ni kwamba utaje Nchi ambayo China amewekeza watu wakapakimbilia?

Kwanini hutaki tuizungumzie Zambia, basi tuongee kuhusu yanayoendelea Namibia.

China bado hana uwezo wa kuvutia watu wafanye kazi kwenye makampuni yao ni njaa tu ndio zinatufanya twende kwao. Tusiende mbali, taja kampuni yoyote ya kichina iliyopo Tanzania ambayo wabongo wanaikimbilia sababu ya maslahi mazuri?
 
Nature ya mbongo akipenda CCM basi wanavyofanya Chadema vyote Vibaya, Akipenda Chadema basi wanavyofanya CCM vyote Vibaya. Kwetu hakuna kati na kati.

Nchi ngapi Marekani AMEZIHARIBU? Nchi ngapi Uingereza Ameziharibu, Nchi ngapi Ufaransa Ameziharibu? Sababu wameharibu je ina maanisha investment zao zote zina madhara kwa Nchi?

Link niliokupa imetaja hadi Maeneo Gani PetroChina wanachimba mafuta OMAN, ila unaipotezea na kuuliza swali hilo hilo.

Na hata ukitumia akili ya kuzaliwa huwezi kumiliki kampuni mbili kubwa zaidi za mafuta Duniani kwa kupewa Vitenda uchwara,

Hizi links za Matenda Makubwa Makubwa yenye Thamani ya Matrilioni ya Hela ambazo PetroChina na Kampuni Nyengine za China wanafanya Duniani.

-moja ya eneo kubwa la Uchimbaji mafuta Iraq kwa sasa

-Qatar block D

-UAE karibia Block 3

-saudia

Kifupi mkuu China siku nyingi wapo Middle East na wanafanya Project kubwa kubwa. Hivyo si kweli kila eneo anakokwenda China wananchi ni masikini.
 
China bado hana uwezo wa kuvutia watu wafanye kazi kwenye makampuni yao ni njaa tu ndio zinatufanya twende kwao. Tusiende mbali, taja kampuni yoyote ya kichina iliyopo Tanzania ambayo wabongo wanaikimbilia sababu ya maslahi mazuri?
Tanzania kampuni gani kubwa ya China Ime invest? Kipindi cha ujamaa kulikuwa na urafiki, Tazara na Project nyengine kubwa hazikuwa zikitoa Ajira na watu kuajiriwa?

Hawa machinga wa China ambao wamejaa siku hizi hawawezi kuwa level moja na Multi Billion corporations.

Unapoongelea projects za Matrilioni ya Hela unatakiwa ufananishe na projects nyengine kama hizo duniani, na sio kufananisha kiduka cha mchina ama viproject uchwara ambavyo kampuni hata haijulikani kimataifa.
 
Unakwepa swali la msingi na unabadili taarifa kila mara. Kampuni ulizotaja kuwa zimewekeza hapo middle zina nguvu gani kuliko za magharibi au za waarabu wenyewe zilizopo hapo? Naona we umeleta tu kampuni zinazochimba huko lakini huelezi ukubwa wao kwenye hizo nchi?

Tuje kwenye mada, unataka kusema sasa hivi watu wanaenda middle East kutokana na huo uwekezaji wa mchina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…